Tume Mipango yamfunda Mbowe

Tume Mipango yamfunda Mbowe

Sijaona citation ya vifungu hapo while mbowe aliainisha vifungu vilivyokiukwa.
Pombe amejaliwa vilaza wengi sana kwenye serikali yake.
Wenye elimu ya hapa na pale ....nenda kaisome huo muongozo usingoje kutafuniwa
 
mbowe ni mtu wa sayari nyingine kumjadili humu mi kupoteza muda . ona sasa mbowe alipoongea aliweka na vifungu vilivyokiukwa ina maana alikuwa na data hivyo aliiweka hoja yake kisayansi zaidi , aliyekuja kujibu kajibu kisanii zaidi hata data
moja hajaweka, huu ni usanii tu. mbowe huwa hatoi hoja kwa kukurupuka ila wanaomjibu mara nyingi wanakurupuka. Mbowe ni mtu ninayemheshimu na nitaendelea kuheshimu michango yake .
 
Hivi ninani aliyewadanganya ukishambulia upinzani kwa kuwakashifu na kuwatetea serikali kwa hoja mfu kama hizo italeta nafuu ya maisha. Udikteta unagonga hodi TZ kumbukeni udikteta unatengenezwa kwa kupitia jamii hata marehemu idd amin dadaa alikuwa na wafuasi wakimshabikia kwa nguvu zote
 
Hata kama Sheria ingekuwa hairuhusu, kwa kuwa uhamisho huo umefanywa kwa maslahi ya Taifa hakuna tatizo!!

Kwa hiyo Mbowe alitakiwa Wakandarasi waendelee kufa kwa magonjwa ya moyo wakati wao walikopa bank ili watekeleze miradi ya Taifa, na Serikali ya JK. haikuwa inawalipa ni hadi alipoingia Magufuli ndipo akaanza kuwalipa haraka ili madeni hayo yasiendelee kuzalisha riba!!!

Hivi hawa UKAWA jamani ni vipi? kwani Tundu lissu hakuwepo Bungeni awasaidie?

Kwani ingefanyika hivyo kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi kwa jambo ambalo nadhani lisingechukua hata masaa matano au siku moja isingekuwa kwa maslahi ya taifa??

Ona sasa, kwa mizuka ya kijinga tu mmemuingiza Rais ktk matope na kashfa ya kuvunja katiba na sheria na wakati huohuo yeye anasimama na kupayuka majukwaani kuwataka watu watekeleze majukumu yao kwa kufuata na kuzingatia sheria!!

Does it make any sense in this situation??......No, no way please!!
 
Na wewe sasa utakuwa jipu, umeambiwa sheria ya bajeti ya mwaka 2015, ingia google hapo isome.
apu ni ya ccm na yanatumbuliwa na maccm kwa maana yalizalishwa na ccm, usinihusishe nayo.
Mimi nalima mihogo nikianza kingia gugo ntalipwa na bunge au halmashauri?? Maana ni kazi atii!!

Sio watupeleke gugo kusoma kurasa zooote kumbe wangetuelekeza tu mara moja.
 
Kama Taifa litakuwa na vijana wenye uelewa mdogo kama hawa wanaomtukana Mbowe tu kwa sababu anakosoa utaratibu uliotumika na serikali kuhamisha fedha bila kufuata sheria basi tunakoelekea siko.
Upinzani wa nchi hii umefanya kazi kubwa sana katika kusaidia Taifa hili kufika hapa lilipofika. Hata Rais wetu analazimika kusema na kutenda kama anavyofanya kwa sababu ya upinzani.
kama wasingekuwa wapinzani Tanzania ilikuwa ni nchi ya viongozi kulala na kula.
Mbowe na timu yake wako sahihi sana kukosoa mwenendo wa Serikali kufanya maamuzi juu ya matumizi ya fedha wakiwa Ikulu.
Ipo siku wataamua kumjengea rais kastri na kama hakutakuwa watu wa kuhoji fedha za umma zitakuwa zimepotea bila kuhoji.
waacheni wabunge wa upinzani waendelee kuhoji mambo yanayofanywa na serikali ili watoe ufafanuzi na sisi walipa kodi tujue namna fedha zetu zinavyotumika.
Ni bahati mbaya sana kuwa vijana wanakimbilia kuwatusi watu wazima na viongozi makini sana kama Mbowe.
Hekima na busara ni namna unavyoo argue na kutoa mawazo yanaoonesha ulivyo.
 
Hivi wanapata wapi mda wa kumjibu mtu kama mbowe ambaye uelewa wake sawa mwanafunzi wa darasa la tano c, uelewa wa mbowe ni mdogo sana yeye mda wote anafanya siasa tu.
Au Mbowe aliandikiwa na Lisu
 
apu ni ya ccm na yanatumbuliwa na maccm kwa maana yalizalishwa na ccm, usinihusishe nayo.
Mimi nalima mihogo nikianza kingia gugo ntalipwa na bunge au halmashauri?? Maana ni kazi atii!!

Sio watupeleke gugo kusoma kurasa zooote kumbe wangetuelekeza tu mara moja.

Nakumbuka Rais Magufuli alisema wanafunzi waliosomeshwa bure toka shule ya msingi alafu akafika form 4 akapata zero nae ni jipu,ndio nimekumbuka hilo lako.Sheria ya bajeti sio ndefu kushindwa kuipitia,ndio maana Mbowe ameshauriwa aisome maana yawezekana hajaisoma pia.
 
SIKU moja baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), kudai kuna uvunjifu wa sheria katika uhamishaji wa fedha zilizoidhinishwa na Bunge, Tume ya Mipango imetoa ufafanuzi na kusema hakuna sheria iliyovunjwa.

Aidha, Mbowe na wabunge wa kambi ya upinzani wametakiwa kwenda kuisoma upya Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 ili waielewe badala ya kuupotosha umma.

Akizungumza na gazeti hili mara baada ya kuzinduliwa kwa Kitabu cha Muongozo kuhusu wa Usimamizi Rasilimali za Umma, Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Mipango, Florence Mwanry alisema madai yaliyotolewa juzi na Mbowe bungeni si ya kweli.

“Wabunge ndio walipitisha wenyewe Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015, ambayo inafafanua kuhusu uhamishaji wa fedha kutoka kifungu kimoja kwenda kingine, hivyo uhamisho wa fedha uliofanywa uko sahihi na hakuna sheria iliyovunja, wakaisome vizuri,” alisema Mwanry.

Mbowe akizungumza na waandishi wa habari juzi baada ya kususa Bunge, alitoa mfano wa bajeti ya maendeleo iliyoidhinishwa na Bunge kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2015/16, iliyokuwa ya Sh bilioni 883.8, ambapo kati ya fedha hizo, fedha za ndani zilikuwa ni Sh bilioni 191.6.

Alisema inashangaza kuwa hadi kufikia Machi 2016, Wizara ilikuwa imeshapokea kutoka Hazina Sh bilioni 607.4, ambazo ni fedha za ndani, tofauti na ilivyopangwa kuwa fedha za ndani ni Sh bilioni 191.6. Mbowe alidai kuwa hiyo inaonesha kuwa kuna ongezeko la fedha zilizotolewa na Hazina hadi kufikia Machi 2016, ikilinganishwa na fedha zilizoidhinishwa na Bunge.

Akitoa ufafanuzi, Mwanry ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Mipango, alisema Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015, inamruhusu Ofisa Masuhuli kuhamisha fedha kutoka kifungu kimoja kwenda kingine, ili mradi asivuke asilimia saba ya bajeti nzima.

Kadhalika, kwa upande wa Waziri, alisema sheria hiyo inampa uwezo wa kufanya uhamisho wa fedha kutoka kifungu kimoja kwenda kingine ili mradi asizidi asilimia 10 ya bajeti na katika uhamisho uliofanywa na wizara tajwa, mambo hayo yamezingatiwa.

“Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ni wizara yenye madeni mengi ya wakandarasi na ni moja ya wizara zinazotumia fedha nyingi kwenye masuala ya miundombinu, sasa ni lazima madeni hao yalipwe na Serikali haiwezi kuacha kuyalipa kwa sababu kadri yanavyobaki, ndivyo riba inavyoongezeka,” alisema Mwanry.

Alisema pamoja na uhamisho uliofanywa ndani ya wizara hiyo, bado fedha zilizohamishwa ziko ndani ya kiwango kinachotakiwa kisheria na bado ni kiwango kidogo ambacho hakijavunja sheria.

Habari Leo

Hapa tuna zungumzia kuongeza bajeti ya wizara sio vifungu vya matumizi ...huyu ofisa anazungumza kuongeza na kupangua bajeti ya vifungu ndani hio 191 billion.
kilichofanyika ni kutoa hazina na kungeza bajeti kufikia 600 billion.
bado nidhamu ya matumizi inahitajika....nidhamu ya matumizi hata nyumbani kwa mtu ni muhimu kufatwa
 
Sijaona citation ya vifungu hapo while mbowe aliainisha vifungu vilivyokiukwa.
Pombe amejaliwa vilaza wengi sana kwenye serikali yake.
Ukitengeneza serikali kwa kuangalia waliokusaidia au watu wako wa karibu matokeo yake ndiyo hayo.Serekali inatakiwa kuongozwa na watu makini na sio wapiga zumari.
 
Sijaona citation ya vifungu hapo while mbowe aliainisha vifungu vilivyokiukwa.
Pombe amejaliwa vilaza wengi sana kwenye serikali yake.
Hata kama vifungu hivyo vipo aslimia 10 ya bilioni 808 ni bilioni 80. Bilioni 80 ongeza fungu husika kama lilivyoidhinishwa yani bilioni 196 unapata bilioni 276 wakati zilizohamishwa ni zaidi ya bilioni 400 badala ya 80. Huyo anaongea kwa kuwa anajua anaongea na vilaza hawataelewa kitu
 
Humu kuna mijitu mijinga mivivu ya kufikir hivi hutujui hata sababu zilizo fanya kambi ya upinzani kutoka bungeni hepu tuachane na siasa za kishabiki ccm washafeli tayari nani asiyejua kama spika wa bunge yupo kwa ajili ya kulinda ujinga wa serikali
 
Hapa tuna zungumzia kuongeza bajeti ya wizara sio vifungu vya matumizi ...huyu ofisa anazungumza kuongeza na kupangua bajeti ya vifungu ndani hio 191 billion.
kilichofanyika ni kutoa hazina na kungeza bajeti kufikia 600 billion.
bado nidhamu ya matumizi inahitajika....nidhamu ya matumizi hata nyumbani kwa mtu ni muhimu kufatwa

Wewe hujaelewa. Bajeti ya maendeleo ni tzs 883bn kati ya hizo fedha za ndani ni tzs 191bn. Kilichofanyika ni fedha za ndani zilitumika zaidi yaani 607bn badala ya 191bn. Hii ni kwa kuwa fedha za nje hazikupatikana na makandarasi ni lazima walipwe. Shida ya Mbowe ni nini hapo?
 
Sijaona citation ya vifungu hapo while mbowe aliainisha vifungu vilivyokiukwa.
Pombe amejaliwa vilaza wengi sana kwenye serikali yake.
Nenda kasome hiyo sheria ya bajeti ya mwaka 2015 halafu ndo utajua pumba ni zipi na mchele ni upi ndo uje na kasoro ulizoziona,sio mpaka kila kitu mpaka utafuniwe ,vitu vingine jiongeze kidogo.
 
Wewe hujaelewa. Bajeti ya maendeleo ni tzs 883bn kati ya hizo fedha za ndani ni tzs 191bn. Kilichofanyika ni fedha za ndani zilitumika zaidi yaani 607bn badala ya 191bn. Hii ni kwa kuwa fedha za nje hazikupatikana na makandarasi ni lazima walipwe. Shida ya Mbowe ni nini hapo?

Makandarasi eeeehhhh..sasa kwa nini tunatumia zaidi ya bajeti ? ...Juzi tulitakiwa kuhakiki malipo BOT ..Jee hawa wakandarasi wamo ?
 
Back
Top Bottom