Malyenge
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 6,658
- 3,646
Habari za asubuhi.
Somo tajwa hapo juu lahusika.
Sisi tuliosoma nje ya nchi tukirudi Tanzania kwenye taasisi za serikali tunanyanyapaliwa sana. Suluba inaanzia hapa:
Kwanza tunaambiwa tukavithibitishe vyeti vyetu TCU. Tukifika TCU usumbufu tunaopata pale ni mkubwa sana!
Unaambiwa upeleke ushahidi kwamba ni kweli ulikwenda nje ya nchi.
Wanataka visa yako ioneshe ni student visa wakati unaondoka. Pia uoneshe sehemu ya passport ulivoondoka na ulovyofika kule yaani uoneshe sehemu iliyogongwa muhuri.
Hayo si issue sana maana mwisho unatakiwa ulipie.
Kubwa ni lile unapofanya kazi wakubwa hawakupi kipaumbele wala kuthamini elimu yako. Wanakuona ni adui na unajifanya mjuaji.
Linapokuja suala la promotion utasugua benchi mpaka utajuta kwa nini ulikwenda kusoma nje ya nchi.
Waliosoma hapa nchini utawaona wanapeta tu na maisha yao yanaenda vizuri. Vyeo wanapewa mpaka unashangaa mtu kapataje maana uwezo wa kiuongozi au kiufundi unamzidi kwa kila kitu.
Kwa kweli hali hii inatuumiza sana.
Je, ni kosa kusoma nje ya nchi?