" 1. Imuulize Prof. Jumanne Maghembe sababu za kufuta FORM TWO ZONAL EXAMINATION
2. Wachunguze iwapo mitaala mibovu iliyopo inaeleweka au la."
MASWALI YA MSINGI: JE!? A. Kuna MTAALA WA ELIMU!? B. Maghembe ni kiongozi au free rider kama walivyowengi ndani ya ccm!!? Maghembe alifanya nini kwenye wizara alizotoka!!!? C. Kwanini tusiige mambo ya msingi yanayoweza kusaidia kuiongoza nchi badala ya mambo yanayowagharimu wananchi!!!?
D. Kibovu ndo kizuri tanzania, lini hili litabadilika!?
A. How can we easily forget so soon that Education Minister failed to answer the question on the same from Mr. Mbatia (MP)!? How!!!? How can someone ask such a question!!? Waziri hajui kama kuna mtaala wa elimu, raisi hajui (kwa sababu waziri wake hajui). Mkurugenzi mstaafu wa Elimu ya Sekondari akihojiwa kwenye kipindi cha Hamza Kasongo Hour alisema hakuna mtaala wa elimu! Badala yake kuna silabasi zinazotumika kuongozea, lakini mfumo hasa bado haujawekwa wazi, ndio sababu wakija free riders (viongozi vihiyo wa uongozi) wanaichezea ofisi husika na kubadilisha miongozo dhaifu iliyopo kama wanavyotaka kama maghembe, mungai ... Matokeo mabovu ya Form 4 yalipotoka Ndalichako kwa werevu wake kakimbilia kwenye vyombo vya habari kuonyesha vikatuni, ulipoulizwa mtaala wa Elimu Tanzania hakuonekana kwenye vyombo vya habari! Swali, je? ni kazi yake kuonyesha vikatuni kwa wananchi!? Jambo la msingi kwake ni lipi!? Au alifikiri anamfurahisha nani!?
B. Speaking about Maghembe, m'bunge mwongo kama wenzake wengi, anayedanganya wananchi mchana kweupe, alipoowambia wananchi wa Goba kuwa maji yatatoka baada ya siku tatu, bila kujali akijua kuwa watu wa Goba kama walivyo majority ya Watanzania, lao kudanganywa, huku akitumia fedha za walipa kodi, hajawai kufanya jambo la maana ambalo hata yeye atalikumbuka maishani mwake kama kiongozi. Unakwenda unawaambia watu maji yatatoka baada ya siku 3 halafu wiki inakwisha hakuna maji, wakikufuata utawajibu nini? Au hao walikuwa mamluki waliopelekwa na malori kuongeza umati wa watu!!!?
B1. Alipokuwa wizara ya elimu ndo kama ilivyotajwa hapo juu. Akiwa wizara ya kilimo na chakula alifanya kazi nyingine ya kijinga isiyo na tija kwa taifa kwa kulazimisha wakulima kutumia mbegu ambazo ukipanda ukavuna huwezi tena kuzirudia kupanda kama ilivyokuwa traditional farming, badala yake inabidi uende tena dukani ukanunue mbegu za kupanda, sasa ikiwa bei dukani haiendani na mfuko wako, basi utapanda mwakani au kidogo. Wakati hapo awali hakukuwa na haja ya kuhangaika kununua mbegu kwani mkulima nageweza kujitengea mbegu kutoka kwenye mavuno yake. Kila baraza la mawaziri likitajwa na huyu jamaa yupo nasema kweli raisi yupo maana kama mawaziri wanachaguliwa kwa utendaji, basi labda utendaji m'bovu ndio kigezo cha kuwa waziri na hili linadhihirishwa kila uchao Tanzania.
NB: Tanzania inahitaji chombo maalum, mbali na Rais wa nchi kuchagua baraza la mawaziri na wasiwe wabunge ili iwe rahisi kwa bunge kuwawajibisha mawaziri na kusiwe na kukingiwa kifua na rais kwa sababu binafsi zisizo na manufaa kwa wananchi kama ilivyo sasa.
C. Kama serikali ya awamu hii imeweza kuiga baadhi ya miundo mbinu ya nje mfano barabara, majengo, na kulazimisha mambo mengi ya nje yasiyo na faida kwa wananchi wengi mbali ya kuwakandamiza kwa faida ya wajinga wachache, nini kimeshindikana kuiga mifumo ya uendeshaji wa vyombo maalumu vya nchi kama Bunge, Mahakama na Dola (kuiga wenzetu kama America, Europe, ...) ambapo huwezi kuhonga wala kula rushwa kirahisi. Eti kukimbilia kuiga barabara zao, mitaa yao ... wenzetu wana system yakinifu zisizo ruhusu mianya ya ukandamizaji inayopelekea kuibuka wala rushwa hatimaye mafisadi. Hayo inabidi yaigwe ili kuwadhibiti watu dhaifu wanaopata free ride kwa jina la 'kiongozi' huku hajui maana ya kuwa kiongozi kama hao kina maghembe.
D. Tanzania ya sasa imekuwa kibovu ndo kizuri. Hapo kabla (kabla ya kibaya kuwa kizuri) mwanafunzi akifeli haendi shule ya serikali badala ya anatafutiwa shule ya private. Leo kwa wenye uwezo hata mwanae akifaulu hampeleki shule ya serikali kwa sababu hakuna kinachoeleweka, anampeleka private.
Ndalichako badala ya kupeleka Mtaala wa Elimu kwenye vyombo vya habari usomwe na wananchi, anapeleka vikatuni Why!!!? Spika wa bunge la wananchi anakataa hoja zinazotetea mahitaji ya wananchi na kutaka kulificha bunge la wananchi kama ni kitu chake. au cha aliyempa madaraka. DPP amekalia kesi za mafisadi halafu yupo bize siju na kazi gani? Yani alimradi tu nchi inakwenda kusiko, au inarudi nyuma.