Tume ya Mkandara yawachanganya mawaziri!

Kithuku

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,395
210
Wakuu mnafahamu nini kuhusu hii tume?

Tume ya Mkandara yawachanganya mawaziri
*Ni ile inayochunguza utendaji wao wa kazi

*Wasema inawakatisha tamaa katika kazi zaoNa Waandishi Wetu

TUME iliyoundwa kwa siri na Rais Jakaya Kikwete kuchunguza utendaji wa mawaziri wa wizara mbalimbali tangu awachague hadi sasa imewachanganya baadhi ya mawaziri kwa kushindwa kufahamu nini hatima ya nyadhifa zao.

Baadhi ya mawaziri sambamba na manaibu wao, ambao baadhi walionyesha kuchukizwa na hatua hiyo ya kuwekewa watu wa kuwatathmini, huku wakifafanua kuwa kitendo hicho kinawadhalilisha na kuwakatisha tamaa katika uwajibikaji wao.

"Unajua unapowekewa watu wa kukuchunguza bila kuwa na taarifa na kisha ukawabaini unakuwa na walakini na mwajiri wako. Sisi tunatazama lolote linaloweza kutokea maana uwaziri tuliukuta na tutauacha," waziri mmoja aliliambia gazeti hili.

Taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali serikalini zinaeleza kuwa, tume hiyo ilipewa siku 60 kukamilisha kazi hiyo na sasa ripoti inaandikwa kabla ya kukabidhiwa kwa rais.

Hivi karibuni gazeti moja la kila wiki lilichapisha habari kwamba ripoti hiyo imekamilika, lakini chanzo chetu kimesema bado kazi ya kuunganisha taarifa inaendelea na inaweza kukamilika katikati ya Februari.

"Si kweli kwamba ripoti imekamilika kama ilivyoelezwa huko nyuma. Tunachokifahamu sisi ni kwamba tume inaunganisha ripoti, maana ilipewa siku 60 kuanzia mwezi Desemba 2007," chanzo kimoja kilisema na kuongeza;

"Nakumbuka kazi hii ilianza katikati ya Desemba na kama nitakuwa sijakosea basi itakamilika katikati ya Februari 2008."

Kwa mujibu wa chanzo kingine; tume hiyo inayoongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandara, imemaliza kazi ya kupitia taarifa na uchunguzi katika wizara mbalimbali hadi sasa na kazi iliyopo mezani ni kuunganisha taarifa kisha kuzifikisha kwa Kikwete.

"Rais aliunda tume hiyo kwa siri, lakini si unajua nchi hii ilivyo sasa? Mambo yote yako wazi na sasa inafahamika. Sijui kama itaweza kufanikisha lengo maana wakubwa wanatazamana na wanaweza kuwafahamu wanaowachongea kama wakienguliwa," chanzo hicho kilidokeza.

Inaelezwa pia kuwa, usiri wa tume hiyo inayojumuisha vigogo wa juu katika Redet ulianza kupotea baada ya wajumbe hao kuanza kufanya ziara katika wizara mbalimbali na huko walikuwa wakiwahoji mawaziri na makatibu wa wizara hizo.

"Ninachofahamu kwa kweli kazi inaendelea, lakini ni kwa siri mno. Kazi hii inafanywa na vigogo wa Redet ni vigumu kubaini nini kilichomo, lakini siku zinavyokwenda tutapata ukweli," chanzo chetu kingine kutoka UDSM kilieleza.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani, tume hiyo iliundwa baada ya utafiti wa awali wa Redet kubainisha umaarufu wa Kikwete kuwa juu ya ule wa Baraza lake la Mawaziri.

"Rais aliamua kuufanyia kazi utafiti ule na ndio maana akaunda tume hii. Lengo ni kutazama na kupata taarifa za kitaaluma kuhusu baraza hilo na kama linakidhi haja iliyopo kwa wakati huu," chanzo chetu kilifafanua.

Profesa Mukandara alipoulizwa kuhusu suala la yeye kuongoza tume hiyo, hakukataa wala kukubali huku akisema; "aah sasa hayo...niulize siku,� alisema.

Baadhi ya vigezo vinavyotumiwa na tume hiyo katika kuchunguza ni pamoja na namna waziri anavyoonekana katika jamii, uwezo wake wa kutenda kazi, mafanikio aliyofikia tangu achaguliwe, nidhamu ya kazi na namna anavyoweza kumudu sifa za utawala bora.

Mwanzoni mwa Desemba mwaka jana, Redet ilitoa ripoti yake ya utafiti juu ya utendaji wa serikali na kubainisha kuwa utendaji wa mawaziri ulikuwa umeshuka, jambo ambalo wachunguzi wa mambo walisema mawaziri hao ni mzigo kwa rais na kumshauri afanye mabadiliko.

Source: gazeti la Mwananchi, 13 Jan 2008.
 
Watu walio wazembe utawajua. Kila siku huwa na hofu na kujishuku. Mimi kama nafanya kazi yangu kwa umakini na ufanisi kutimiza malengo ya mwajiri wangu, kwa nini nihofie kuratibiwa na "vivuli" nisivyoviona?

Kama ni kweli JK aliunda hii tume na atatekeleza matokeo ya tume kwa kuondoa Mawaziri wazembe, wavivu, mafisadi, wahujumu, wasiowajibika na wasio mahiri kuleta maendeleo ya Taifa, nitampa Tano ya nguvu!
 
Kuundwa kwa Tume kuchunguza utendaji wa mawaziri! hapa kuna mtu ambaye hafanyi kazi yake, hali inayompekelea Rais kuunda tume kuchunguza kile anachopaswa kuwa updated kila anapoingia ofisini. Labda pengine baraza la mawaziri la watu 60 ni kubwa mno kiasi linahitaji tume kulipima utendaji wake wa kazi.
 
Zoezi zima ni upuuzi mtupu. Rais kuunda tume ya siri kumtumia rafiki yake Mkandara na kujidai kuwa ni utafiti wa kitaalamu, ni uptezu wa fedha za umma bure. Mawaziri kujishuku pia ni upuuzi bure.
 
Kama nimeelewa sawa, kinachofanyika ni performance review ambayo kwa huku
nje ni kitu cha kawaida hasa kwenye private companies. Inaweza kufanywa ndani ya kampuni au kwa kutumia watu wa nje kama JK alivyotumia REDET.

Sidhani kama mawaziri wana sababu ya kuogopa hiyo review. Badala yake inaweza kugundua udhaifu wao na hivyo kuwasidia kujirekebisha. Lakini pia
inaweza kusaidia kuwaondoa baadhi yao.

Kama waziri na wizara yake wanachapa kazi, sioni sababu kabisa ya kuogopa.

Wakati hili baraza linaanza, JK alipita kila wizara na kuwaagiza nini walitakiwa kufanya (objectives) kwa wizara zao. Huenda sasa ndio wanapimwa kama wametimiza hizo objectives zilizowekwa.
 
Kwa Marekani, idara za serikali sasa hivi zina-implemet annual performance review. Na kama atafanya kweli sio matatizo ya matumizi ya review.
 
na hivi jamani kuna yoyote aliyesikia habari yoyote ya mabadiloko ya cabinet, mana tumesubiri mpaka tumeshachoka sasa. na hii tume ni upuuzi mtupu,hakuna lolote
 
Jamani kutokana na urithi wetu wa Utumwa yawezekana mwafrika hawezi kwenda bila fimbo!... Lol .
Na kwa taarifa zenu tu jamaa wanaenda mbio kishenzi maanake hawajui kabisa kama wapo ktk darubini ama huru. Sasa kama kiongozi akiwa na hofu ya namna hiyo hii ni ishara moja kubwa sana ya kuonyesha kuwa viongozi wetu wana walakini mkubwa sana na JK mwenyewe hata awe na baraza dogo kiasi gani hawezi kuondoa hulka ya urithi huo wa utumwa..yaani Kutojituma.
Na atafukuza wangapi ikiwa hulka hii imerithiwa toka Azimio la Zanzibar?...Chukua chako mapema.
Tunashindwa kabisa kujituma na kuwa waadilifu kuweka maslahi ya taifa mbele unless tunafanya kazi za watu binafsi tena basi wawe wahindi ama wazungu utaona uwezo wa viongozi wetu kufanya kazi kwa ufanisi. Cha kujiuliza ni hiki Je, Mhindi na Mzungu hawa jamaa hufanya kitu gani ambacho kinawafanya viongozi wetu wawe waadilifu kazini!....
 
Mkandara:

Do you remember The Piller from BCS forum?

Si upendi ujamaa, si kupenda JKT. Sikupendi karibu vitu vote alivyofanya Nyerere ukiondoa uhuru. Lakini kama wale alionao Nyerere wangefanya japo 50% tusingekuwepo hapa tulipo.

Viongozi wa Tanzania ni kama mafundi mechanics wanaopiga kelele na stori nyingi kuhusu utengenezaji wa mitambo lakini ukiwa spana waifanyie nini?
 
Mimi nafikiri hawa jamaa wamezidi na hizo tume zao. Kama mtu kachemsha mpige chini hakuna majadiliana. We have to be responsible sometime. Hakuna haja ya tume ni kutumia vibaya hela za umma.
 
Mkandara:

Do you remember The Piller from BCS forum?

Si upendi ujamaa, si kupenda JKT. Sikupendi karibu vitu vote alivyofanya Nyerere ukiondoa uhuru. Lakini kama wale alionao Nyerere wangefanya japo 50% tusingekuwepo hapa tulipo.

Viongozi wa Tanzania ni kama mafundi mechanics wanaopiga kelele na stori nyingi kuhusu utengenezaji wa mitambo lakini ukiwa spana waifanyie nini?

Sasa wewe unaanzisha ugomvi ngoja tuone....
 
Hivi kwanini viongozi wengi Tanzania wana hulka ya kuwa wazembe mpaka wasikie kuwa kuna tuzo fulani au bosi anakuchunguza? Je kweli JK alikosa watu wenye ujuzi wenye kujituma ili wawe mawaziri? Kweli hii "nepotism" ni mbaya sana na ingefaa JK aanze kuwaondolea uvivu akianzia na kiranja wake mkuu, Lowassa.
 
Bin Marium,

Haaa haaa haa kumbe Pillar, duh! Yes mzee wangu karibu tena hata hivyo Ujamaa bomba, JKT ilitufunza nidhamu na kuipenda nchi yetu huyo Nyerere wangu wala hana mfano.... haaa haaa haa!... baada ya kifo cha vitu hivi tu meli ikakosa dira.

Hapana mkuu wangu ebu turudi ktk reality hapa kisha nambie mwenyewe. Mkapa alikuwa nothing wakati wa Ujamaa na Nyerere lakini baada ya hapo umeyaona mwenyewe. Akina Mramba, Lowassa, Sumaye na wengine wote wakiwa ndani ya ngozi ya kondoo at least tuliwaona watu kwa sababu ya hivyo usivyovikubali. Kifupi hawakuweza kuiba mali zetu hata kama walikuwa mbwa mwitu.
Leo hii chini ya Ubepari Mkapa peke yake kakupua sii chini ya Billion 1 tena dollar acha hesabu ya mkewe, haya hao kina Mramba waliokuwa wakiishi zile flat za Aluminium leo hii ni ma Don wanaitwa real estate developer bila kutumia senti toka mfukoni. Huyo Mramba, Lowassa na Sumaye wana majumba mji mzima wa Arusha yaani wamegawana mitaa..Hapo dar ndio usiseme, sasa uncle kweli unaweza sema haya yametokana na Ujamaa ama Nyerere?... au una maana ukimzuia sana mtoto basi mwisho wake akija onja dunia ni lazima atakuwa limbukeni wa kila kitu.
Mimi nasema hivi, sikubaliani kabisa na Azimio la Zanzibar na kama kweli tungeweza fanya hata 50% ya Azimio la Arusha kwa kutumia Utandawazi na soko huria basi leo hii Tanzania tungekuwa hatushikiki kabisa.
 
Sasa perfomance review ya Rais anafanya nani? Kama ni sisi wananchi I will give 20%
 
Kwanza mtu mwenyewe anayefanya kazi hiyo ya uchunguzi wa mawaziri tena wa siri eti ni"mkandara" wote tunajua mkandara ni mshikaji wa kikwete, vile vile mkandara ana ushikaji fulani na mawaziri wengi. Hivyo sidhani kama report atakayotoa either ya kumlinda au kumlima waziri fulani hata kama ina itilafu juu ya ukweli JK hawezi kuikataa. Mkandara mwenyewe naye ana yakemaana wanaomjua mzee huyu hana biashara, lakini ana majumba kibao kila kona ya bongo anapangisha mizungu tu. Kwa mshara wake wa chuo kikuu hata kabla ahalamba position mpya hawezi kuwa na utajiri alionao. Kwa hiyo naye ana kaufisadi kengine kwa kushirikiana na dili za serikalini. Yeye alikuwa mshauri wa masuala ya politics na uchumi kwa Kikwete kwa muda wote kabla kuepwa hiki cheo, aliyomshauri kikwete hasara wote tunaziona.
Hii tume sidhani kama itasaidia chochote.
Kikwete mwenyewe ana macho ya kuona...anaweza akaangalia ni waziri gani hafanyi kazi vizuri kama alivotaka yeye maana alishawapa semina na kutumia pwesa nyingi ya walalahoi. Sasa kama hawakufanya kile alichotaka wafanye hapo sionin haja ya tume..nni yeye kuwawajibisha tu. Kuna baadhi ya vitu viko wazi na yeye rais anaviona. Tume zisifikie wakati ikawa dili kwa TZ. Wapelelezi wa Tanzania wanafanya kazi gani...za kiusalama tu? Kazi nyingine ni hizo..waingie huko mawizarani wafanye kazi ya kuwapeleleza hao mawaziri kwa kutumia proffesional zao. Tume ya mkandara nni bomu kwani naye ni fisadi wa kisiri.
 
Jamani eeeh! Mukandara na sio Mkandara... acheni kuchafua jina kubwa. Heee heee heee!
 
Back
Top Bottom