Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Kv-london

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
2,823
4,829
Habar wapendwa humu JF

Bila kupoteza muda katika pulukushani za maisha kuwa magumu kuna wakati unaona the only solutions ni kuchukua mkopo katika taasisi za fedha mbalimbali ili kufungua ofisi nyingine itakayokuingizia kipato zaidi.

Ila cha kushangaza sasa unakuta tunaangukia pua na maisha kuwa tete zaidi ya hapo nyuma ilivyokuwa.

Mfano ni mimi; 2013 nilikopa 5 milions kwenye benki ya NMB kwa muda wa miaka 4 ambapo nilipanga kufungua biashra zangu mjini ili sister angu ndio azisimamie huko town basi nikaongea nae akanipa michongo yake ya biashara za mahindi zinavyomlipa anatoa mahindi Dodoma anapeleka Dar.

Akaniambia mimi nitakuwa napata laki 300000 kila atakapouza mzigo at the same time my capital remains costant. Mimi nikachukulia kama biashara ndio hivyo basi nitatengeneza pesa ndefu ndani ya muda mfupi sababu ndani ya mwezi anaenda kufunga Mzigo Mara 3.

Nikamtumia 4.5 milions kwa akaunti na ile laki tano kama kawa nikaitia kibiriti na Toto's za mjini nkajua after 1 week ntaanza kupokea pesa zangu za faida. Hapo salary nlikuwa napokea 190000 net baada ya makato yote.

Kumbe nae sister ndio kawa tycoon wa mjini anazitumbua pesa tu na vibwana vyake mpaka na kuja kumpigia sim vipi mbona kimya hunitumii ile pesa yani amelewa haezi hata kuongea.

Nikampigia kesho yake eti akaniambia aliibiwa pesa yote na hapo alipo amebakiwa na laki 3 tu na ndio anataka alipe kodi ili asifukuzwe kwenye chumba alichopanga. Nilikaaa chini bado nusu nilie ila nikajikaza kiume namshukuru Mungu nlikuwa sina mke wala mtoto.

Maisha yakawa magumu zaidi loan board walipoanza kunikata nikawa sasa kutoka 190000 nkawa napokea salary 135000 na madeni yalikuwa yameniandama sana sikuona raha ya kufanya kazi sababu nlishidwa kumsaidia mtu yeyote nyumbani sio baba wala mama wala ndugu yeyote.

Mungu sio wewe wala mimi; mwaka huu deni likaisha na namshukuru Mungu naishi maisha ya furaha na mwaka huu nitaenda nyumban kuwasalimia since 2012 sijawahi kwenda kabisa.

Kwa wale mliochukua mikopo jamani kuweni makini na yale mtakayoenda kufanya msije mkachanyikiwa mkatamani kujinyonga kama mimi.
 
Kutapeliwa na ndugu/rafiki wa karibu inauma sana maana huna hata la kumfanya
Yan habar hiyo isikie tu kwa mwenko
Kina jamaa alikuwa ughaibuni huko akawa anamtumia baba yake pesa amjengee nyumba na Raman akamtumia

Jamaa akarudi kumuulisa mshua nyumba iko WAP hamna nyumba ndio kwanza amechimba msingi na alishatafuna kama 75mls.

Sasa kama ndio ww utamfunga mzee wako au
Jamaa ucku ule ule aligeuka wakaenda kulala kwa hitel keshokesho yake hao Japan na mkewe
 
Duu pole!watumishi pesa zao nyingi zimeteketea kwa kuwa miradi wanayobuni inasimamiwa ndugu,jamaa ama rafiki.Ambapo matokeo utakayoyapata ni majibu ya kisanii kama hayo.Maana take ulikuwa unafanya biashara kwa simu,ila nashukuru kwa kutufungukia kwani ni wachache wenye moyo huo.
 
Hii D9 hii ilitaka kunipiga dole la kijambio...
Jamaa yangu alinishawishi sana nitafute 4.8 Millioni nijiunge package ya Gold+ ya D9.
Kwa mahesabu ni kuwa kila week nalipwa 170 USD, hivo kwa mwezi napata 630 USD (baada ya makato) ambayo ni zaidi ya 1.3 Millioni.
Hivo nilikua na uhakika ule mtaji wa 4.8 Millioni ningerudisha ndani ya miezi mitatu hivi na week mbili...

Nikaenda kuomba mkopo taasisi moja hivi, mkopo wa 5 Millioni. Marejesho jumla ningetakiwa kulipa 6.5 Millioni.

Mkopo ilikua nipate cku hiyo hiyo tatizo nilikua sina Salary Slip ya mwezi mmoja hivi, ikabidi niende kuifatilia kesho waniingizie mpunga.

Kesho yake niko njiani kupeleka Slip, nikaingia Jamiiiforums, nakuta uzi watu wanasema Danilo Santana CEO wa D9 amekamatwa na Polisi wa Brazil... Account zake zimekua suspended...

Kubabake, nikageuza kwanza kurudi ghetto. Jamaa wa mkopo kanipigia simu kishenz "Boss mbona hauji, si ushapata Salary Slip.. Wahi nakusubiri uweke signature hapa tukuwekee pesa yako"
Nikamwambia nampeleka mama yangu Kairuki nakuja kesho boss...

Nikasema ngoja kwanza nisikilizie hatma ya D9 kwanza...
Mpaka leo bado natembea na ile Salary Slip kwenye bag langu la Ofisini na bado sijajua D9 itarudi lini.
Kubabake leo hii ningelikua nakatwa mshahara kwa mkopo ulioyeyuka hewani.
 
Hapo padri ulikuwa ulikuwa unalambika mbele ya mazabahu na waumini wanakuona yan safi sana siwezi idahau Jf since 2014 love u more sweet japo hauna kale katundu pendwaaa na madume
 
Back
Top Bottom