Tulitaka kutengenezewa ukame bwawa la Mtera, tupazeni sauti tukiona ndivyo sivyo

"Hata kama tusipopata tone la maji bado tunaweza kuzalisha umeme kwa miezi saba ijayo" - Meneja Bwawa la Mtera.

Ole wao mafisadi wa nchi hii wamshughulikie huyo meneja, ameamua kuwa mkweli kwa nafsi yake na nchi yake, hawa jamaa ni wezi na wanafahamika kwa matendo yao miaka na miaka, kuwatetea kwa kutuletea namba nyingi kwenye long articles ni kupoteza muda tu.

Rais anakurupuka kuleta habari za LNG na wajanja nao wanachukua nafasi hiyo kutengeneza mianya ya kutupiga huku Zitto akiwa mpiga zumari, wanajua pale kuna $ 30 mil. ni nani mwenye akili timamu wakuiamini combination ya Zitto na Makamba?

Badala ya kumalizia mradi wa Bwawa la Nyerere wanaenda kutumbukiza mapesa mengi kutengeneza mradi mpya, hivi kwa akili ya kawaida tu hii kitu inaeleweka kweli?
Kwa faida ya wasomaji ni 30b usd na sio 30m usd
 
Mkapa akiwa Rais aliwa kusema ni bahati na faraja kubwa kuwa Rais wa Tanzania kwani Watanzania ni wapole na wavumilivu. Kikwete nae alikuja kuinukuu kauli hii.

Hapa ndipo tatizo linapo anzia, viongozi wanajua Watanzania ni wapole kwa hiyo wanaweza fanya chochote hata hujuma za wazi kabisa kwasababu wanajua no action will be taken. Kuna mambo yanafanywa na viongozi wakuu ingekuwa kwa nchi nyingine wasinge thubutu.
 
“Kwa kina hiki cha mita 5.76 tunaweza kuzalishha umeme kwa kiwango cha juu cha megawatts 80 kwa miezi saba ijayo hata kama tone moja la mvua halitaingia kwenye bwawa la Mtera”

- Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme Mtera, Elias Mwalupilo
Kihansi, Kidatu na Pangani ndiyo mabwawa yaliyoathiriwa na upungufu wa mvua. Bwawa la Mtera lina uwezo wa kuhifadhi maji kwa mwaka mmoja. Yaani lina resrvoir inayoweza kuback-up kwa mwaka mzima kwa hiyo huwa linakuwa la mwisho kukauka.
Kama hali ni mbaya zaidi wanaachia not at maximum capacity kurefusha matumizi na kusubiri mvua.
 
“Kwa kina hiki cha mita 5.76 tunaweza kuzalishha umeme kwa kiwango cha juu cha megawatts 80 kwa miezi saba ijayo hata kama tone moja la mvua halitaingia kwenye bwawa la Mtera”

- Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme Mtera, Elias Mwalupilo
 
Back
Top Bottom