Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,996
Salaam,
Kwanza naomba niwatulize mioyo wale ambao kwa namna moja au nyingine wanajisikia kukwazika na kile kilichoendelea Bungeni leo hii na hasa suala la Richmond. Ninafahamu watu wengi wangependa kuona mambo makubwa yanatokea tena na watu wanatimuana na hata ikibidi kupeana mipasho ya papo kwa papo. Wengine wangetamani kuona wale ambao walijitangaza kuwa ni wapiganaji wanachukua msimamo mkali zaidi na kutokubali kwa namna yoyote ile kulimaliza suala hili kimya kimya.
Hata mimi ningependa hivyo.
Hata hivyo, inaposemwa kuwa "siasa ni mchezo mchafu" siyo suala la utani ni suala la ukweli. Wakati wowote unaposhughulika na wanasiasa ni lazima utarajie mambo kama haya kama gharama ya wanasiasa. Lakini zaidi pia ni lazima tuzingatie kuwa wanasiasa wote (na hapa naamanisha wote duniani) wanafanya mambo wakiongozwa na kanuni kubwa tatu duniani:
a. Watafanya jambo lolote ili wachaguliwe kushika madaraka
b. Wanataka wachaguliwe tena kushika madaraka (re-election)
c. Endapo kuna uwezekano wa wao kutochaguliwa, angalia kanuni "a".
Hivyo, yaliyotokea Bungenii leo na yatakayotokea kwenye suala la Kamati ya Mwinyi na hata baadaye kabla ya kuvunjwa kwa Bunge katikati ya mwaka huu ni LAZIMA yaangaliwe kwa mwanga huo.
Kwa maneno mengine msipate matumaini ya uongo kusikia wanasiasa wanaanza kujitokeza kuwa wapiganaji ufisadi kweli kweli baadaye mwaka huu huku miongoni mwao wakiwa ni wale waliokuwa mawaziri.
Hawa mtawasikia wakijitetea kuwa wakiwa mawaziri wanatakiwa kusimamia maamuzi ya serikali n.k na wengine watasema walichukua maamuzi mbalimbali ili kuonesha umoja ndani ya chama na siyo kwa sababu walikuwa ni dhaifu! Yote ni katika kufanya kazi kwa kanuni "a".
Ninachosema ni kuwa tusiwaangalie wanasiasa kama chanzo cha matumaini yetu ya kulibadilisha taifa letu! Tusiweke imani yetu yote kwa wanaotaka madaraka kwa namna yoyote ile kwani uwezekano wa wao kutuangusha ni mkubwa mno kama tulivyoona. Wakati umefika sisi wananchi wenyewe tuamue kumshika ng'ombe mapembe yake na kumuongoza tunakotaka.
Hii ina maana gani? Maana yake ni kwamba bila ya sisi wananchi kusimama pamoja na kusema nini tunachotaka (siyo kukubali kile ambacho wao wanasema nini tunataka" basi hatuwezi kupata mabadiliko tunayoyataka.
Naomba niwatie shime enyi wana na mabinti wa taifa langu; msikate tamaa kwa kukatishwa tamaa na wanasiasa! Msiinamishe vichwa vyenu kwa masikitiko kwa sababu hawajakidhi mahitaji yenu! La hasha! Tuinue vichwa vyetu juu na kusema "tunawaelewa" na kwa sababu hiyo hatuwataki tena.
Muda unakuja ambapo Watanzania wataitwa wachukue msimamo dhidi ya wanasiasa wao; msimamo ambao utalitikisa taifa letu. Tumeanza kuona dalili zake toka mbali (CCJ na sasa "Tamko").. kama Moshi uliofichwa nyuma ya kilima tunaweza kusema kwa uhakika mahali fulani kuna moto; kama mwangaza wa jua linavyopambazuka tunaona nuru yake kabla hata halijatoka, lakini tuna uhakika kuwa nyuma yake lipo jua!
Mwaka huu ni mwaka wa Uamuzi wetu; ni mwaka wa uchaguzi wetu. Tusiwaache wanasiasa watuamulie tunachotaka ili tuwachague; tuwaamulie kile tunachotaka ili wakikubali tuwachague!!
Ni mimi ndugu yenu,
Mwenzenu,
rafiki yenu,
Na wengine adui yenu wa kudumu
Mpaka msalimu amri!!
M. M. Mwanakijiji
NB: Tutaanza matangazo yangu ya audio wiki ijayo inshallah.. mwendo mdundo mpaka kampeni.. zikiiva..tutaonana majukwaani!!
Wenye uwezo wa kurekodi CDs (downloads) tutakuwa na option ya kudownload episodes za "kijijini leo hii" na mnaruhusiwa kuzicheza na kuzisambaza mahali popote!!