Tuwaongezeni mishahara vijana wetu wa kazi

PharaohMtakatifu

JF-Expert Member
Jul 3, 2023
659
1,074
Heshima kwenu Wana Jf.

Ni Vyema Na Haki kabisa kuwaongeza mishahara (posho) wafanyakazi wetu wa majumbani.

Ni nadra sana kuona au kusikia mfanyakazi wa ndani(house girl/Boy) kaongeza Hela japo hata kidogo tu kwenye mshahara wake.

Jambo hili nimefatilia sana Kwa jamaa zangu wa karibu walio na wafanyakazi either wa ndani au wa mashambani.

Unakuta kijana ni mwaminifu sana na ameshakuwa kama mmoja wa wanafamilia hapo nyumbani na umemwamini kadumu zaidi ya miaka3-5 upo nae.

Cha ajabu hujawahi ongeza hata Hela kidogo tu. Hii inakatishaa tamaa sana.

Ajabu ni kwamba huyu mtu Ambae hujamwongezea posho hata likizo hujawaza waza kumpa Kwa mwaka hata wiki 2 tu aende kwao kusalimia ni hamna!

Mbona wewe hujiulizi kwann mwajiri wako anakupa mapumziko? Kwann anakuongeza mshahara?

Kuna dhambi Gani kati ya hiyo pesa ukamuongeza hata 10k Kila mwezi je utapungukiwa au utafirisika?

Mtoto wawatu umemtia mbali kote mkoani unampa jukumu la kumlelea Watoto wako wewe kutwa nzima haupo na umemwamini Kwa kiwango (si jambo dogo kumwachia mtu usiye mwamini Watoto wako wadogo ashinde nao na awapikie chakula familia nzima).


Walio wengi humu wasipopewa hata bonus ya quarter tu Huwa hapakaliki huko makazini akitoboa mwaka bila increments
Anaweza kuongonza mgomo hapo kazini kwake Cha ajabu mtu huyo huyo kwake hawafanyii wafanyakazi wake.

Mimi vijana wanao nifanyia kazi Huwa nahakikisha kabisa na kujiridhisha kuwa jamaa huyu anaipenda kazi yake na nikiona faida na mshirikisha na mwambia Tena bila kinyongo namwambia mdgo wangu faida hii umeisababisha wewe ndio maana tumeipata hivo huu mwezi katika mkataba wako itaongezeka kiasi hiki Cha pesa.

Dogo lazima afurahi sana na atajituma sna na kuongeza bidii mnoo! Siku akizingua mwambie Tena dogo umezingua tumekula hasara hii jitahidi tuweze kufanikiwa pamoja!( Hapo hukati mshahara wake ikijirudia fanya adhabu kidogo tu usimuumize kama kukata hata 5k tu hii itategemeana na uzembe ulio fanyika).

Nimewahi kuishi na mfanyakazi huyu kwangu alikuwa zaidi ya mfanyakazi dogo alikuwa mtii,nidhamu, ucheshi na mpiga kazi hasa! Dogo huyu ilifikia wazazi wake nawatumia Hela mwenyew bila kugusa Hela yake. Sikukuu Moja niliwaomba wazazi wake waje tule pamoja kwangu nao wakaja tukasherehekea na waliondoka na zawadi kabambe!

Baada ya muda dogo akachoka kazi akaniaga kuwa aende kwao akawatunze wale ng'ombe aliokuwa ana nunua kipindi anafanya kazi kwangu na alikuja anamiaka14 tu akaondoka ana miaka 21.

Nilimuruhusu Kwa Baraka zote na pesa ya ziada nikampa Nje ya mkataba wake.
Ktk kipindi Iko dogo nilikuwa nimempa mbuga awe analima pia mpunga na alikuwa anavuna gunia4-7 Kwa mwaka.
Nazi nunua mwenyewe cash Hela anatuma kwao.

Baada ya kuchoka na kwenda wazazi wake walinipatia mdogo wake sema dogo hakudumu hakuwa na tabia nzuri tulikaanae miezi2 tu nikarudisha kwao.

Wale wazazi wakanitafutia wenyewe kijana mwingine. Yeye nae alikuwa mzuri Kwa kiasi chake alifanya kazi Kwa miezi7 akachoka akarudi.

Wapo wafanyakazi wenye tabia nzuri na mbaya na tunajua namna ya kuishi nao ikishindikana rudisha kwao.

Nimejifunza mengi sana katika kuboresha maslahi ya wafanyakazi kazi wetu majumbani Huwa wanakuwa na furaha sana na kumakinika katika utendaji kazi wao.

Pia wafanye kuwa marafiki zako ukienda shambani au kwenye mifugo Yako usianze kutoa lawama na kutukana tu Ili uonekane wewe ndo boss la hasha.

Mimi Huwa siitwi boss Huwa nawaambia waniite kaka tu inatosha na majina ya utani kabisa. Kama nipo mapumziko ni kazi kazi wote hakuna kusimamia.

Niishie hapa Kwa Leo .

karibuni sna.

Nje ya mada kidogo=> Nipo na heka3 za nyanya nikirutubishin gani kizuri Cha majani nitumie? Zipo katika Hali hii Kwa Sasa
 
Nyanya zipo katika Hali I hii Kwa sasa
IMG_20231223_183742_851.jpg
 
Uko sahihi ila kwa kumuongezea 10k kila mwezi akikaa miaka minne utakua unamlipa mpaka 500k, hio ni salary ya mtumishi wa halmashauri
Mkuu huo ni mfano kulingana na kazi anayo fanya. Mfano unafuga kuku &mbuzi kibiashara Hela hiyo ni kubwa? Au unalima mazao ya bustani

Mfano saivi dumu la lita20 nyanya linauzwa 27,000-30,000/= geita kijijni
Assume mlikuwa mmekubaliana Kwa mwezi 50,000 ukimuongeza hiyo Hela utapungukiwa ? Sidhani.

Cha msingi Angalia faida na mafanikio ulipofikia tangu ukiwa nae je amezalisha ipasavyo?
 
Wanatusaidia sana haswa wa shambani wanafanya kazi kwa uaminifu sana
Nakubaliana nawewe. Na ukitaka ku prove Hilo Angalia maisha ya shambani wanayoishi na maisha ya kwako nyumbani Angalia na msosi wao wengi huhemea Hivi
Marage kg5
Dagaa kg2
Mahindi debe1
Chumvi na vitunguu
Hakumbuki Hawa ndo wanazalisha zaidi wanastahili kutunzwa vilevile
 
Maji mvua haijanyesha kama siku 1 tu nauliza booster kama unaijua mkuu nisaidie au hakuna umhimu?
Booster ni muhimu, Kuna booster ya maua......hapo Cha muhimu piga sumu ya kulinda majani na booster.

Tulikua tunatumia ile pump ya 10L unaweka maji, unaweka sumu unachanganya na booster humo humo unapuliza nyanya zinakaa powa
 
Back
Top Bottom