Anataka tuachane na tayari nimekwishalipa mahari kwao na mipango ya ndoa ipo

nanix

Senior Member
Oct 26, 2015
153
166
Hello wanajamvi

Mimi ni kijana wa miaka 30, ninaishi mkoa x kikazi.. nimekuwa na mahusiano na mwanamke kwa muda wa miaka 5 tumekuwa tukiishi pamoja, mwaka jana nilikwenda kwao na kutoa mahari.

Mwezi uliopita niliomba likizo moja ya vitu tulivyotarajia kuvifanya kipindi hicho cha likizo ni pamoja na kurudi nyumbani mkoa Y kwa ajili ya kusalimia wazazi na kuweka mipango ya ndoa.
Baada ya kulifikisha swala hili kwa mpenzi wangu yeye aliniomba kuwa aende mara moja kwao mkoa Z kumsalimia bibi yake then baada kama ya siku kama 3 atarudi kuungana na mimi.

Nilimpa ushirikiano wote katika safari yake hiyo pamoja na kufanya shopping, na kumlipia nauli, na kuwa na mipango mingi ya kufanya baada ya yeye kurudi na kuungana na mimi.

Cha kushangaza baada tu ya kufika kwao tu nikaanza kunotice hata pattern ya mawasiliano yamebadilika, hanijulii hali, nikimpigia simu anadai yupo busy. Nikimuuliza atarudi lini hanipi majibu ya uhakika.

Baada ya siku kama nne akanipigia simu kuwa anataka kurudi ila atapitia mkoa T kwa rafiki yake ninayemfahamu before kuja kuungana na mimi na kuniomba nimtumie nauli nikafanya hivyo.

Siku ninayotarajia kuwa atakuwa safarini anakuja kuungana na mimi akanitumia sms kuwa anaumwa sana, baadaye akaniambia kuwa amekosa magari ya kuja huku nilipo, ukimpigia simu hapokei lakini wakati wa jioni nikampata kwenye simu katika kumuuliza kuwa anaendeleaje ana mpango gani na hiyo safari akaniambia kuwa kuna ujumbe amenitumia kwenye simu.. kucheki ule ujumbe alikuwa ameandika kuwa anaona ni wakati umefika wa kumaliza mahusiano yetu.

Hivi sasa hapa nyumbani walikuwa wanamsubiria kwa ajili ya kudiscuss naye kuhusu swala la ndoa na tayari nimekwishalipa mahari kwao.

Hapa nipo kwenye dilema sijui la kufanya nimezungumza na mama yake na yeye anashangaa anajaribu kuwasiliana naye ila hapokei simu zake.

Huyu mpenzi wangu sijawahi kuwa na ugomvi wowote mkubwa tumekuwa tukiishi vizuri tu.
 
Hello wanajamvi
Mimi ni kijana wa miaka 30, ninaishi mkoa x kikazi.. nimekuwa na mahusiano na mwanamke kwa muda wa miaka 5 tumekuwa tukiishi pamoja, mwaka jana nilikwenda kwao na kutoa mahali

Mwezi uliopita niliomba likizo moja ya vitu tulivyotarajia kuvifanya kipindi hicho cha likizo ni pamoja na kurudi nyumbani mkoa Y kwa ajili ya kusalimia wazazi na kuweka mipango ya ndoa.
Baada ya kulifikisha swala hili kwa mpenzi wangu yeye aliniomba kuwa aende mara moja kwao mkoa Z kumsalimia bibi yake then baada kama ya siku kama 3 atarudi kuungana na mimi..
Nilimpa ushirikiano wote katika safari yake hiyo pamoja na kufanya shopping, na kumlipia nauli, na kuwa na mipango mingi ya kufanya baada ya yeye kurudi na kuungana na mimi...

Cha kushangaza baada tu ya kufika kwao tu nikaanza kunotice hata pattern ya mawasiliano yamebadilika, hanijulii hali, nikimpigia simu anadai yupo busy. Nikimuuliza atarudi lini hanipi majibu ya uhakika.
Baada ya siku kama nne akanipigia simu kuwa anataka kurudi ila atapitia mkoa T kwa rafiki yake ninayemfahamu before kuja kuungana na mimi na kuniomba nimtumie nauli nikafanya hivyo...
Siku ninayotarajia kuwa atakuwa safarini anakuja kuungana na mimi akanitumia sms kuwa anaumwa sana, baadaye akaniambia kuwa amekosa magari ya kuja huku nilipo, ukimpigia simu hapokei lakini wakati wa jioni nikampata kwenye simu katika kumuuliza kuwa anaendeleaje ana mpango gani na hiyo safari akaniambia kuwa kuna ujumbe amenitumia kwenye simu.. kucheki ule ujumbe alikuwa ameandika kuwa anaona ni wakati umefika wa kumaliza mahusiano yetu...

Hivi sasa hapa nyumbani walikuwa wanamsubiria kwa ajili ya kudiscuss naye kuhusu swala la ndoa na tayari nimekwishalipa mahari kwao...


Hapa nipo kwenye dilema sijui la kufanya nimezungumza na mama yake na yeye anashangaa anajaribu kuwasiliana naye ila hapokei simu zake.

Huyu mpenzi wangu sijawahi kuwa na ugomvi wowote mkubwa tumekuwa tukiishi vizuri tu...
Hapo kuna shida labda hayuko tayari...kuna mtu zaidi yako....
 
Huenda hauko kwenye mipango yake I mean si mwanaume wa ndoto zake,alikuwa nawe kwa ajili ya kusogeza siku tu na hayo mambo ya ndoa ndio yamemvuruga kabisa...

Usiforce kijana,hiyo ndoa itakuja kukutesa vile hukutegemea

Kimbia kama umeona haramia.
 
Akikuacha kwahio utaanzisha mahusiano mentioned ambayo mutakaa miaka mitano ndio muanze ishu za ndoa technically utakuwa na miaka 35 na huyo akizingua itakuchukua tena miaka 5 means utakuwa na 40.

Huyo mwanamke ni mujinga na wewe unahitaji kujifunza mahusiano ya sasahivi hayapo stable haitakiwi uwe na uhusiano wa muda mrefu ukiwa vizuri kiuchumi ndani ya miezi mitano inatosha kuoa ukiendela hivyo utafika 50 unaandaa mipango ya ndoa tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom