NECTA na TIE ni tatizo kwa Elimu yetu

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
24,474
34,515
Mimi ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa sehemu fulani hapa nchini.

Jana nilipata ugeni wa mwalimu mkuu msaidizi wa shule moja kutoka Kata ya jirani na kata yetu. katika mazungumzo naye tulijadili changamoto zinazoikabili sekta ya elimu na namna serikali inavyoshiriki kutatua. Ingawa katika mazungumzo yetu ilionekana kuwa viongozi wengi wa serikali wanafanya siasa kwenye utatuzi wa changamoto za elimu.

Nilimuuliza swali kwamba, kwa wastani wa ufaulu ni asilimia ngapi ya wanafunzi wanaoendelea mbele kwa masomo kwa alama za ufaulu? na pia pale shuleni kwao wanafunzi waliopokelewa ni wangapi wanaofanikiwa kumaliza kidato cha nne? Katika majibu yake niligundua kwamba karibia asilimia 40 wanaishia njiani. Sababu zipo nyingi lakini kubwa iliyonistua ananiambia wanafunzi wengi wa kike wanaandika barua za kuacha masomo kwa hiyari zao na wanazo hizo barua.... Pia anasema yeye na shule za wilaya yao wanakwama katika kuinua taaluma vizuri kwa sababu Afisa Elimu wa Wilaya ni kikwazo kikubwa na hana ubunifu na hataki ubunifu wowote katika sekta hiyo.
Enewei maongezi yalikuwa marefu sana ukichukulia mwalimu huyo ni ke na hakika kichwani yupo vizuri alikuwa ananihamasisha sana kufunguka kwenye agenda hii.

MTAZAMO WANGU
Tanzania Institute of Edecation - T. I. E. (Curriculum developer)

Hivi majuzi tumeshuhudia namna TIE walivyotia aibu kwa kutunga vitabu vilivyo chini ya kiwango na kuvisambaza mashuleni... Lakini hili tatizo la juzi ni matokeo ya uwekezaji wa hovyo kwenye elimu unaofanywa na viongozi wetu na kwa kushindwa kusimamia vyema sekta ya elimu. TIE ni Taasisi ya Ukuzaji Mitaala ndiyo ambayo inatunga mitaala yote ya elimu ya chekechea, msingi na Sekondari nchini. Ina wataalamu lukuki na wabobezi katika eneo hilo. Kwa namna ilivyoundwa ndiyo tuseme ni regulator wa elimu kwa kutunga mitaala inayotumiwa katika mashule yetu. Ingawa sijajua nguvu zake kwenye shule za binafsi maana nyingi za shule hizo wanatumia mitaala ya nje...
Tatizo linakuja pale ambapo Taasisi (Tanzania Institute of Education) imelazimishwa kufanya biashara ya uchapaji wa vitabu vya kiada na kuingia kwenye soko la ushindani. Tatizo hili si dogo na limepelekea kuua morali ya wachapishaji huru na hata kufifisha soko la vitabu nchini.
Kwa nini serikali isiifufue TPH (Tanzania Publishing House) na ikaendeshwa kwa ubia wa private publisher na serikali kwa upande mwingine? Hivi TES (Tanzania Elimu Suppliers) ilikufanye ilihali ilikuwa inafanya vizuri sokoni?
Sasa hili la TIE nadhani ni wrong kuiruhusu kushiriki ushindani wa soko la vitabu wakati yeye ni msimamizi wa mitaala hiyo.
Ninakumbua mwishoni mwa miaka ya 90 nilibahatika kufanya kazi na TIE kama private consultant. Kazi ilikuwa ni kuandaa vitabu kwa level ya darasa la tatu hadi la saba. Lakini mitaala ambayo waliitunga wao wenyewe iliwapa wakati mgumu sana kuitafsiri kupitia vitabu hivyo. Nikagundua kwamba Wakuza Mitaala wakati ule walifanya kunakili mitaala kutoka nchi zingine na kuitafsiri hivyo suala la ubunifu halikuwepo. Na mingi ya mitaala hiyo tuliyoandikia vitabu ilikuwa migumu kwa waalimu kuifundishia.
Kuna wakati fulani Rais Mkapa alitoa agizo mitaala hiyo itengenezewe Teacher's mannual ikafundishwe vyuo vya ualimu. Nilishiriki kutengeneza vitabu vile kupitia kampuni ya Macmillan Tanzania na sijui kama vitabu viliwahi kutumika kwani it waz complex indeed naamini pesa ililiwa bure na wahusika waliopaswa kuchapisha.
Sasa naijadili NECTA kisha nitatoa mapendekezo yangu mwishoni.

National Exmination Council of Tanzania - NECTA
Baraza la Mitihani la Taifa limekuwepo na limekuwa linatekekeza majukumu yake ya kuwapima wanafunzi na kupanga viwango vya ufaulu. Kazi inayofanywa na Baraza ni nzito na inahitaji kuwapongeza kwa dhati.
Kutunga na kusimamia mitihani nchi nzima ni sawa na Tume ya Uchaguzi kuendesha uchaguzi na kukamilisha kutoa matokeo ya kura. Lakini Baraza limekuwa linajitahidi kutekeleza wajibu wake hata kwenye mazingira magumu huko vijijini ambapo mawasiliano ya barabara ni mtihani mwingine wa Taifa.
Pamoja na pongezi hizi, nimeona kuna jambo au maeneo ambayo Baraza la Mitihani wanakosea. Kwanza ukitoa ukaribu wa kupakana majengo baina yake na TIE sijaona kama wanashirikiana pamoja kukuza ama kuendeleza elimu nchini.
Watunga mitaala wanatimiza wajibu wao na mitaala ikishatungwa husambazwa kwenye Halmashauri zetu na Maafisa Elimu wanasimamia utekelezwaji wa mitaala hiyo kwenye mashule yetu ndiyo maana tunapata wakaguzi wa elimu na waratibu elimu. Waalimu wanaitumia mitaala hiyo kuandalia masomo (Lessons Plan) na zana za kufundishia.

Lakini hakuna hata siku moja ambapo TIE wala NECTA walifanya tathmini kuwa ni kwa kiwango gani mitaala imekuwa inafikiwa lengo na kwa asilimia ngapi. Unakuta wilaya nzima ina upungufu wa waalimu wa Sayansi au masomo kadhaa na wanafunzi ama shule nyingi hawajasoma masomo ya mchepuo fulani kutokana na upungufu wa waalimu na hilo lipo wazi kabisa. Lakini bado NECTA watapeleka mitihani huko kuwapima wanafunzi kwa masomo wasiyosoma. Huu ni uonevu na upungufu mkubwa.
Pia NECTA imekuwa mstari wa mbele kuchuja wanaopaswa kuendelea na masomo na haina mpango na walioshindwa kufikia lengo la alama zinazohitajika.

USHAURI WANGU
NI vizuri kabla mitihani haijafanywa kuwe na possible assessment ya kutosha kushawishi wanafunzi kufanya mitihani kwa masomo husika. TIE washiriki kufanya tathmini kujua changamoto za ufundishaji na kukamilisha mitaala ili kujua kama lengo limetimizwa na kuisaidia kuishauri NECTA kuangazia maeneo na aina ya mitihani wanayoweza kutunga. Ni upotevu wa rasilimali kuwatahini wanafunzi kwa masomo ambayo siyo tu yana upungufu wa waalimu lakini hawakusoma kabisa.

Ninashauri vyombo hivi viwili viboreshwe

  1. TIE wabaki katika kutunga na kuendeleza mitaala kwa shule zetu, lakini waende mbele zaidi wawe na udhibiti wa mitaala inayofundishwa shule zisizo za serikali... Nimewahi kushika chaki na hili nalijua kwani wanafunzi wa baadhi ya shule hizi hufanya Mtihani wa Taifa optional na si lazima kwani wanakuwa washafanya mitihani ya mitaala wanayofundishiwa
  2. TIE wasiruhusiwe kushiriki utunzi wa vitabu vya kiada, Maana yake ni kwamba hata developer wa Curriculum wasiruhusiwe kutunga vitabu labda tu anapokuwa siyo muajiriwa wa TIE.
  3. TIE wafanye tathmini ya mara kwa mara kuhakikisha kama mitaala waliyoitunga inaendana na ulimwengu wa sasa. Hatuwezi kuwa na mitaala ya miaka ya 80 ili kupata wataalam wanaoweza kuingia kwenye ushindani wa soko huria.
  4. NECTA ifumuliwe na kubadilishwa kimfumo ambapo badala ya Kuwa baraza la Mitihani pekee liongezewe kipengele cha continuity. Kwa mfano wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na uhafifu wa alama za ufaulu ni vizuri wakaingizwa katika mfumo wa NACTE. Hili linaweza kufanyiwa study ya mfumo wa Elimu wa Ujerumani ambapo baada ya mchujo kunakuwa na mwendelezo wa waliofeli pia.(Sisemi sana hapa ni somo refu)
  5. NECTA iwe huru kiutendaji kwani mara nyingi maamuzi ya kisiasa yanakuwa ni kikwazo kutekelez wajibu wake. Ikumbukwe sakata la watu wa dini fulani waliinuka kudai vijana wao wanaonewa kwenue usahihishaji mitihani na kusababisha kutopata alama za kutosha. Hili liliamuliwa kisiasa.
  6. Ajira na job descriptions za maafisa elimu Wilaya na Mikoa ziangaliwe upya. Kama hakuna creativity na tija inakuwa automatically way out kwa hao watu.

Kwa kumalizia.
Tuna Maktaba kuu na Makataba za mikoa hadi wilaya. Je vipi kuhusu MAABARA? vijana wetu ambao shule zao hazina maabara ama zipo na zina changamoto wa zana basi wawe na mahala pa kwenda kufanya majaribio yao.
Tatizo ni kwamba Mkemia mkuu anajiona hana mchango mkubwa wa kukuza elimu nchini ilihali yeye ndiye mtafiti mkuu wa kisayansi nchini (tafsiri yangu)


Nimesema
 
Safi Mdau, NECTA na TIE fanyieni kazi huo ushauri please.!
Hapo kulikuwa na kamati inaitwa EMAC ambayo imeshavunjwa lakini ndiyo iliyofanikisha kufifisha tasnia ya uchapishaji vitabu nchini.
Bado TIE wana uwezo wa kuregulate na kutoa ithibati ya vitabu vinavyokidhi mitaala
 
Msanii umesema vizuri sana ila kusema NECTA itunge mitihani kikanda eti kwa kua kuna watu hawajasoma somo flani si sawa.
 
Asante Msanii kwa uzi mujarab. Kipengele kimoja tu ambacho ningependa kuchangia ni hiki--- Umesema : //Tatizo linakuja pale ambapo Taasisi (Tanzania Institute of Education) imelazimishwa kufanya biashara ya uchapaji wa vitabu vya kiada na kuingia kwenye soko la ushindani.// ----------- ninavyoelewa ni kuwa hawana ushindani. Wao ndio wametamkwa kuwa ni PEKEE walio na ruhusa kuandika vitabu vya kiada. Kwa hiyo, kuna zero ushindani. Na hilo hasa ndilo tatizo kubwa. Ingekuwa vema na haki kama huo ushindani ungekuwapo, kisha EMAC iachwe ifanye kazi yake. Yaani, waandishi binafsi waandike, TIE waandike wakitaka - kisha pande zote mbili zikaguliwe na EMAC kwa usawa. Asiyefaa atupwe nje bila kujali ni Taasisi au si Taasisi. Msingi uwe kwenye kusimamia viwango.
 
Feza boys wanapiga mtihan mmoja na tegetelo secondary school yenye mazingira mabovu, walimu wachache hivi unategemea nini?
 
Msanii umesema vizuri sana ila kusema NECTA itunge mitihani kikanda eti kwa kua kuna watu hawajasoma somo flani si sawa.
Mheshimiwa nilimaanisha hivi...

Kabla ya kutunga mitihani wapitie tathmini ya taarifa kutoka kwa maafisa elimu wilaya na kukagua ni kwa kiwango gani shule nyingi zimefikia katika kukamilisha mtaala husika. Na ikionekana kuwa asilimia kubwa ya shule walifikisha 60% ya ufundishaji (mtaala) basi hao asilimia 40 ambao walifikisha kiwango cha asilimia kubwa ya hapo wasiwe ndiye kigezo cha margin ya mtihani bali mtihani utungwe kwa kuzingatia uwezo wa hao 60% hapo haki itakuwa imetendeka...

Lakini ili hili lisitokee ni vizuri NECTA ikawekewa sharti la kuratibu continuity ya waliokosa alama za ufaulu kwa kuwapatia elimu ya ufundi ambayo kiwango chake cha juu ni diploma na endapo mtahiniwa akifaulu diploma hiyo kwa GPA ya Upper Second basi anaweza kurejeshwa katika mfumo wa TCU...

Hii itasaidia kuondoa jeshi kubwa la wanaokosa elimu kwa kigezo cha kuchujwa na mitihani ya NECTA....
 
Naandika haya kwa sababu ninapata uchungu mkubwa huku mtaani ambapo mimi ni Mwenyekiti wa Mtaa nina vijana ambao hawana mbele wala nyuma na hakuna prog yoyote kuwasaidia na hawana msaada zaidi ya kutumbukia kwenye makundi hatarishi...

Kukosa elimu haina tofauti na kukosa msimamo
 
Back
Top Bottom