Tuliowahi kufukuzwa kazi tukutane tupeane experience

kiroka

JF-Expert Member
Feb 28, 2018
355
1,856
Kati ya vitu vinavyouma katika maisha ni kufukuzwa kazi, nakumbuka miaka kadhaa nyuma baada ya kumaliza degree yangu nikabahatika kupata kazi kwenye kitaasisi kimoja hivi.

Nikapiga kazi kwa kujituma sana aliekuwa boss wangu akawa ananichukia mno visa kila siku kikianza hiki kinakuja hiki nikawa Nina stress saana na kazi.

Mara nikajikuta naambiwa nimewatukana staff mate wenzangu yaani balaa juu ya balaa, nakumbuka nilienda likizo ya kawaida kama ilivyo haki ya mfanyakazi yoyote nikiwa likizo watu wa kazini wakanitonya kuwa kuna mtu kaajiriwa anafanya majukumu yangu ni balaa.

Siku narudi kazini namkuta mfanyakazi mpya kakalia kiti changu na anatumia computer yangu nikashindwa nikae wapi na nifanye majukumu gani mzee nikashinda bench siku nzima, baada ya happy tukawa tunafanya kazi kwa kupokezana kwenye computer nlokua natumia Mimi shida hizi jamani.

Basi bhana aliekuwa msaidizi wa boss wangu akaniita kiutu uzima akanambia hapa kazi hamna kama unaweza apply sehemu nyingine wenzio wanakusubiria uteleze kidogo tu wakule kichwa, nikabaki dilemma basi siku moja foleni za mjini hapa nikachelewa kuingia kazini kama dakika kumi hivi boss akawaandikia HR office kama hayupo tayari kufanya kazi na Mimi.

Hr mmoja akanambia kama naweza niandike resignation letter au nisubirie kufukuzwa nikaona maji yamekua mengi nikaandika barua ya kuacha kazi kwa mwezi mmoja boss akaacha kunifatilia tangu siku nlipoandika barua nikawa naingia kazini kiubish mpk mwezi ukaishi nikalipwa mafao yangu mambo yakawa yanasonga.

Ugumu wa kwanza baada ya kuacha kazi ni ile hali ya kuamka asubuhi hujui uende wapi, unajikuta unachukia sehemu ulokuwa unafanyia kazi hata kupapita hutaki tena marafiki wa kazini wanakutenga na wengine wanakupotezea kabisaa majirani na ndugu wanaanza kukusengenya usipojipanga unaweza kujiua.

Nashukuru Mungu niliweza kupambana na maisha bila kazi nimesimama tena nje ya ajira.
 
Kuna hoteli niliwahi fanya kazi ya utunza bustani wakati nasubiri majibu ya form four. Nilivyomaliza chuo nikaambiwa wananitafuta wanataka mtu wa store, nikaenda, tukakubaliana mshahara, ilikua ni 180K kwa mwezi, basi ikawa mziki mshahara ila nikakaza.

Basi bwana baada ya almost mwaka nikaitwa na meneja wa waswahili akaniambia bwana ni hivi mimi naona wewe kukulipa hatuwezi. Kichwani najiongelesha "Hawa jamaa wananilipa 180K lakini wanaona ni kubwa walitarget wanilipe sh ngapi?"

Kauli ya mwisho nikasikia "Kwahiyo tumeona tukuache" basi mambo yakawa hivyo.
 
Binafsi hadi nineisha zoea private nikifanya kazi najua kufukuzwa ni muda wowote tu.

Cha kwanza sinaga kumuogopa mtu awe boss awe nani yani hii hali inaniponza sometimes siwezi kunyenyekea..

Kazi za hospitali kupiga madili huwa kupo tu mala moja moja
Nimefanya kazi Zahanati nyingi sana sitoboi hata nusu mwaka nisha fukuzwa.

Ila nilipofukuzwa mala ya mwisho ndio inachekesha na kutia simanzi.
Nesi mmoja alikua ni mke wa mtu akawa ananitaka, shobo shobo kibao, mala akija job aseme amenimiss na kutaka kunikiss juu, mwamba nagoma.

Bwana hee nikapokeaga elfu 30 ya mgonjwa nikaichapa juu kwa juu.
Huyo nurse akajua, alinichoma kwa bosi live bila chenga.

Kilichoniuma sio kufukuzwa kazi, yani ni kuchomewa na demu ambae nilikua na uwezo wa kumla/ kuchapa mashine na tukashirikiana vizuri kila sector
 
Sitaki kukumbuka kampuni ile, natakiwa kusimamia stocktaking and at the same time natakiwa kwenda manunuzi , cable zikaibiwa ...... Huku na kule nina fundi amepata kazi ya nje ya kusupply cable ukubwa tofauti hawezi kuwasiliana na kampuni ile kwa sababu barua zinatakiwa ziwe in english, nikamfanyia ile kazi, kumbe wenyewe wakasupply cable tofauti na ile waliyohitajika kusupply hivyo yule jamaa akapewa barua ya kurejct ile cable hivyo akanitumia mimi nimsomee kisha nimwambie inahusu nini na walipaswa kurejesha 5M ambayo walipewa before supply of that cable.

Hiki kilikua kipindi cha corona sasa zile homework za watoto shule walikua wanatutumia wazazi ikawa naprint ofisini sijui nini kilitokea na ile barua boss akaipata ya rejected cable ambayo walipaswa kurwjesha ile 5 M wakachanganya na ka cable ka 2.5 kalikopotea yani hapo ndo mambo yakawa magumu mpika nikaandika barua mwenyewe ya kuacha kazi kwa kuwa wanasema sitakiwi kufanya kazi za nje zinazohusiana na umeme kabisa kwa sababu lazima waone ni mwizi
 
Binafsi hadi nineisha zohea private nikifanya kazi najua kufukuzwa ni muda wowote tu.

Cha kwanza sinaga kumuogopa mtu awe boss awe nani yani hii hali inaniponza sometimes siwezi kunyenyekea..

Kazi za hospitali kupiga madili huwa kupo tu mala moja moja
Nimefanya kazi Zahanati nyingi sana sitoboi hata nusu mwaka nisha fukuzwa.

Ila nilipofukuzwa mala ya mwisho ndio inachekesha na kutia simanzi.
Nesi mmoja alikua ni mke wa mtu akawa ananitaka, shobo shobo kibao, mala akija job aseme amenimiss na kutaka kunikiss juu, mwamba nagoma.

Bwana hee nikapokeaga elfu 30 ya mgonjwa nikaichapa juu kwa juu.
Huyo nurse akajua, alinichoma kwa bosi live bila chenga.

Kilichoniuma sio kufukuzwa kazi, yani ni kuchomewa na demu ambae nilikua na uwezo wa kumla/ kuchapa mashine na tukashirikiana vizuri kila sector
Huwez jua man
Pengne angekupa Arv
 
Huwez jua man
Pengne angekupa Arv
Hahahaaaaa Ningemtia tu hata kwa kondom, kwanza ningetaka kumla peku ningempima tu kwanza.

Ila ni kusudi la Mungu najua alitaka nisiendelee kufanya kazi hapo, maana kuna sheikh alikua anataka kunipanda kichwani... kwenye Zahanati ya Bakwata.

Na mimi kipindi hizo nimezama kiroho balaa,,
Yani nilikua nataka kumuoneshea Jina la Yesu lilivo na nguvu na usheikh wake nilimwambia hunibabaishi kitu
 
Binafsi hadi nineisha zoea private nikifanya kazi najua kufukuzwa ni muda wowote tu.

Cha kwanza sinaga kumuogopa mtu awe boss awe nani yani hii hali inaniponza sometimes siwezi kunyenyekea...
Mimi nimewahi kufundisha shule fulani private. Mkuu wa shule alikuwa na mambo ya kiwaki kisenge.

Sometimes, anaweza kukufokea hata mbele ya wanafunzi.

Ikifikia tarehe za mishahara basi ndio kufoka nje nje. Nyumba niliyokuwa nimepewa ilikuwa karibu na ya kwake, so, sometimes washkaji wakija gheto mkawa mnaongea kwa nguvu mnabishana mnacheka, anawaibukia anafoka Walimuu mnapiga kelele kama watoto wa primary🤣

Nikawa najisemea tu huyu dawa yake iko jikoni.

Kuna wakati tunakaribia kuchukua mshahara, mwisho wa mwezi akawa anafoka, ooh kama hujaandika scheme of work na lesson plans sikulipi mshahara 🤣 (walimu wanaijua hii midude.

Basi nikajipinda nikaandika hayo ma-scheme of works ( plan ya miezi 6 ) na lesson plans, nilivyomaliza nikampelekea.

Akasema poa, nenda kwa Accountant akupe mshahara wako. Nilivyolipwa tu, nitatafuta muda huyo mkuu wa shule hayupo, nikaiingia ofisini kwake nikayaiba hayo scheme of works nikaenda nikayachoma moto halafu nikaacha kazi, nikasepa🤣. Ilikuwa 2013 hiyo.

Kiukweli mimi kuvumilia dharau nilishashindwa kabisa. Siwezi.

Mimi chuoni nimewahi kumfuata Lecturer ( HoD ) ofisini kwake nikamtukana. Alikuwa ananisumbua sana.

Mimi probably nitakuja kumnyenyekea mtu nikiwa na watoto 6, mmoja ana ugonjwa wa kudumu, nadaiwa kodi ya nyumba, mama ana matatizo.

Hapo nitajitahidi kunyenyekea. Kwasasa nitakuwa muongo. Sitaweza.
 
Kati ya vitu vinavyouma katika maisha ni kufukuzwa kazi, nakumbuka miaka kadhaa nyuma baada ya kumaliza degree yangu nikabahatika kupata kazi kwenye kitaasisi kimoja hivi...
Pole sana. Ila watu wengi sana wanaonewa makazini na kufukuzwa kazi au kuresign kwa sababu tu hawajui haki zao kama wafanyakazi.

Kama hapo wewe ulichotakiwa kufanya ni usinge resign, usubiri jamaa wakufukuze kwa kosa hilo moja tu; Ungewaendesha sana iwapo baada ya wao kukufukuza ungeenda kwenye vyombo vya utetezi kama tume ya usuluhishi wa migogoro sehemu za kazi (CMA).

Maana mfanyakazi hafukuzwi kazi kirahisi hivyo, lazima kuwe na ushahid kwamba alishaonywa mara kadhaa, sio kosa lake la kwanza na mambo kama hayo, ukipeleka kesi kama hiyo kwa jamaa wa CMA hao waajiri wako wangekukoma; na wangeamuriwa kukulipa fidia ya kutosha tuu.

Tena kwa taasisi za binafsi ndo huwa CMA wanawakalia zaidi kooni. Ila ndo hivyo pia waru wengi hata hawawajui hao CMA.

But anyways, god for you kwamba you have moved on na maisha yameendelea! kiroka
 
Mimi nimewahi kufundisha shule fulani private. Mkuu wa shule alikuwa na mambo ya kiwaki kisenge.

Sometimes, anaweza kukufokea hata mbele ya wanafunzi...
Alafu kibaya zaidi pesa unayo lipwa unakuta ya dharau vibaya mno.

Sina mke pesa ninayolipwa peke yangu tu hainitoshi sasa nikiongeza na mwanamke itakuaje. !?

Nakumbuka niliwahi kufanya kazi sehemu nalipwa laki 2 kwa mwezi,
Alafu kuna jamaa angu, alikua jobless nakaa nae mala akapata kazi, kasoma inshu za kusfisha madini.
Jamaa miezi sita ya mwanzo tu mshahara ni m 1.4 aisee hapo ndo niliposanuka sipo sehemu sahihi hata kidogo.

Haya maisha sio ya kubweteka na kaajira ka private unafanyishwa kazi zaidi ya masaa 8 kwa siku na hakuna cha mafao wala nini.
 
Back
Top Bottom