Ukitaka watoto wasipandikizwe chuki na mama yao, fanya hivi. Kama mmebarikiwa kuwa na nyumba, wakati wa kutoa pesa ya matumizi utoe wakati mmekaa kama familia. Watoto waone helq ya mboga inatoka wapi. Wakianza shule, mpe mama yao hela ya mahitaji ya shule mbele yao (unampa mama awape). Mkeo hatakuja kupata nafasi ya kuwadanganya watoto wako hata siku moja. Tatizo la sisi wanaume tunawaamini sana wake zetu kuliko kitu kingine linapokuja suala la malezi. Una watoto wanasoma, hela ya ada unampa mkeo chumbani na mahitaji ya familia. Ndio akiwapa watoto utasikia "wanangu mnaona navyohangaika ili msome, simnaona baba yenu yeye hata hajui ada ni shingapi. Hata shule nawasindikiza mimi, someni mje mnisaidie." Tuishi nao kwa akili.