Tuliowahi kufukuzwa kazi tukutane tupeane experience

Ni machungu sana, nayakumbuka, niliyoyapitia, ila ulifanya harakavkuandika barua ya kuacha ungesubiri wao ndo wakuteme.
Hii ndo njia pekee itakayoweka salama kimaisha ya kama unategemea kuwa mwaajiriwa tena,resignation ni nzuri kuliko kufukuzwa ni sawa kuna mafao utayakosa but still unajitengenezea njia bora ya kuajiriwa tena bila CV yako kuchafuliwa na vukuzwavukuzwa.Mimi nimepitia njia hii nadhani ningelikuwa nimefukuzwa huko nilikotoka nadhani nisengelikuwa ajirani tena
 
Mkuu naomba unisaidie mahali,kuna kitu umeongea kimenigusa sn

Mimi ni mwajiriwa wa private sector.Ni operator wa mashine.Kazini kwetu kuna kipindi kazi huwa zinakuwa nyingi sn kiasi kwamba tunafanya shift(wawili usiku,wawili mchana )Kwa wiki moja moja

Ndani ya mwezi Mimi ninafikisha masaa Hadi masaa130.
Mshahara ukiingia wao wanaweka masaa 50 ktk Yale 130(yaani haijalishi umefanya kazi masaa mangapi ya overtime,kampuni itaweka masaa 50 tu)

Siku moja tukauliza Kwa manegement Kwa nn pesa ya overtime ni ndogo kuliko masaa ya overtime yenyewe tofauti na miaka kadhaa iliyopita,tukajibiwa serikali(ya magufuli) inakataza mwajiri kumfanyisha kazi mwajiriwa wake zaidi ya masaa 50 ya overtime Kwa mwezi.Tukauliza lkn kinyume chake Sisi tunafanya tena masaa zaidi ya Mia Kwa mwezi mmoja,Kwa hiyo mkilipa masaa 50 hayo masaa yanayozidi Kwa kila mfanyakazi mnatulipa vipi?

Wakatujibu;kampuni itawalipa kipindi kazi zimepungua

Hapa ngoja nielezee kitu mkuu Kwa nn walijibu hivi..kampuni ninayofanya kazi inajihusisha na usafirishaji wa zao Fulani nje ya nchi(ulaya,Amerika,Japan na south Africa)

Kwa hiyo kuna kipindi kazi za kuleta mazao kutoka mikoani Hadi hapa bandarini(ilipo kampuni) zinakuwa nyingi takriban miezi 6-8 kiasi kwamba machine operators inatubidi kufanya shift ya day&night na ndiyo kipindi masaa ya overtime yanakuwa mengi sn.
Kwa hiyo ndy maana tukajibiwa tutalipwa masaa tunayodai ktk miezi Ile ambayo haina kazi(ambayo inakuwa minne Hadi sita);yaani kila mwezi tutakuwa tunawekewa masaa 50 Hadi yaishe Yale masaa yaliyozidi

Cha ajabu huu ni mwaka wa pili mfululizo sasa tunatumikishwa kazi usiku na mchana na masaa yanakuwa mengi lkn kampuni hailipi zaidi ya masaa 50 ambayo wanadai ndy ya serikali

Haya masaa yanayozidi hatujawahi kulipwa kabisa na tumeshawahi kutishiwa na mtu mkubwa wa hapo ofisini kwamba mkijifanya kudai sn anatafuta mtu wa kutolewa mfano afukuzwe kazi

Mkuu hakuna ambaye hataki kazi lkn tunapata mateso sn..nipe mwongozo ktk hili nini tunapaswa kufanya
pole sana
 
Nilivyo sipendi Dharau nimeshaacha kazi kwenye kampuni zaidi ya 3 na zote ni figisu za wafanyakazi wenzangu kazi ya mwisho Nilimtukana mpaka bosi wangu maana alikuwa hajitambui anapelekeshwa na Vilaza wenzake Miaka miwili baadae nimerudi Nimekuta
Wafanyakazi wote wamehama na kampuni Imefilisika!
 
Nilivyo sipendi Dharau nimeshaacha kazi kwenye kampuni zaidi ya 3 na zote ni figisu za wafanyakazi wenzangu kazi ya mwisho Nilimtukana mpaka bosi wangu maana alikuwa hajitambui anapelekeshwa na Vilaza wenzake Miaka miwili baadae nimerudi Nimekuta
Wafanyakazi wote wamehama na kampuni Imefilisika!
Ulirudi kwenda kufanya nn?
 
Hivi serikalini unaweza fukuzws kazi kweli , je ikitokea taasisi ulifanyia kazi ikafutwa kisheria inakuwaje?
 
Pole sana. Ila watu wengi sana wanaonewa makazini na kufukuzwa kazi au kuresign kwa sababu tu hawajui haki zao kama wafanyakazi.

Kama hapo wewe ulichotakiwa kufanya ni usinge resign, usubiri jamaa wakufukuze kwa kosa hilo moja tu; Ungewaendesha sana iwapo baada ya wao kukufukuza ungeenda kwenye vyombo vya utetezi kama tume ya usuluhishi wa migogoro sehemu za kazi (CMA).

Maana mfanyakazi hafukuzwi kazi kirahisi hivyo, lazima kuwe na ushahid kwamba alishaonywa mara kadhaa, sio kosa lake la kwanza na mambo kama hayo, ukipeleka kesi kama hiyo kwa jamaa wa CMA hao waajiri wako wangekukoma; na wangeamuriwa kukulipa fidia ya kutosha tuu.

Tena kwa taasisi za binafsi ndo huwa CMA wanawakalia zaidi kooni. Ila ndo hivyo pia waru wengi hata hawawajui hao CMA.

But anyways, god for you kwamba you have moved on na maisha yameendelea! kiroka
Nipe hiyo elimu aisee
 
miaka kumi na ushee iliyopita....
Nilikiwa kwenye ajira kwenye kampuni niliyufanyia kazi kwa zaidi ya miaka nane katika vitengo tofauti tofauti kwa ufanisi mzuri tuu,sasa nikiwa mkoani tukaitwa Makao makuu kwa ajili ya kujifunza system mpya ya kazi, tulivyomaliza wakati narudi kituo changu wakati tunakabidhiana kazi na msaidizi wangu nikagundua upotevu wa vifaa ambavyo thamani yake ilikuwa ni kama milioni 2 hivi,nilikuwa na uwezo wa kulificha hili au kulimaliza kichinichini ila baada ya kugundua upotevu ule haukumhusisha msaidizi wangu nikaamua kuliripoti makao makuu kwa hatua za ziada,ikiwa ni pamoja na kuwaelezea ninavyohisi upotevu umetokea na vielelezo ambavyo wangevitumia ilikuwa rahisi kubaini upotevu huu,baada ya muda alitumwa mkaguzi wa ambae alikuja kuangalia lilivyotoea,(mbwa sana yule mhindi)..alinilazimisha kuandika kuwa kosa amelitenda msaidizi wangu ili achukuliwe hatua,nilimwambia siko tayari kuchuma hiyo dhambi na kama anadhani kosa lipo basi nitalibeba mimi,story ni ndefu ila baadae nlikuja kuitwa kwa mahojiano yaliyochukua zaidi ya siku tatu na waliokuwa wanasimamia wakanikandamiza kuwa kosa limetendeka chini yangu hivyo ni kosa langu, (wapuuzi wale walikuwa wanafanya kazi kwa kulamba lamba makalio ya wazungu ili waonekane wanajua wanachokifanya)baada ya kuona mwelekeo niliamua kufuatilia upotevu huo kivyangu bila kushirikisha ofisi ambapo nilifanikiwa kuwanasha waliofanya uhalifu huo na kuwafikisha mahakamani na wakahukumiwa kifungo,hili nililifanya bila kutoa taarifa ofisini,hatimae baada ya muda nilipewa barua ya kufukuzwa kazi bila ya kujua kuwa nilishalifanyia kazi na kufanikiwa kuwakamata wahalifu waliohusika, niliipokea barua kwa furaha kiasi kwamba hata walioniletea barua walibaki wananishangaa,niliwakabidhi pesa ya ofisi kama milioni 35 ambayo ningeweza kupotea nayo,nilivyomalizana nao nikaenda kufungua kesi CMA,kule wakaniwahi wakamrubuni wakili wangu akawa hahudhurii mahakamani mwishoe nikashindwa,nikatafuta wakili mwingine nika appeal,huyu walimfuata kumhonga wakashindwa, mlolongo ulikuwa mrefu lakini hatimae nilishinda na walinilipa stahiki yangu tosha kabisa,nashukuru wakati kesi inaendelea nilianza kujishughulisha na biashara ndogo ndogo na zilifanikiwa kwa kiasi kizuri tuu, wale wapuuzi walionikandamiza kuna wengine nakutana nao mitaani wamepauka hadi meno, niliifanya kazi kwa moyo sana lakini baada ya tukio hili nilichana vyeti vyangu vyotena kuvitia moto ili nisikumbuke tena kutafuta ajira... ...
@@kiteitei Hongera sana
Kiteitei hongera sana.
 
Ila Afika Bhana

Yaani hakuna tunachokifanya kikaenda smooth. Kiukweli tunahitaji kubadilika sana

Just imagine; unaajiriwa ila boss anakutreat kama mnyama vile.... au from nowhere anakuchukia tu ili mradi kazi ikushinde😁😁
Kuna maboss huwa wanahisi watakuwa on pick siku zote especially sekta Binafsi mfano kwenye ma NGO iwe local au International,huwa wanafikiria siku zote utakuwa chini hutainuka siku moja uwe kama wao au kuwazidi,hawafikirii kuna leo na kesho unamkuta uliyemdharau ni somebody somewhere anaweza mfanyia interview hata mwanae..ila maisha haya boss anaaamua tu kukuondoa kazini bila sababu ya msingi uwezo na experience well committed nodham ya kazi unayo ila analetwa mtu mpya asiejielewa wala hana uzoefu wa kazi wala mazingira na analalamikiwa performance still hawaoni..iliwahi nikuta hii najua maumivu yake ila Ma HR na Ma boss wa mashirika Binafsi MUNGU ANAWAONA NA MTALIPWA TU
 
Ile ilikua family company kwa hyo mtu baki akiwa na maendeleo ilikua ni tabu lazima uwe mwizi accoarding to wao. Maana kwa mfano mm nimeingia napata support ya mume nlikua nna duka tayari la bidhaa za nyumban na tulikua na boda tano, sasa wanawaza huyu hatujalipwa miezi mitatu anapata wapi pesa ya kuishi akati sie tuna tabu unaandamwa mpk mwenyewe unaacha kazi
Hakuna kitu baadhi ya maboss hawapendi kama kuona unapiga hatua kwa kufanya vitu vya ziada kumzidi yeye au wafanyakazi wengine..binafsi baada ya kufanyiwa figisu nlijikita zaidi kufanya ujasiriamali,japo walishangaa kuona mbona nimeweza kuinvest pesa nyingi kwa muda mfupi ktk biashara yangu siishi nyumba ya kupanga,nausafiri wangu binafsi nafanya biashara yangu kwa amani so wanashangaa kwa nn maisha yanaenda.MUNGU HAKUPI KILEMA AKAKUNYIMA MWENDO NIMESHUDIA nlipata nguvu hii baada ya kuona dalili mapema kwamba naweza nisiwe kazini soon baada ya mkataba kuisha
 
Mimi nimewahi kufundisha shule fulani private. Mkuu wa shule alikuwa na mambo ya kiwaki kisenge.

Sometimes, anaweza kukufokea hata mbele ya wanafunzi.

Ikifikia tarehe za mishahara basi ndio kufoka nje nje. Nyumba niliyokuwa nimepewa ilikuwa karibu na ya kwake, so, sometimes washkaji wakija gheto mkawa mnaongea kwa nguvu mnabishana mnacheka, anawaibukia anafoka Walimuu mnapiga kelele kama watoto wa primary

Nikawa najisemea tu huyu dawa yake iko jikoni.

Kuna wakati tunakaribia kuchukua mshahara, mwisho wa mwezi akawa anafoka, ooh kama hujaandika scheme of work na lesson plans sikulipi mshahara (walimu wanaijua hii midude.

Basi nikajipinda nikaandika hayo ma-scheme of works ( plan ya miezi 6 ) na lesson plans, nilivyomaliza nikampelekea.

Akasema poa, nenda kwa Accountant akupe mshahara wako. Nilivyolipwa tu, nitatafuta muda huyo mkuu wa shule hayupo, nikaiingia ofisini kwake nikayaiba hayo scheme of works nikaenda nikayachoma moto halafu nikaacha kazi, nikasepa. Ilikuwa 2013 hiyo.

Kiukweli mimi kuvumilia dharau nilishashindwa kabisa. Siwezi.

Mimi chuoni nimewahi kumfuata Lecturer ( HoD ) ofisini kwake nikamtukana. Alikuwa ananisumbua sana.

Mimi probably nitakuja kumnyenyekea mtu nikiwa na watoto 6, mmoja ana ugonjwa wa kudumu, nadaiwa kodi ya nyumba, mama ana matatizo.

Hapo nitajitahidi kunyenyekea. Kwasasa nitakuwa muongo. Sitaweza.
We jamaa una akili kama zangu kabisa niliwatukana wahindi enzi hizo hawatokaa wanisahau!
Na mpaka sasa sina mpango wa kuajiriwa tena maana naweza mpiga kichwa boss akizingua
 
Back
Top Bottom