Mzee Wa Kale Kabisa
JF-Expert Member
- Mar 25, 2018
- 2,602
- 4,266
Kiherehere chako tu...Kupewa mke bila mahari au mahari Kiduchu ni Mtego mkubwa
Wakati naoa niliomba wazee waende ukweni kwa mzee Macha ili waeleze nia ya kijana wao na kupewa taratibu za mahari.
Kichwani kwangu nilikuwa nawaza hiyo list ya mahari maana mzee alikuwa jeuri na binti amemsomesha. Wazee wakaambiwa njooni mwezi ujao na huyo kijana niwatajie mahari, tulipofika mzee akaita binti yake, Mankaaaaa njoo hapa! Mzee akamuuliza Unamjua huyu kijana? Umempenda mwenyewe? Manka akajibu ndio baba. Mzee akaniambia kijana kama mmependana nawapa baraka mkaishi vizuri hayo Ndio mahari.
Sasa ni Mtego Kwasababu ukweni wakikohoa tu Nimeshafika kwa jinsi ninavyowaheshimu na kuwapenda, yaani niko frontline utadhani mimi mtoto wao wa kiume.