Tuliooa kwa mahari ndogo tuje tuseme lolote juu ya jambo letu hili

Kupewa mke bila mahari au mahari Kiduchu ni Mtego mkubwa
Wakati naoa niliomba wazee waende ukweni kwa mzee Macha ili waeleze nia ya kijana wao na kupewa taratibu za mahari.

Kichwani kwangu nilikuwa nawaza hiyo list ya mahari maana mzee alikuwa jeuri na binti amemsomesha.Wazee wakaambiwa njooni mwezi ujao na huyo kijana niwatajie mahari,tulipofika mzee akaita binti yake,Mankaaaaa njoo hapa!
Mzee akamuuliza Unamjua huyu kijana?umempenda mwenyewe? Manka akajibu ndio baba.
Mzee akaniambia kijana kama mmependana nawapa baraka mkaishi vzr hayo Ndio mahari.

Sasa ni Mtego Kwasababu ukweni wakikohoa tu Nimeshafika kwa jinsi ninavyowaheshimu na kuwapenda,yani niko frontline utadhani mm mtoto wao wa kiume
umeoa manka wa kichaga
 
Walitaka laki tisa plus mazagazaga kama kofia ,koti, mtoto wa kike akataka dressing table

Nikawaambia sawa nilipogeuza hawakuniona tena na mtoto wao nilimchana hiyo hela sina labda elfu 50 ila baadaye nikaamua nimpige chini huyu atanisumbua mpka leo ananilaani eti nimemleta uchuro eti nimekuja kutoa posa bila kuoa

Nakubaliana na kulipa mahari ila sio kwa kukomoana maana hata sisi tuna thamani kwa wazazi wetu
 
Hilo halipo, sababu wenye mitazamo sawa hawaepukiki, ndiyo maana sote tunatakiwa tupambike na tabia njema. Uwakilishi haukwepeki bibie.

Unaichukuliaje siku ya Wanawake duniani na kwanini iwepo na inatija gani ?
Naichukulia kama tunavo- celebrate bithdays, Christmas, Easter.. As for "women's day",ni siku ya kucelebrate mafanikio au hatua alizopiga mwanamke.

Kusherekea kitu ni vibaya?
 
Tafuta wapo kibao, ila kaa ukijua ya kuwa ndege wafananao huruka pamoja.

Mimi kuna swahiba wangu mmoja, alioa kwa mahari ya Juzuu, nenda kaulizie bei ya juzuu madukani utaambiwa, nahisi juzu halizi Tsh 500/-.

Haya mambo sijui kwanini watu wanayatia uzito namna hii.
Kwa hili jambo naungana na waislamu mambo yanatakiwa yafanyike smoothly kama hivyo

Kuna siku mshkaji wangu alikuwa anaoa nakumbuka tulikaa stationery masaa mawili tunaandika mahitaji ya wakwe
 
Wapi Nimesema tuna tatizo mkuu?Tuko raha mustarehe Mimi na mke na wakwe zangu, acha kutuchulia
Hujaelewa nilichokiandika.

Pili, unaweza usione tatizo, lakini tatizo likawepo na unaweza usiseme lakini tatizo likawepo. Nimezungumzia yale uyatendayo kisa umetoa mahari ndogo au umepewa bure mke.
 
Unajua kuna tofauti ya kuoza na kuoana? Au hata kiswahili nacho ni kazi kwako?
Nifundishe Kiswahili kaka. Ila weka akilini hili ya kuwa kuna tamko moja lenye maana zaidi ya moja kulingana na mjengeko wa sentensi au maana. Mfano wa maneno hayo ni hilo "kuoza", kama yalivyo maneno "Kaa", "Paa", "Fua" na kadhalika.

Hakuna "kuoana" katika Kiswahili, rejea kwa Waswahili upate hukumu.
 
Naichukulia kama tunavo- celebrate bithdays, Christmas, Easter.. As for "women's day",ni siku ya kucelebrate mafanikio au hatua alizopiga mwanamke.

Kusherekea kitu ni vibaya?
Kusheherekea jmsiyo jambo ubaya ni nini unasherehekea na je ulazima wa kufanya hilo upo na je kuna natija ya kufanya hivyo ?

Ni ipi maana ya kusherehekea siku ya Wanawake duniani ? Sijaona haja hiyo na sababu ninazo.
 
Back
Top Bottom