Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Mikopo inaumiza sana. Tangu nimalize mikopo, sina deni now sidaiwi na mtu, basi nalala usingizi mnono kama mtoto mchanga. Nilishawahi kukopa milioni kumi nikaongezea na za kwangu nikanunua gari ya biashara. Ndani ya mwezi mmoja gari ikala mzinga. Niliteseka sana kulipa deni na kuishi kigumu gumu. Nimeshaapa siku mtu akinona najaza fomu kuchukua mkopo kwenye taasisi ya fedha, basi mtu huyo anichinje kwa msumeno!
Nimecheka sana na kwa sauti ya juu .
 
Hii mada inafundisho jamani nataka kukopa kama m50 ninanyumba nimepangisha napata kodi nzuri tu kama 2.5 m kwa mwezi ila ninanyingine nimeanza kujenga ili nimalize nahitaji m 50 za haraka plan yangu kodi ya kule ilipe hilo deni ila kwa kusoma mada hizi nimeingia uoga mimi sifanyi kazi nafanya shughuli zangu tu naombeni ushauri kwa wazoefu wa mikopo
 
Wewe uko vizuri, huwezi pata shida. Chukua tu.
 
Wewe uko vizuri, huwezi pata shida. Chukua tu.

Ila nimepitia post nzima naona kila aliyechukua kapata matatizo nataka kujua naomba je m50 wanataka ngapi kwa mwezi na kwa muda gani je wanamuda walioupanga mfano lazima miaka 5 tu au unaweza kuchukua muda mrefu nahitaji ufafanunuzi zaidi kabla sijaingia kwenye deni naogopa sana madeni
 
huu uzi nimeusoma mwanzo mwisho......kila mtu ametoa lake la moyoni kuhusu changamoto alizopitia baada ya kuchukua mkopo....
changamoto nilizoziona ni:

a. mtu anakopa kabla ya kubuni afanye nn na hizo hela
b. mtu anakopa anaanzisha project anamweka ndugu
c. mtu anakopa, pale mwanzo kabla ya kuanzisha project anajikuta anazitumbua wee kuja kustuka robo au nusu ya hela inakua imeshakata

d. mtu unakopa let say 10mil, unajitutumua pale mwanzo mara paap 1m inapotea bila kufanya la maana, mara umenunua hiki, mara ulikua na kiporo cha deni siku nyingi, theni iliyobakia unatafuta frem kwa mda wa mwezi(nimekadiria mwezi kwa sababu unaweza pata sehem ambayo hujaridhika nayo kwa mazingira ya biashara,) unapata unalipia kodi, unanunua vitu muhimu kama fridge, mizani, meza, kiti, kabati, unatafuta leseni, mara paap inabaki na 3mil, unafungua kiduka kidogo biashara inayumba hapo unaanza kukabwa marejesho... ni lazma ufeli tu na kama uliweka nyumba dhamana itauzwa maana hauna namna... kwa wale waajiriwa hiki kipindi utakua unaishi kama lucifer mkuu..

ushauri
a. usikope hela kabla ya kujua hela utaifanyia nini, tena uwe na taarifa sahihi khs utakachokifanya mfano ufugaji, biashara ama kilimo
b. usikope hela ukajenge au ununue kiwanja, kopa hela uifanyie project hela iwe inazunguka
c.usikope hela ukaanzishe project ambayo hukuwahi kuifanya before, hata kama unazo taarifa sahihi khs unachotaka kwenda kukifanya, lazima utafeli
d. mkopo mzuri ule ambao unakopa kupanua kile ambacho tayari unacho mfano, una biashara yako ushaijulia mzunguko wake, lakn una mtaji mdogo, unaweza kukopa hela ukainedeleza
e. hii ni njia nzuri zaidi, ili ufaidi mkopo wako fanya haya... tufanye mfano wa duka,,, chukulia una duka moja lenye thamani ya 10mil,linakulipa vzr tu na mzunguko uko poa, then ghafla ukapata dili lingine mfano ufugaji wakuku, na inahtaj 4mils. kw a haraka haraka hiki kiasi ni kikubwa sana compared na mtaji wako wa 10mils, kuzipata mara moja ni ngumu hapa utalazimika kukopa,,

Sasa ukikopa fanya hivi, tengeneza utaratibu wa kufanya serving kwenye ile biashara yako then ufanye marejesho, mdogo mdogo, then ule mradi uliofungua kwa mkopo uwe unakua taratibu, aft one year piga hesabu angalia ni nini ambacho umeambulia kama faida ? then jilipe mwenyewe kwa kuwa ulikua unajikopa kwenye duka kulipa marejesho, hapo utajua faida na hasara iko wapi
 
Ila nimepitia post nzima naona kila aliyechukua kapata matatizo nataka kujua naomba je m50 wanataka ngapi kwa mwezi na kwa muda gani je wanamuda walioupanga mfano lazima miaka 5 tu au unaweza kuchukua muda mrefu nahitaji ufafanunuzi zaidi kabla sijaingia kwenye deni naogopa sana madeni
Mikopo mingi inayotolewa kwenye mabenk na taasisi za fedha huwa haizidi mienzi 72 sasa na miaka 6,

Hakuna anayeweza kufanikiwa,bila kujaribu ama kuthubutu usiogope kwa uliyoyasikia Bali uwe makini sana.
Mkopo ni mzuri na wenye manufaa ikiwa unajitambua,unajua nini ufanye na kwa namna IPI.

Ukipitia story za wakuu hapo juu,utagundua wengi hawakuwa serious na mikopo waliyochukua,kuaminiana kulikopitiliza,kutokujiamin,na kukurupuka ndo kumechangia kuwaangusha,

Binafsi Nina mifano hai ya jinsi Jamaa zangu wawili walivyofanikiwa kimaisha kupitia mikopo.

Kitu muhimu ni kujitambua,kujua lengo lako,kulitekeleza na kulisimamia kwa ufanisi,Mengine ni kudra za Mungu tu.

Ila mkopo sio m,baya kama unavyodhanishwa.
 
huu uzi nimeusoma mwanzo mwisho......kila mtu ametoa lake la moyoni kuhusu changamoto alizopitia baada ya kuchukua mkopo....
changamoto nilizoziona ni:
a. mtu anakopa kabla ya kubuni afanye nn na hizo hela
b. mtu anakopa anaanzisha project anamweka ndugu
c. mtu anakopa, pale mwanzo kabla ya kuanzisha project anajikuta anazitumbua wee kuja kustuka robo au nusu ya hela inakua imeshakata
d. mtu unakopa let say 10mil, unajitutumua pale mwanzo mara paap 1m inapotea bila kufanya la maana, mara umenunua hiki, mara ulikua na kiporo cha deni siku nyingi, theni iliyobakia unatafuta frem kwa mda wa mwezi(nimekadiria mwezi kwa sababu unaweza pata sehem ambayo hujaridhika nayo kwa mazingira ya biashara,) unapata unalipia kodi, unanunua vitu muhimu kama fridge, mizani, meza, kiti, kabati, unatafuta leseni, mara paap inabaki na 3mil, unafungua kiduka kidogo biashara inayumba hapo unaanza kukabwa marejesho... ni lazma ufeli tu na kama uliweka nyumba dhamana itauzwa maana hauna namna... kwa wale waajiriwa hiki kipindi utakua unaishi kama lucifer mkuu..

ushauri
a. usikope hela kabla ya kujua hela utaifanyia nini, tena uwe na taarifa sahihi khs utakachokifanya mfano ufugaji, biashara ama kilimo
b. usikope hela ukajenge au ununue kiwanja, kopa hela uifanyie project hela iwe inazunguka
c.usikope hela ukaanzishe project ambayo hukuwahi kuifanya before, hata kama unazo taarifa sahihi khs unachotaka kwenda kukifanya, lazima utafeli
d. mkopo mzuri ule ambao unakopa kupanua kile ambacho tayari unacho mfano, una biashara yako ushaijulia mzunguko wake, lakn una mtaji mdogo, unaweza kukopa hela ukainedeleza
e. hii ni njia nzuri zaidi, ili ufaidi mkopo wako fanya haya... tufanye mfano wa duka,,, chukulia una duka moja lenye thamani ya 10mil,linakulipa vzr tu na mzunguko uko poa, then ghafla ukapata dili lingine mfano ufugaji wakuku, na inahtaj 4mils. kw a haraka haraka hiki kiasi ni kikubwa sana compared na mtaji wako wa 10mils, kuzipata mara moja ni ngumu hapa utalazimika kukopa,, sasa ukikopa fanya hivi, tengeneza utaratibu wa kufanya serving kwenye ile biashara yako then ufanye marejesho, mdogo mdogo, then ule mradi uliofungua kwa mkopo uwe unakua taratibu, aft one year piga hesabu angalia ni nini ambacho umeambulia kama faida ? then jilipe mwenyewe kwa kuwa ulikua unajikopa kwenye duka kulipa marejesho, hapo utajua faida na hasara iko wapi
Mkuu kwenye ushauri hapo hiyo c sijakubaliana nayo
 
Mimi nilikopa mwaka jana NMB Mi. 9 kwa miaka mitano. Nikachukua pikipiki mbili. Moja ya bodaboda na nyingine ya kwangu kutembelea. Mil.4 nikachukua kiwanja na shamba kwa ajili ya kilimo. Laki 5 nikalimisha shmaba na kupanda mahindi na laki tano nikafanyia mambo yangu menginene. Mshahara nikabaki 247,000

Matokeo yake;

i)Bodaboda ilidumu miezi sita ikaibiwa.
ii) mahindi sikupata hata nusu gunia,kwa sababu ya ukame.
iii)mipango yangu ilikuwa mwaka huu nioe kama mambo yangeenda vizur kinyume chake nimeshindwa,mchumba wangu alipoona hali imekuwa tete akaanza visa kumbe kashaanza mahusiano na mwanaume mwingine,nikabaki mimi kama mimi.
iv)Baada ya bodi ya mkopo kuanza kukata 15% nikaanza kuchukua 197,000/= kwa mwezi
v) kwa sasa siwezi saidia chochote kwa mama na ndugu zangu kibaya zaidi mdogo wangu kachaguliwa chuo cha afya diploma ada mil.2. 5 sijaweza kumpa hata mia.

Sina bahati kabisa
Pole sana kiongozi, bado unaweza pata nafasi ya kufanya jambo lingine na kukuza kipato chako Mwenyezi Mungu akusaidie.
 
Huu uzi nimeuona punde tu ulivyo anzishwa lakin nilisita kuchangia kutokana na maswahibu yaliyo nipata...Mikopo ilinifanya mpaka nikaathirika kisaikolojia...ingawa bado sija recover....nimeona nisitia neno kwanza...nijipe mda kidogo niweze kusahau...

Nilichanganyikiwa kweli kweli...ilifikia hatua hata bara bara ya vumbi navushwa na watoto wadogo....Mweh..Ndugu zangu kuwen makini na mikopo...na hiz banks za Tz nyingi ni wafanya biashara sidhan kama zina malengo ya kumnufaisha mkopaji...zina interest kubwa...kiasi kwamba lazma uwe makin sna..
 
Huu uzi nimeuona punde tu ulivyo anzishwa lakin nilisita kuchangia kutokana na maswahibu yaliyo nipata...Mikopo ilinifanya mpaka nikaathirika kisaikolojia...ingawa bado sija recover....nimeona nisitia neno kwanza...nijipe mda kidogo niweze kusahau...nilichanganyikiwa kweli kweli...ilifikia hatua hata bara bara ya vumbi navushwa na watoto wadogo....Mweh..Ndugu zangu kuwen makini na mikopo...na hiz banks za Tz nyingi ni wafanya biashara sidhan kama zina malengo ya kumnufaisha mkopaji...zina interest kubwa...kiasi kwamba lazma uwe makin sna..

Pole jamani lakini masharti yao yanakuwaje ili wakupe mkopo vigezo gani unatumia kama si mwajiriwa au ndio unaweka hati kama dhamna
 
Nimemaliza chuo mwaka jana imefika wakati n nimeamin mtaji ndo changamoto kwangu lkn nikahisi bank anaweza kuwa mkombozi wangu lkn kwa uzi huu nimekuwa mwoga ghafla mpaka kichwa kinaniuma dah
Usiogope bwana ndo mana hawa wenzetu kwa upendo mkubwa wameamua kuchukua risk ya kuweka true story zao hapa za namna walivyotumia mikopo yao VIBAYA. Unafikiri ni kwa nini? Ni kwa sababu mimi na wewe TUJIFUNZE tusije kutumbukia tena kwenye makosa kama yao wakati tumeshaambiwa. So jifunze kutoka kwenye MAKOSA ya wenzetu!!
 
Ni sahihi mkuu na nimekuelewa bt kikubwa kinachonitisha shuhuda zote ni za maumivu tupu hakuna alifaidika kupitia mkopo dah
 
Back
Top Bottom