Tume ya 'Operation Tokomeza' yadai Waziri Khamis Kagasheki na wenzie hawana hatia

Then nani anahusika basi?

Kama hao hawahusiki, tunataka watuambie ni nani anahusika basi kwa sababu kupitia operesheni hiyo watu waliumizwa, walidhalilishwa utu wao na wengine kupoteza maisha (kufa).

Ni rahisi tu, wawe hao au wasiwe hao tunachotaka ni waliohusika na unyama huo kuwa responsible and accoutable kwa matendo yao maovu!!
 
Kama hawana hatia nani mwenye hatia? walioteswa? walioumizwa?
Hii haisaidii kitu. Kipigo October kiko pale pale. Wasubiri tu waone cha moto toka kwa waathirika! Mangalichoti
 
Mda mwingine tuwe tunaacha kubwatuka tu tena mi naomba operations kama hiyo ije tena mana matunda yake tumeyaona na tunaendelea kuyashuhudia big up sana Kagasheki,endeleeni kubwatuka tu msimamo ndo huo
 
Uchunguzi wa Kamati ya Tume ya "Operation Tokomeza" Imebaini na kutoa taarifa baada ya uchunguzi kwamba Waziri, Balozi Kagasheki na Mawaziri wenzake hawakushiriki kabisa katika maafa yaliyotokea.

Na hivyo kujiuzuru kwao ilikuwa ni uwajibikaji wa Kisiasa. Ikulu imesema wanapaswa kusafishwa na kulipwa fidiai.

Ikumbukwe Balozi Khamis Kagasheki alijiuzuru wadhifa wa Waziri wa Maliasiri na utalii-tokana na kashfa hiyo ya 'Operation Tokomeza' huku Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Dr. Emmanuel Nchimbi na David Mathao walisimamishwa kazi.


Tujikumbushe kwa kupitia mada hii - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...bi-na-nahodha-watimuliwa-na-rais-kikwete.html


Tanzania bana, mtu aliyewajibika kisiasa anatakiwaje kulipwa fidia????

Nakumbuka hata Jairo aliambiwa na Luhanjo kuwa amesingiziwa na alipwe fidia, baada ya kurudi ofisini na mbwembe wote tunajua kilichotokea.

Bahati mbaya sana watawala ujiona wao ndiyo wenye haki tu, manake niliona huyo Ombeni alipoulizwa kama serikali itawalipa waadhirika wa matukio hayo alisema itaangalia kama iwape kifuta machozi ama la! Ona kwa hawa mawaziri ambao waliwajibika kwa haki eti walipwe fidia!

Kwanza walipwe na nani??? na

Ni kwanini walipwe???
 
Back
Top Bottom