Tume ya 'Operation Tokomeza' yadai Waziri Khamis Kagasheki na wenzie hawana hatia

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Uchunguzi wa Kamati ya Tume ya "Operation Tokomeza" Imebaini na kutoa taarifa baada ya uchunguzi kwamba Waziri, Balozi Kagasheki na Mawaziri wenzake hawakushiriki kabisa katika maafa yaliyotokea.

Na hivyo kujiuzuru kwao ilikuwa ni uwajibikaji wa Kisiasa. Ikulu imesema wanapaswa kusafishwa na kulipwa fidiai.

Ikumbukwe Balozi Khamis Kagasheki alijiuzuru wadhifa wa Waziri wa Maliasiri na utalii-tokana na kashfa hiyo ya 'Operation Tokomeza' huku Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Dr. Emmanuel Nchimbi na David Mathao walisimamishwa kazi.


Tujikumbushe kwa kupitia mada hii - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/572487-waziri-kagasheki-ajiuzulu%3B-david-mathayo-nchimbi-na-nahodha-watimuliwa-na-rais-kikwete.html
 

Attachments

  • FB_IMG_1431119031973.jpg
    FB_IMG_1431119031973.jpg
    42.6 KB · Views: 606
hii ndo tz unafikir ba liz anapenda ondok kwa bifu.
 
Najuta kuwa mtanzania mwenye akili timamu na umri sahihi huku nikishuhudia uongo na uzandiki wa uongozi wa nchi hii awamu ya nne.bora ningekuwa kichaa au mtoto mdogo wa umri wa chini ya miaka 5 nisingeyajua haya'
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa hiyo, muda anaotaka kuendelea kukaa hapa ni kuwasafisha mafisadi na wahalifu? AU anawasafisha mafisadi na wahalifu ili aondoe upinzani dhidi ya agenda yake ya kuendelea kukaa hapo? Ninaona mara kina maswi mara saa kagasheki,.

Ninasikika harufu ya Unkurunzinza wa kulazimisha majudge wafanye anachotaka ama la wa face consequences!. Harufu hiyo ninaihisi iko na hapa kwetu.
 
Najuta kuwa mtanzania mwenye akili timamu na umri sahihi huku nikishuhudia uongo na uzandiki wa uongozi wa nchi hii awamu ya nne.bora ningekuwa kichaa au mtoto mdogo wa umri wa chini ya miaka 5 nisingeyajua haya'


Mwalimu asingekufa, haya yote tusingeyaona!. Inaumiza kwa kweli. Sasa hivi wezi na mafisadi wote wanasafishwa maadamu ni wana ccm. Tenan wanasafishwa na mtu mmoja kwa udictator. Anatafuta nini katika unafiki na usaliti huo?

Ni kwamba aliwatuma wafanye yale na hivyo anajisikia guilty kuwatelekeza lazima tu awaokoe maana ni washirika wkae na pengine hiyo ndiyo sababu inayomfanya aanze kung'ang'ana kukaa hapo kidictator, hadi hapo atakapokuwa amewakoa wote na kumalizia maovu mengine aliyoyakusudia?

Ni kwamba anasaliti public interests na sheria ili ajipatie marafiki ili apunguze uchungu mioyoni mwa watu kusudi asipate upinzani kwenye nia yake ya kubaki hapo kinyume cha katiba ili kumalizia mengine anayoyajua yeye ambayo anauhakika hayana mashiko kwa taifa na hakuna mwingie atakayekubali kuyakamalisha? Ni yapi hayo kama si majanga zaidi kwa nchi?

NINAMKUMBUKA MWALIMU ALIPOSEMA, KATIBA YA TANZANIA ILIKUWA INAMRUHUSU HATA KUWA DICTATOR. SASA WATANZANIA YAMETUFIKA. TUNAFANYA NINI? NAOMBA TUPEANE MAARIFA.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Lembeli na wenzake ndiyo walipe hiyo fidia na washtakiwe kwa kuleta taarifa za uongo na kusababisha mitafaruku nchini! Pia na wananchi walioathirika vibaya na operation hiyo walipwe fidia stahiki.
 
Najuta kuwa mtanzania mwenye akili timamu na umri sahihi huku nikishuhudia uongo na uzandiki wa uongozi wa nchi hii awamu ya nne.bora ningekuwa kichaa au mtoto mdogo wa umri wa chini ya miaka 5 nisingeyajua haya'

Yaani inafikia hatua unajuta kuzaliwa tanzania
 
Lembeli na wenzake ndiyo walipe hiyo fidia na washtakiwe kwa kuleta taarifa za uongo na kusababisha mitafaruku nchini! Pia na wananchi walioathirika vibaya na operation hiyo walipwe fidia stahiki.

Watalipwaje,walipwe na nani? Unaambiwa hawana makosa
 
Siyo imedai bali ni kwamba uchunguzi wa kina umeonesha ukweli huo.
 
Ile tume ya Lembeli ilifanya kazi kwa visasi na chuki za wazi kabisa liko wazi sana jambo hili.
 
Ile tume ya lembeli ilikuwa na visa na chuki binafsi kwa akina kagasheki
Wadau mkumbuke watu walikufa,walijeruhiwa na kudhalilishwa,na watendaji walikuwa ni kwenye hizo wizara,sasa kuwaengua hao mawaziri hakukwepeki kabisa,sema kwa sasa jambo limekwishapoa,tujikumbushe watu walivyodhalilishwa kwa kusokomezwa majiti na kadhalika.Kaghasheki na Nchimbi wanahusika kwakua watendaji wa chini yao ndio waliofanya haya,yaani tunasahau ripoti na kuanza utetezi usio na tija,though hawakuwepo field ila watendaji wao ndo waliofanya haya.
Hivi kwanini tunaposema elimu inadorora tunasema Kawambwa mzigo,kwani yeye ndo anafundisha?ila yeye ni waziri mwenye dhamana.
So operesheni tokomeza isingewezekana kuwaacha hawa na haiwez kuwasafisha.
 
Lembeli na wenzake ndiyo walipe hiyo fidia na washtakiwe kwa kuleta taarifa za uongo na kusababisha mitafaruku nchini! Pia na wananchi walioathirika vibaya na operation hiyo walipwe fidia stahiki.
Mdau je hakuna watu walioathirika kwa hiyo operesheni?tuanzie hapo kwanza,na je kama wapo nani atawafidia hao waathirika?baadhi ya picha zililetwa hapa za watu kufanyiwa unyama
 
Ile operesheni ilisaidia kuleta nidhamu. Wale mawaziri wanastahili pongezi. Watz tuwe wakweli wakat mwingine ili itusaidie kupiga hatua. Walilileta heshima taifa. Kama tume imeona hilo tuwapongeze. They made a decision
 
Mwalimu asingekufa, haya yote tusingeyaona!. Inaumiza kwa kweli. Sasa hivi wezi na mafisadi wote wanasafishwa maadamu ni wana ccm. Tenan wanasafishwa na mtu mmoja kwa udictator. Anatafuta nini katika unafiki na usaliti huo? Ni kwamba aliwatuma wafanye yale na hivyo anajisikia guilty kuwatelekeza lazima tu awaokoe maana ni washirika wkae na pengine hiyo ndiyo sababu inayomfanya aanze kung'ang'ana kukaa hapo kidictator, hadi hapo atakapokuwa amewakoa wote na kumalizia maovu mengine aliyoyakusudia? Ni kwamba anasaliti public interests na sheria ili ajipatie marafiki ili apunguze uchungu mioyoni mwa watu kusudi asipate upinzani kwenye nia yake ya kubaki hapo kinyume cha katiba ili kumalizia mengine anayoyajua yeye ambayo anauhakika hayana mashiko kwa taifa na hakuna mwingie atakayekubali kuyakamalisha? Ni yapi hayo kama si majanga zaidi kwa nchi? NINAMKUMBUKA MWALIMU ALIPOSEMA, KATIBA YA TANZANIA ILIKUWA INAMRUHUSU HATA KUWA DICTATOR. SASA WATANZANIA YAMETUFIKA. TUNAFANYA NINI angkuwepo mwl cdm angekuwa ameifuta
 
Back
Top Bottom