Tulizeni mioyo Watanzania

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Salaam,

Kwanza naomba niwatulize mioyo wale ambao kwa namna moja au nyingine wanajisikia kukwazika na kile kilichoendelea Bungeni leo hii na hasa suala la Richmond. Ninafahamu watu wengi wangependa kuona mambo makubwa yanatokea tena na watu wanatimuana na hata ikibidi kupeana mipasho ya papo kwa papo. Wengine wangetamani kuona wale ambao walijitangaza kuwa ni wapiganaji wanachukua msimamo mkali zaidi na kutokubali kwa namna yoyote ile kulimaliza suala hili kimya kimya.

Hata mimi ningependa hivyo.

Hata hivyo, inaposemwa kuwa "siasa ni mchezo mchafu" siyo suala la utani ni suala la ukweli. Wakati wowote unaposhughulika na wanasiasa ni lazima utarajie mambo kama haya kama gharama ya wanasiasa. Lakini zaidi pia ni lazima tuzingatie kuwa wanasiasa wote (na hapa naamanisha wote duniani) wanafanya mambo wakiongozwa na kanuni kubwa tatu duniani:

a. Watafanya jambo lolote ili wachaguliwe kushika madaraka
b. Wanataka wachaguliwe tena kushika madaraka (re-election)
c. Endapo kuna uwezekano wa wao kutochaguliwa, angalia kanuni "a".

Hivyo, yaliyotokea Bungenii leo na yatakayotokea kwenye suala la Kamati ya Mwinyi na hata baadaye kabla ya kuvunjwa kwa Bunge katikati ya mwaka huu ni LAZIMA yaangaliwe kwa mwanga huo.

Kwa maneno mengine msipate matumaini ya uongo kusikia wanasiasa wanaanza kujitokeza kuwa wapiganaji ufisadi kweli kweli baadaye mwaka huu huku miongoni mwao wakiwa ni wale waliokuwa mawaziri.

Hawa mtawasikia wakijitetea kuwa wakiwa mawaziri wanatakiwa kusimamia maamuzi ya serikali n.k na wengine watasema walichukua maamuzi mbalimbali ili kuonesha umoja ndani ya chama na siyo kwa sababu walikuwa ni dhaifu! Yote ni katika kufanya kazi kwa kanuni "a".

Ninachosema ni kuwa tusiwaangalie wanasiasa kama chanzo cha matumaini yetu ya kulibadilisha taifa letu! Tusiweke imani yetu yote kwa wanaotaka madaraka kwa namna yoyote ile kwani uwezekano wa wao kutuangusha ni mkubwa mno kama tulivyoona. Wakati umefika sisi wananchi wenyewe tuamue kumshika ng'ombe mapembe yake na kumuongoza tunakotaka.

Hii ina maana gani? Maana yake ni kwamba bila ya sisi wananchi kusimama pamoja na kusema nini tunachotaka (siyo kukubali kile ambacho wao wanasema nini tunataka" basi hatuwezi kupata mabadiliko tunayoyataka.

Naomba niwatie shime enyi wana na mabinti wa taifa langu; msikate tamaa kwa kukatishwa tamaa na wanasiasa! Msiinamishe vichwa vyenu kwa masikitiko kwa sababu hawajakidhi mahitaji yenu! La hasha! Tuinue vichwa vyetu juu na kusema "tunawaelewa" na kwa sababu hiyo hatuwataki tena.

Muda unakuja ambapo Watanzania wataitwa wachukue msimamo dhidi ya wanasiasa wao; msimamo ambao utalitikisa taifa letu. Tumeanza kuona dalili zake toka mbali (CCJ na sasa "Tamko").. kama Moshi uliofichwa nyuma ya kilima tunaweza kusema kwa uhakika mahali fulani kuna moto; kama mwangaza wa jua linavyopambazuka tunaona nuru yake kabla hata halijatoka, lakini tuna uhakika kuwa nyuma yake lipo jua!

Mwaka huu ni mwaka wa Uamuzi wetu; ni mwaka wa uchaguzi wetu. Tusiwaache wanasiasa watuamulie tunachotaka ili tuwachague; tuwaamulie kile tunachotaka ili wakikubali tuwachague!!

Ni mimi ndugu yenu,
Mwenzenu,
rafiki yenu,
Na wengine adui yenu wa kudumu

Mpaka msalimu amri!!

M. M. Mwanakijiji

NB: Tutaanza matangazo yangu ya audio wiki ijayo inshallah.. mwendo mdundo mpaka kampeni.. zikiiva..tutaonana majukwaani!!

Wenye uwezo wa kurekodi CDs (downloads) tutakuwa na option ya kudownload episodes za "kijijini leo hii" na mnaruhusiwa kuzicheza na kuzisambaza mahali popote!!
 
Kaka yangu matumaini ni kitu muhimu sana. Tunaambiwa wakati ule wa vita ya pili, kilichomsukuma Pope John Paul kwenye seminari ya siri ni tumaini kubwa lililokuwa ndani ya moyo wake kwamba hali ile ya siasa za nazi kuikalia Poland zilikuwa ni za mpito tu.Ndivyo pia alivyoishi wakati wa ukomunist ambao ulihakikisha dini haifui dafu kwenye himaya yake.

Lakini historia inatuonyesha pia ni kwa matumaini hayo hayo, baada ya kuwa pope, alijitahidi sana kuhakikisha vyama vya wafanyakazi vinapata nguvu kuupinga ukomunist nchini Poland.Mchango wake unathaminiwa sana kama ni mmoja aliyesaidia kuanguka kwa lile Iron Curtain.

Hata leo hii bado tuna kila sababu ya kuwa na matumaini kwamba all is not lost.Siku moja tutaona kitu tofauti.
 
Mi si mpenda vurugu. Lakini kuna siku nyingine napatwa na hasira ambayo haina kipimo. Mfano wa siku kama hizo ni leo.

Ushauri wangu kwa wanajeshi na polisi ni huu: badala ya kupiga na kuua wananchi (wengi wao wasio na hatia) tafadhali jikusanyeni pale Dodoma mtembeze mkong'oto kwa hii mijitu inayosahau akina nani waliwapa dhamana ya kukaa katika lile jengo, si kwenda kulala, la! Si kukaa kimya! KUSIMAMIA HAKI YA MWANANCHI!!
 
Bila shaka ajenda hii ni muhimu kwa mstakabali wa ustawi wa taifa letu na watu wake. Hata hivyo, mtoa hoja naomba nimrudishe nyuma kidogo! Je, ni nini kimetokea leo Bungeni? Maana maelezo yanaonyesha kuna hali imetokea yenye kukatisha tamaa wananchi, lakini hasa ni nini hicho? Ni maamuzi gani hayo yaliyofanywa na wanasiasa wetu ndani ya nyumba yetu? Nauliza maswali haya nikimaanisha kwamba si wote wana JF wamepata au kwa kusikiliza ama kutazama kwenye Runinga yaliyojiri bungeni, la hasha! Hivyo, ingekuwa vyema tukapata muhtasari wa nini kimetoke maana wengine wako nje ya mipaka ya nchi. Halafu baada ya hapo ndipo sasa tunaweza kuchangia tukiwa na uelewa sambamba juu ya ajenda hii. Nashukuru!
 
Mi si mpenda vurugu. Lakini kuna siku nyingine napatwa na hasira ambayo haina kipimo. Mfano wa siku kama hizo ni leo.

Ushauri wangu kwa wanajeshi na polisi ni huu: badala ya kupiga na kuua wananchi (wengi wao wasio na hatia) tafadhali jikusanyeni pale Dodoma mtembeze mkong'oto kwa hii mijitu inayosahau akina nani waliwapa dhamana ya kukaa katika lile jengo, si kwenda kulala, la! Si kukaa kimya! KUSIMAMIA HAKI YA MWANANCHI!!
Wanasiasa si watu wa kuwafuata nyuma tukahisi tuko salama. Wanasiasa wa Tanzania have stopped living in the world of realities. They live in the world of fantansies.Do you think wanafikiria uongozi ni dhamana? Wwengi wapo pale ili wale washibe na tena wavimbiwe. Time will tell and again time will heal everything.Tusifanye vurugu tukaiharibu nchi yetu. Kuna namna bora za kuwapa adabu wanasiasa bila umwagaji wa damu.
 
Ndahani, nakubaliana na wewe kabisa. Shida ni kwamba, je nani ataanzisha na kumalizia hizo njia bora za kuwapa adabu wanasiasa? Wale "wapiganaji" wako wapi? Mbona wamekuwa kimya? Mbona wamevua boxing gloves?

Ni kitu gani au ni nani amewanyamazisha?

Yes, time will tell, but when will this "time" come? Isn't this the time? Aren't we the ones to tell?
 
Iwapo watanzania wataelewa kwa nini Abraham Lincoln alisema "Politicians are a set of men who have interests aside from the interests of the people and who, to say the most of them, are, taken as a mass, at least one long step removed from honest men".

Kwa hakika mioyo yao itatulia.
 
Watanzania watamjulia wapi na kumwelewa Abe Lincoln wakati hata hawahusum na wengi wao hawamjui?
 
Sheep-3.jpg
 
Mimi hata sikutegemea chochote from the get go, kwa hiyo nimejiepushia disappointment.
 
Mzee Mwanakijiji ni vigumu sana kutuliza mioyo katika hali kama hii. Mioyo inauma kama ufe hivi uondokane na maumivu haya. Hawa mnawaita wabunge sijui wanaona sote ni punguwani (is it punguani or punguwani?) whatever it is! Jua hili litatelemka lini?
 
mzee mwanakijiji ni vigumu sana kutuliza mioyo katika hali kama hii. Mioyo inauma kama ufe hivi uondokane na maumivu haya. Hawa mnawaita wabunge sijui wanaona sote ni punguwani (is it punguani or punguwani?) whatever it is! jua hili litatelemka lini?

jamani tusiwalaumu sana. Maisha yenyewe magumu hivi, wamebahatia kuongoza watu wasiochukua hatu, walio mabingwa wa kusema tu na kutoa ofa za ushindi wa kishindo, sasa jamani wafanye nini?

Nawatahadharisha wote wanaofikiri jk ni rais dhaifu, waone mikakati yake na wajifunze sasa!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
yupo wapo mzee wa viwango na speed,wapo wapi manabii wetu Mwakyembe,Mpendazoe,Shelukindo na mama kilango..kweli siasa ni mchezo mchafu,nimeamini ni bora kumuamini mmasai maana akikimbia unaweza kubaki hata na nguo kuliko kuwaamini wanasiasa,wametuuzia samaki kwenye maji.....
 
we knew it mkuu! ila inaelekea watu wasahaulifu sana. CCM tangu enzi hizo wana kitu cha kuwadanganyia raia!!
 
Wanasiasa si watu wa kuwafuata nyuma tukahisi tuko salama. Wanasiasa wa Tanzania have stopped living in the world of realities. They live in the world of fantansies.Do you think wanafikiria uongozi ni dhamana? Wwengi wapo pale ili wale washibe na tena wavimbiwe. Time will tell and again time will heal everything.Tusifanye vurugu tukaiharibu nchi yetu. Kuna namna bora za kuwapa adabu wanasiasa bila umwagaji wa damu.

Jaribu kuzipendekeza uone wanafiki watakavyokuangukia na justifications za 25 divided by 5 is = 14...........damn!
 
Watanzania wenzangu hapa plan A imekataa au haijaaply,and what to do now? we come with plan B, and what is plan B?.Many of our fellow Tanzanian they dont know what is going right now,na wale wanaojua baadhi yao hawataki kushirikisha ubongo wao.sasa kinachotakiwa ni create this plan B and pass information to all Tanzanian by any means.what is plan B ? need your contridution.
"WE CAN CHANGE OUR COUNTRY GOD BLESS US"
 
Haya ni masikitiko makubwa sana kwa kila mpenda maendeleo wa nchi yetu njema ya Tanzania. Watanzania sasa tumekuwa ni watu tunaoyumbishwa kimaendeleo na kifikra kutokana na hawa watu wanaoitwa wanasiasa ambao ni wanafiki na wenye uroho wa madaraka ambayo yanaonekanani matamu kutokana na kuwa ni njia rahisi kwao kutunyonya sisi na kujilimbikizia mali wao pamoja na fanilia zao.

Hii ni kusema kuwa wanasiasa hasa hawa wa chama kinacoitwa tawala si watu wa kuwaamini kabisa kwani mara nyingi chochote watakachokisema au kukifanya huwa ni kwa maslahi yao na nafasi walizo nazo. Ninacoweza kusema ni kuwa hawana msaada kwetu kabisa kwani ni watu ambao wanaweza kubadilika wakati wowote kulingana na upepo wa kisiasa unavyoweza kuwajenga na kuwaimarisha wao.

Kitu kingine wana JF ninachoweza kusema ni kuwa hii michango yetu na hasira zetu tuanazozitoa hapa ni kama vile tunapiga risasi hewani au kichakani bila ya kuwa na uhakika kama hapo kichakani kuna adui au la na kama yupo je hizo risasi zinampata? Je hawa watawala wanaathirka na michango tunayotoa hapa

Swali ambalo bado najiuliza ni kuwa ni nini hatua ya wananchi? Je nini kinaweza kufanyika hapa ukiacha ya uchaguzi (kwa sababu nina uhakika watashida tu). Kunahitajika nguvu ya ziada halisia zaidi na pengine ikiwa ni nje ya vyama vya siasa. Kunahitajika nguvu na movement ambayo tutakuwa na uhakika kwa kuona kuwa haya mambo yanawaingia hawa watawala wetu la sivyo tutaendelea kuandika makala zenye uchambuzi wa kina na zenye akili lakini walengwa haziwaletei athari kwa kuwa public haijaamua kuvalia njuka physically
 
Back
Top Bottom