Tume Mipango yamfunda Mbowe

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
SIKU moja baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), kudai kuna uvunjifu wa sheria katika uhamishaji wa fedha zilizoidhinishwa na Bunge, Tume ya Mipango imetoa ufafanuzi na kusema hakuna sheria iliyovunjwa.

Aidha, Mbowe na wabunge wa kambi ya upinzani wametakiwa kwenda kuisoma upya Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 ili waielewe badala ya kuupotosha umma.

Akizungumza na gazeti hili mara baada ya kuzinduliwa kwa Kitabu cha Muongozo kuhusu wa Usimamizi Rasilimali za Umma, Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Mipango, Florence Mwanry alisema madai yaliyotolewa juzi na Mbowe bungeni si ya kweli.

“Wabunge ndio walipitisha wenyewe Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015, ambayo inafafanua kuhusu uhamishaji wa fedha kutoka kifungu kimoja kwenda kingine, hivyo uhamisho wa fedha uliofanywa uko sahihi na hakuna sheria iliyovunja, wakaisome vizuri,” alisema Mwanry.

Mbowe akizungumza na waandishi wa habari juzi baada ya kususa Bunge, alitoa mfano wa bajeti ya maendeleo iliyoidhinishwa na Bunge kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2015/16, iliyokuwa ya Sh bilioni 883.8, ambapo kati ya fedha hizo, fedha za ndani zilikuwa ni Sh bilioni 191.6.

Alisema inashangaza kuwa hadi kufikia Machi 2016, Wizara ilikuwa imeshapokea kutoka Hazina Sh bilioni 607.4, ambazo ni fedha za ndani, tofauti na ilivyopangwa kuwa fedha za ndani ni Sh bilioni 191.6. Mbowe alidai kuwa hiyo inaonesha kuwa kuna ongezeko la fedha zilizotolewa na Hazina hadi kufikia Machi 2016, ikilinganishwa na fedha zilizoidhinishwa na Bunge.

Akitoa ufafanuzi, Mwanry ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Mipango, alisema Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015, inamruhusu Ofisa Masuhuli kuhamisha fedha kutoka kifungu kimoja kwenda kingine, ili mradi asivuke asilimia saba ya bajeti nzima.

Kadhalika, kwa upande wa Waziri, alisema sheria hiyo inampa uwezo wa kufanya uhamisho wa fedha kutoka kifungu kimoja kwenda kingine ili mradi asizidi asilimia 10 ya bajeti na katika uhamisho uliofanywa na wizara tajwa, mambo hayo yamezingatiwa.

“Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ni wizara yenye madeni mengi ya wakandarasi na ni moja ya wizara zinazotumia fedha nyingi kwenye masuala ya miundombinu, sasa ni lazima madeni hao yalipwe na Serikali haiwezi kuacha kuyalipa kwa sababu kadri yanavyobaki, ndivyo riba inavyoongezeka,” alisema Mwanry.

Alisema pamoja na uhamisho uliofanywa ndani ya wizara hiyo, bado fedha zilizohamishwa ziko ndani ya kiwango kinachotakiwa kisheria na bado ni kiwango kidogo ambacho hakijavunja sheria.

Habari Leo
 
Hivi wanapata wapi mda wa kumjibu mtu kama mbowe ambaye uelewa wake sawa mwanafunzi wa darasa la tano c, uelewa wa mbowe ni mdogo sana yeye mda wote anafanya siasa tu.
 
Mbowe form six kilaza tu
Kwanza muda wote wanasusa hawezu kukumbuka kama kuna sheria ilipitishwa 2015
 
Only in Tanzania wanapoteza mda kujibu watu wasiojielewa!
Demokrasia ni kumsikiliza kila mtu mawazo yake na mwisho wa siku mnapata muafaka.Kila Mtanzania ana haki yakikatiba yakusikilizwa na kuheshimiwa kama mnataka hii nchi iende mbali acheni ushabiki wa vyama vya siasa,tuwe na mitazamo ya maslahi ya kitaifa
 
Hata kama Sheria ingekuwa hairuhusu, kwa kuwa uhamisho huo umefanywa kwa maslahi ya Taifa hakuna tatizo!!

Kwa hiyo Mbowe alitakiwa Wakandarasi waendelee kufa kwa magonjwa ya moyo wakati wao walikopa bank ili watekeleze miradi ya Taifa, na Serikali ya JK. haikuwa inawalipa ni hadi alipoingia Magufuli ndipo akaanza kuwalipa haraka ili madeni hayo yasiendelee kuzalisha riba!!!

Hivi hawa UKAWA jamani ni vipi? kwani Tundu lissu hakuwepo Bungeni awasaidie?
 
Only in Tanzania wanapoteza mda kujibu watu wasiojielewa!
KWANI UMEONA ALICHOKIJIBU?
AU WEWE NI MOJA YA ZILE PRODUCTS ZA VYUO VIKUU MAJINA?
MTU anapoamua kusema kwamba mwenzake amepotosha uma, lazima aweke vifungu anavyosema vinamlinda huyo aliyefanya kitendo cha kuhamisha matumizi ya budget,
Alivyowaajabu anasema sheria ya mwaka 2015 inaruhusu kufanya hayo et wakasome vizuri,
SHERIA IPI?
NB: nakubaliana asilimia 100 na alichokifanya Mh Rais na Bunge pia kwani wakati huu ni tofauti na uliopita, ilimradi hizo hela ni productive, hazijachukuliwa kwenda kuwanufaisha wachache na mafisadi, ni sehemu ya maendeleo ya nchi.
Na ili nchi ipige hatua maamzi hama hayo ya serikali ni mhimu sana.
 
Sijaona citation ya vifungu hapo while mbowe aliainisha vifungu vilivyokiukwa.
Pombe amejaliwa vilaza wengi sana kwenye serikali yake.
Halafu ni maelezo ya kiupuuzi tu hayo.
Lengi la juhamisha fedha ni ili kufukia mapeango au kukabiliana na dharula iliyojitokeza, sasa hapa ni kinyume eti wamepewa bajeti ya shilingi bilioni moja, wanakwenda kuhamisha shilingi bilioni 500, yaani mara tano ya bajeti halisi.
Huku si kuwaona watu kama maounguani tu!!!
 
Sijaona citation ya vifungu hapo while mbowe aliainisha vifungu vilivyokiukwa.
Pombe amejaliwa vilaza wengi sana kwenye serikali yake.
Nyumbu kweli wewe,unataka mpaka umezewe? Umeshaambiwa reference lakini mpaka uandikiwe citations,tatizo la kuzoea misaada,au unataka na hili wahisani waje wakusomee? Kaa ukisubiri citation bila kujishughulisha.
 
Sijaona citation ya vifungu hapo while mbowe aliainisha vifungu vilivyokiukwa.
Pombe amejaliwa vilaza wengi sana kwenye serikali yake.
Ebu nionyeshe kifungu alicho quote Mbowe kwenye suala la bajeti?Mbowe aliitaja hiyo sheriq ya bajeti kuwa inakata mafungu kuhamishwa, ndio anafundishwa hapa kuwa hajaielewa sheria ile na ameshauriwa akaisome vizuri maana inaruhusu kuhamisha mpaka 10% ya kiwango kilichopitishwa na Bunge bila kuhitaji ruhusa ya bunge.
 
Halafu ni maelezo ya kiupuuzi tu hayo.
Lengi la juhamisha fedha ni ili kufukia mapeango au kukabiliana na dharula iliyojitokeza, sasa hapa ni kinyume eti wamepewa bajeti ya shilingi bilioni moja, wanakwenda kuhamisha shilingi bilioni 500, yaani mara tano ya bajeti halisi.
Huku si kuwaona watu kama maounguani tu!!!

Ebu soma kifungu vizuri, bajeti ya wizara ni Billion 800 na wamepewa Billion 600 tu.
 
Back
Top Bottom