Tuliowahi kufukuzwa kazi tukutane tupeane experience

Sector binafsi inabidi uwe mtu wa kufunika kombe sana mwanarahamu apite, uwe kunguru muoga uweze kudumu kwenye kazi moja mda mrefu na ujifunze majungu mambo yaende lakini sisi wengine dakika moja mbele kwa kweli tushazoea hali hii. Ni kama tu pepe kupewa card nyekundu na kutolewa nje
 
Kati ya vitu vinavyouma katika maisha ni kufukuzwa kazi, nakumbuka miaka kadhaa nyuma baada ya kumaliza degree yangu nikabahatika kupata kazi kwenye kitaasisi kimoja hivi.
Pole sana na hongera kwakupambana kiume
 
Huyo boss ni kama boss wangu wa sasa...

Nipo namlia timing tuu sku akijichanganya lazima nimtie hasara...
Lianzishe mkuu
Yani boss anaambia watu km hamjafunzwa kwenuu tena kwa nyodoooo kwenye kikao cha staff..will never regret quiting that job
 
Niliacha kazi mwaka 2018 mpaka leo najuta Kwa kweli naona bora nisinge acha kazi.Sijui wenzangu mnatumia mbinu gan kupata kazi Kwa haraka
Dah pole mkuu, kama kwenye ajira ulikuwa unapata milioni kwenda juu sawa , ila trust me, kama una mishe yako unapata hata 700k as faida per month hadi 1m komaa na biashara yako, na ukisema uajiriwe basi make sure take home inakuwa 1m kwenda juu, ila hizi 800k, wakikata unabaki na 500k stress tupu.
 
Back
Top Bottom