Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 17,547
- 28,494
Billionea Rostam Aziz 'kada' wa CCM
Moja ya misingi ya Imani ya mwana CCM ni kwamba :
- Binadamu wote ni sawa
- Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake
- jamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru
Pamoja na Imani hizi ambazo ni za kimsingi kabisa kibinadamu na ki utu, bado kuna Ahadi za mwana CCM.
AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI
(1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja
(2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote
(3) Nitajitolera nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.
(4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.
(5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
(6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.
(7) Nitashjirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.
(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.
(9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.
Imetolewa na : Chama Cha Mapinduzi - CCM
Sasa hebu kwa vigezo hivyo tuipime CCM ya leo na tumpime Rostam Aziz.
Tukumbuke Rostama Azizi ni Bilionea mkubwa si Tanzania tu, bali Afrika mashariki na Afrika.
Kwake huyu Ujamaa ni tusi.
Na tujiulize kati ya Rostam Aziz na Humphrey Polepole, utamwamini nani hata kama humpendi.