Tuliowahi kufukuzwa kazi tukutane tupeane experience

Kuna wafanyakazi airport wamefukuzwa Kazi baada ya kupokea asante kwa kuhudumia abiria vizuri.Unamfukuza Kazi mtu kisha kapewa elf 5 kama Asante.Uonevu mtupu halafu kuna mijizi inapiga mamilioni inahamishwa tu wizara au halmashauri
 
Kati ya vitu vinavyouma katika maisha ni kufukuzwa kazi, nakumbuka miaka kadhaa nyuma baada ya kumaliza degree yangu nikabahatika kupata kazi kwenye kitaasisi kimoja hivi.

Nikapiga kazi kwa kujituma sana aliekuwa boss wangu akawa ananichukia mno visa kila siku kikianza hiki kinakuja hiki nikawa Nina stress saana na kazi.

Mara nikajikuta naambiwa nimewatukana staff mate wenzangu yaani balaa juu ya balaa, nakumbuka nilienda likizo ya kawaida kama ilivyo haki ya mfanyakazi yoyote nikiwa likizo watu wa kazini wakanitonya kuwa kuna mtu kaajiriwa anafanya majukumu yangu ni balaa.

Siku narudi kazini namkuta mfanyakazi mpya kakalia kiti changu na anatumia computer yangu nikashindwa nikae wapi na nifanye majukumu gani mzee nikashinda bench siku nzima, baada ya happy tukawa tunafanya kazi kwa kupokezana kwenye computer nlokua natumia Mimi shida hizi jamani.

Basi bhana aliekuwa msaidizi wa boss wangu akaniita kiutu uzima akanambia hapa kazi hamna kama unaweza apply sehemu nyingine wenzio wanakusubiria uteleze kidogo tu wakule kichwa, nikabaki dilemma basi siku moja foleni za mjini hapa nikachelewa kuingia kazini kama dakika kumi hivi boss akawaandikia HR office kama hayupo tayari kufanya kazi na Mimi.

Hr mmoja akanambia kama naweza niandike resignation letter au nisubirie kufukuzwa nikaona maji yamekua mengi nikaandika barua ya kuacha kazi kwa mwezi mmoja boss akaacha kunifatilia tangu siku nlipoandika barua nikawa naingia kazini kiubish mpk mwezi ukaishi nikalipwa mafao yangu mambo yakawa yanasonga.

Ugumu wa kwanza baada ya kuacha kazi ni ile hali ya kuamka asubuhi hujui uende wapi, unajikuta unachukia sehemu ulokuwa unafanyia kazi hata kupapita hutaki tena marafiki wa kazini wanakutenga na wengine wanakupotezea kabisaa majirani na ndugu wanaanza kukusengenya usipojipanga unaweza kujiua.

Nashukuru Mungu niliweza kupambana na maisha bila kazi nimesimama tena nje ya ajira.
Mkuu uko sahihi sana, usipojipanga unaweza fanya nini vile.............
 
Kuna hoteli niliwahi fanya kazi ya utunza bustani wakati nasubiri majibu ya form four. Nilivyomaliza chuo nikaambiwa wananitafuta wanataka mtu wa store, nikaenda, tukakubaliana mshahara, ilikua ni 180K kwa mwezi, basi ikawa mziki mshahara ila nikakaza.

Basi bwana baada ya almost mwaka nikaitwa na meneja wa waswahili akaniambia bwana ni hivi mimi naona wewe kukulipa hatuwezi. Kichwani najiongelesha "Hawa jamaa wananilipa 180K lakini wanaona ni kubwa walitarget wanilipe sh ngapi?"

Kauli ya mwisho nikasikia "Kwahiyo tumeona tukuache" basi mambo yakawa hivyo.

We are hiring
 
Mimi nimewahi kufundisha shule fulani private. Mkuu wa shule alikuwa na mambo ya kiwaki kisenge.

Sometimes, anaweza kukufokea hata mbele ya wanafunzi.

Ikifikia tarehe za mishahara basi ndio kufoka nje nje. Nyumba niliyokuwa nimepewa ilikuwa karibu na ya kwake, so, sometimes washkaji wakija gheto mkawa mnaongea kwa nguvu mnabishana mnacheka, anawaibukia anafoka Walimuu mnapiga kelele kama watoto wa primary

Nikawa najisemea tu huyu dawa yake iko jikoni.

Kuna wakati tunakaribia kuchukua mshahara, mwisho wa mwezi akawa anafoka, ooh kama hujaandika scheme of work na lesson plans sikulipi mshahara (walimu wanaijua hii midude.

Basi nikajipinda nikaandika hayo ma-scheme of works ( plan ya miezi 6 ) na lesson plans, nilivyomaliza nikampelekea.

Akasema poa, nenda kwa Accountant akupe mshahara wako. Nilivyolipwa tu, nitatafuta muda huyo mkuu wa shule hayupo, nikaiingia ofisini kwake nikayaiba hayo scheme of works nikaenda nikayachoma moto halafu nikaacha kazi, nikasepa. Ilikuwa 2013 hiyo.

Kiukweli mimi kuvumilia dharau nilishashindwa kabisa. Siwezi.

Mimi chuoni nimewahi kumfuata Lecturer ( HoD ) ofisini kwake nikamtukana. Alikuwa ananisumbua sana.

Mimi probably nitakuja kumnyenyekea mtu nikiwa na watoto 6, mmoja ana ugonjwa wa kudumu, nadaiwa kodi ya nyumba, mama ana matatizo.

Hapo nitajitahidi kunyenyekea. Kwasasa nitakuwa muongo. Sitaweza.

Kweli wewe mkaruka Mkaruka
 
Amemaanisha hiyo ultavet haikuwa mtego? Iliishaje hii ishu yako pale Lead?
Utravet haikuwa mtego,mm sikwenda kwa kuwa tayari nilikuwa na mkataba na LEAD PROJECT,na Niko govt tayr,so nikaamua nimwambie ukweli Yule manager wa utravet ,nakumbuka email yake ilianza kwa jina la laagie.somethin hiv,so nikaamua kum connect jamaa angu aliitwa somebody msoka,from tanga.manager wa utravet akaniambia jamaa yuko vizur nikamwambia yes,akasema mwambie atume maombi kwa email,Ila huyu tutampiga interview tukiona anafaa basi tutampa offer,nikampa contact jamaa angu awasiliane nae,ofcoz jamaa alienda wakampiga interview baadae ,akaenda Nairobi Kenya kwa 2weeks seminar.alipiga nao kazi.
 
Niliacha kazi mwaka 2018 mpaka leo najuta Kwa kweli naona bora nisinge acha kazi.Sijui wenzangu mnatumia mbinu gan kupata kazi Kwa haraka
hakikisha unaongea vizuri na walinzi wa hiyo kampuni/ofisi wakukonnect na HR, then ukipata chance ipambanie.
 
Nilikuwa nafanya kazi mahali ila asee kauli za yule boss ililuwa kama anaongoza vitoto via nursery school. Halafu anaogopwa hatari. Akipatikana mchapa kazi na anayetoa mapendekezo ya nini kifanyike kampuni iboreshwe anamfukuza . Kifupi hakutaka maoni wala kunyanyua kichwa.

Na alikuwa fukuza fukuza na kila siku pale wanaajiri. Basi nikapata dharura ya kifamilia nikapotea miezi 2 na sikupanga kirudi ikawa ndio ticket ya wao kunisimamisha.

Japo supervisor alikuwa mchongeaji hatariii (najua we mdada umechongea wengi na umeharibu maisha ya wengi ila kumbuka KARMA is a bitch 40 yako itakuja tu).
Huyo boss ni kama boss wangu wa sasa...

Nipo namlia timing tuu sku akijichanganya lazima nimtie hasara...
 
miaka kumi na ushee iliyopita....
Nilikiwa kwenye ajira kwenye kampuni niliyufanyia kazi kwa zaidi ya miaka nane katika vitengo tofauti tofauti kwa ufanisi mzuri tuu,sasa nikiwa mkoani tukaitwa Makao makuu kwa ajili ya kujifunza system mpya ya kazi, tulivyomaliza wakati narudi kituo changu wakati tunakabidhiana kazi na msaidizi wangu nikagundua upotevu wa vifaa ambavyo thamani yake ilikuwa ni kama milioni 2 hivi,nilikuwa na uwezo wa kulificha hili au kulimaliza kichinichini ila baada ya kugundua upotevu ule haukumhusisha msaidizi wangu nikaamua kuliripoti makao makuu kwa hatua za ziada,ikiwa ni pamoja na kuwaelezea ninavyohisi upotevu umetokea na vielelezo ambavyo wangevitumia ilikuwa rahisi kubaini upotevu huu,baada ya muda alitumwa mkaguzi wa ambae alikuja kuangalia lilivyotoea,(mbwa sana yule mhindi)..alinilazimisha kuandika kuwa kosa amelitenda msaidizi wangu ili achukuliwe hatua,nilimwambia siko tayari kuchuma hiyo dhambi na kama anadhani kosa lipo basi nitalibeba mimi,story ni ndefu ila baadae nlikuja kuitwa kwa mahojiano yaliyochukua zaidi ya siku tatu na waliokuwa wanasimamia wakanikandamiza kuwa kosa limetendeka chini yangu hivyo ni kosa langu, (wapuuzi wale walikuwa wanafanya kazi kwa kulamba lamba makalio ya wazungu ili waonekane wanajua wanachokifanya)baada ya kuona mwelekeo niliamua kufuatilia upotevu huo kivyangu bila kushirikisha ofisi ambapo nilifanikiwa kuwanasha waliofanya uhalifu huo na kuwafikisha mahakamani na wakahukumiwa kifungo,hili nililifanya bila kutoa taarifa ofisini,hatimae baada ya muda nilipewa barua ya kufukuzwa kazi bila ya kujua kuwa nilishalifanyia kazi na kufanikiwa kuwakamata wahalifu waliohusika, niliipokea barua kwa furaha kiasi kwamba hata walioniletea barua walibaki wananishangaa,niliwakabidhi pesa ya ofisi kama milioni 35 ambayo ningeweza kupotea nayo,nilivyomalizana nao nikaenda kufungua kesi CMA,kule wakaniwahi wakamrubuni wakili wangu akawa hahudhurii mahakamani mwishoe nikashindwa,nikatafuta wakili mwingine nika appeal,huyu walimfuata kumhonga wakashindwa, mlolongo ulikuwa mrefu lakini hatimae nilishinda na walinilipa stahiki yangu tosha kabisa,nashukuru wakati kesi inaendelea nilianza kujishughulisha na biashara ndogo ndogo na zilifanikiwa kwa kiasi kizuri tuu, wale wapuuzi walionikandamiza kuna wengine nakutana nao mitaani wamepauka hadi meno, niliifanya kazi kwa moyo sana lakini baada ya tukio hili nilichana vyeti vyangu vyotena kuvitia moto ili nisikumbuke tena kutafuta ajira... ...
 
Mkuu hongera khaaa!

We kabila gani?
 
Binafsi hadi nineisha zoea private nikifanya kazi najua kufukuzwa ni muda wowote tu.

Cha kwanza sinaga kumuogopa mtu awe boss awe nani yani hii hali inaniponza sometimes siwezi kunyenyekea..

Kazi za hospitali kupiga madili huwa kupo tu mala moja moja
Nimefanya kazi Zahanati nyingi sana sitoboi hata nusu mwaka nisha fukuzwa.

Ila nilipofukuzwa mala ya mwisho ndio inachekesha na kutia simanzi.
Nesi mmoja alikua ni mke wa mtu akawa ananitaka, shobo shobo kibao, mala akija job aseme amenimiss na kutaka kunikiss juu, mwamba nagoma.

Bwana hee nikapokeaga elfu 30 ya mgonjwa nikaichapa juu kwa juu.
Huyo nurse akajua, alinichoma kwa bosi live bila chenga.

Kilichoniuma sio kufukuzwa kazi, yani ni kuchomewa na demu ambae nilikua na uwezo wa kumla/ kuchapa mashine na tukashirikiana vizuri kila sector
K ikakuchoma
 
Hahahaaaaa Ningemtia tu hata kwa kondom, kwanza ningetaka kumla peku ningempima tu kwanza.

Ila ni kusudi la Mungu najua alitaka nisiendelee kufanya kazi hapo, maana kuna sheikh alikua anataka kunipanda kichwani... kwenye Zahanati ya Bakwata.

Na mimi kipindi hizo nimezama kiroho balaa,,
Yani nilikua nataka kumuoneshea Jina la Yesu lilivo na nguvu na usheikh wake nilimwambia hunibabaishi kitu
Sasa alikutupia jini la wizi
 
Back
Top Bottom