Tulitaka kutengenezewa ukame bwawa la Mtera, tupazeni sauti tukiona ndivyo sivyo

mwananyaso

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
2,843
3,128
“Kwa kina hiki cha mita 5.76 tunaweza kuzalishha umeme kwa kiwango cha juu cha megawatts 80 kwa miezi saba ijayo hata kama tone moja la mvua halitaingia kwenye bwawa la Mtera”

- Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme Mtera, Elias Mwalupilo
 
"Hata kama tusipopata tone la maji bado tunaweza kuzalisha umeme kwa miezi saba ijayo" - Meneja Bwawa la Mtera.

Inavyoonekana hawa wazito huwa wanaenda field wanapewa taarifa za kweli, lakini wao wakija kwenye majukwaa yao ya twitter wanaingiza siasa zao ili kutimiza malengo yao ovu kwa taifa, na kwa vile hawa mameneja miradi hawana uwezo wa kuwapinga, basi mafisadi wanajifanyia watakavyo.

Ole wao mafisadi wa nchi hii wamshughulikie huyo meneja, ameamua kuwa mkweli kwa nafsi yake na nchi yake, hawa jamaa ni wezi na wanafahamika kwa matendo yao miaka na miaka, kuwatetea kwa kutuletea namba nyingi kwenye long articles ni kupoteza muda tu, haya mambo ni kile kinachotokea field na wala sio kutuletea namba za darasani.

Rais anakurupuka kuleta habari za LNG na wajanja nao wanachukua nafasi hiyo kutengeneza mianya ya kutupiga huku Zitto akiwa mpiga zumari, wanajua pale kuna $ 30 mil. ni nani mwenye akili timamu wakuiamini hii combination ya Zitto na Makamba?

Badala ya kumalizia mradi wa Bwawa la Nyerere wanaenda kutumbukiza mapesa mengi kutengeneza mradi mpya, hivi kwa akili ya kawaida tu hii kitu inaeleweka kweli? tumezungukwa na circle ya wapigaji lazima tuwe makini.
 
“Kwa kina hiki cha mita 5.76 tunaweza kuzalishha umeme kwa kiwango cha juu cha megawatts 80 kwa miezi saba ijayo hata kama tone moja la mvua halitaingia kwenye bwawa la Mtera”

- Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme Mtera, Elias Mwalupilo
Nilitaka kushangaa ukame gani wa ghafla huo,
Raisi laziam aingilie kati, vinginevyo atakua analea wahalifu.
 
Back
Top Bottom