Tuliolelewa na baba zetu tukutane hapa

Tuliolelewa na baba zetu tukutane hapa

Redpanther

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2019
Posts
3,049
Reaction score
4,301
Habari gani wanajamvi wenzangu..! Natumaini siku ya ya leo Jumapili imeenda vyema. Na mapambano dhidi ya corona yanaendelea na tuukaribu kumshinda huyu adui asiyeonekana.

Hivi kwanini wazazi wetu wa kiume tumekuwa tukiwapuuza kana kwamba hawana mchango katika mafanikio yetu ??
IMG_3210.JPG

Nakumbuka tarehe 21/05/2005 Mama angu mzazi alifariki na nikabakiwa na Baba yangu. Mama alifariki mimi nikiwa darasa la saba, mimi nikiwa mtoto wa Kwanza na wadogo zangu wengine wanne tuliachwa na Baba pekee yake.

Niseme tu, Baba yangu amepambana sana kiasi kwamba katika kipindi hiki chote toka mama afariki alioa wanawake wengi sana na wote walishindwa kuishi na sisi ila Baba yangu hakuthubutu hata kunyanyua mguu wake kutuacha pekee yetu.

Wanawake hawa walishindwa kukaa na sisi ni kwa sababu Baba alikataa sisi tusiadhibiwe na mtu yoyote isipokuwa yeye kwa maana alikuwa hapendi kutuona tukiwa wanyonge au hudhuni.

Hakika Baba yangu alitupenda. Wale akina mama walikuwa wanatofautiana, wengine walionyesha nia ya kutulea vizuri wengine walikuwa wakorofi kwa sababu hatukuwa watoto wao.

Ndio maana baba alikuwa akigundua tu kuwa tunachapwa au kuadhibiwa ovyo ovuo alikuwa tayari aache kazi anayoifanya afatilie nini sababu ya adhabu na mengineyo. So wengi wa hao wanawake walishindwa.

Hatimaye tumekuwa sasa. Mdogo wangu wa mwisho yupo form five sasa hivi wengine chuoni. Na mwaka Jana Baba naye akawa ametangulia mbele za haki.[emoji24][emoji24][emoji24]

Hivyo watu wanapokuwa wanataja mama tu kana kwamba Baba zetu hawajafanya jambo si vyema. Baba zetu nao wanavipiga vita sawa sawa ili kuhakikisha mahitaji nyumbani yanakuwepo.

NAKUPENDA SANA BABA YANGU, NITAKUOMBEA KWA MUNGU. Hakika Baba yangu ni shujaa.!

Sikatai mama naye anamchango ila mimi niliye lelewa na Baba mpaka muda huu 28+ nabsikuteseka. Oooh Ahsantee Baba kwa Malezi mema, Naahidi namimi nitakuwa Baba Bora kama Wewe.

PUMZIKA KWA AMANI SHUJAA WANGU. BABA.
 
mkuu mimi sikulelewa na baba yangu peke yake,baada ya mama kufariki 97,baadae baba akaoa mke mwingine 2003,ila tunashukuru huyu mama hakuwa na matatizo.but mchango wa baba kwa miaka ile 7 tuliuona,mpaka leo yuko hai na mama mdogo huyo.

njia bora ya kumuenzo baba yako kama malipo ni wewe kusimamia uanaume wako kwa watoto wako kuzidi hata baba yako.atafurahi aliko.
 
Sawa Mkuu. Nimekuelewa kamanda..! Na hiyo ndiyo ahadi yangu kwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu jifunze kwa wanyama. Ukiangalia simba anakua na kazi ngumu ya kulinda himaya yake, kulinda kizazi chake, anapigana na madume wengine wanaotaka kuwamia himaya yake na kuharibu uzao wake karibu maisha yake yote. Ila akiishiwa nguvu mama hushirikiana na watoto kumfukuza na kumtimua akafie mbali.

Hayo ndio maisha ya wanyama karibu wote. Sasa hii haina tofauti sana na sisi binadamu ni vile tu sisi tunaweza kufikiri kwa kurudi nyuma na kwenda mbele tukawa na 'ubinadamu' ila ukweli ni kua watoto ni wa mama.

Sisi wanaume tunatumika tu kuprovide food and security lakini baadae jitihada zetu, sacrifice zote tulizofanya zinaonekana sio kitu.

Na pale itakapoonekana hatuwezi ku-provide food basi hatuhitajiki kabisa. Angalia financially independent women ambao wanaweza ku-provide food hua wanaume hatuna umuhimu tena kwao, labda atataka umzalishe tu baada ya hapo huna umuhimu tena.

Ni kweli wababa wanajitoa na kupoteza na kuhatarisha maisha yao sana ila mama ndio wanakua recognized sana.

Tuendelee kutenda wajibu wetu na kuacha bloodlines zetu, tusitegemee malipo kutoka kwa watoto.
 
Umeongea maneno mazito na mifano madhubuti kabisa..! Ama kweli mchango wangu ni mbegu za kiume na kutoa Huduma kusaidia jamii yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ways back kipindi naanza kuinuka kimaisha, always ukikaa na mama lazima ampondee mzee kwamba hana mchango kwenye life letu na ametulea alone....mindset yake ni kututeka nyara na kumuignore mzee.

Kwangu hiyo ikawa big no, ila kibabe sana bila mumuudhi mama coz nampenda mama angu. Ilikua nikienda kuwatembelea, nikitaka kusepa nahakikisha namtia mdingi kilo 2 kwa siri, namuachia maza laki kwa siri..afu kipindi naanga naangusha 50 hadharani kwamba hali yangu mbaya iwasaidie! Baasss wote hufurahi na kujiona mashujaa...rest n peace dady, nashindwa kuiga tabia zako, ulikua hujui kuchukia hata mtu akukwaze vipi, wew ni kimya tu na kupuuza!

Hongera mama you are now alone, ila sikukubali kupandikizwa chuki za wazazi, ndoa zina mambo mengi sana, na sasa najionea kwa mke wangu
 
Hongera sana kwa kutambua hilo na nimejifunza kitu hapa
Sisi mdingi alikuwa anapiga sana mtungi na mambo ya kutafuta hela nje ya kazi hakuwa nayo ila shule alitusimamia mno na kuhakikisha tunaexcel na imetusaidia wote tumemaliza chuo na kupata kazi nzuri ila wanafamilia na ndugu wengine hawalioni hilo wanakumbuka ulevi wake tu
Ways back kipindi naanza kuinuka kimaisha, always ukikaa na mama lazima ampondee mzee kwamba hana mchango kwenye life letu na ametulea alone....mindset yake ni kututeka nyara na kumuignore mzee. Kwangu hiyo ikawa big no, ila kibabe sana bila mumuudhi mama coz nampenda mama angu. Ilikua nikienda kuwatembelea, nikitaka kusepa nahakikisha namtia mdingi kilo 2 kwa siri, namuachia maza laki kwa siri..afu kipindi naanga naangusha 50 hadharani kwamba hali yangu mbaya iwasaidie! Baasss wote hufurahi na kujiona mashujaa...rest n peace dady, nashindwa kuiga tabia zako, ulikua hujui kuchukia hata mtu akukwaze vipi, wew ni kimya tu na kupuuza! Hongera mama you are now alone, ila sikukubali kupandikizwa chuki za wazazi, ndoa zina mambo mengi sana, na sasa najionea kwa mke wangu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Don't ignore mzee wako kwa hali yyte ile mkuu, hilo alilifanya ni kubwa sana...kama mama anamdiss mzee usimchane maza atajisikia vibaya, ila akili kumkichwa, ila kama ndugu tu..unaweza kuwaelimisha kwamba, aliyofanya ndio Mungu alimuwezesha, tusimhukumu bas..

Wazazi hawa wakike wanapabdikiza sumu sana kwa watoto..! Na hii ni hatari mnoo kwa ustawi wa Famili kiujumla. Ahsantee kwa mchango wako kamanda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Don't ignore mzee wako kwa hali yyte ile mkuu, hilo alilifanya ni kubwa sana...kama mama anamdiss mzee usimchane maza atajisikia vibaya, ila akili kumkichwa, ila kama ndugu tu..unaweza kuwaelimisha kwamba, aliyofanya ndio Mungu alimuwezesha, tusimhukumu bas..

Sent using Jamii Forums mobile app

Uko sahihi sana mzee.! Na sisi pia tunapaswa kuwa wa mfano kwa jamii yetu. Tutimize wajibu wetu hakika watoto wetu pia wataona nafasi yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera kwa kulelewa na baba Bora.

Nimelelewa na wazazi wote hadi ukubwani..ila mshua wangu alikuwa Bora aisee..Baba alipambana kwa ajili yetu Jamani...R.i.p
 
Hongereni! Mimi Natamani ningemuona hata baba yangu nimshike tu mkono, hongera zenu pongezi kwa baba zenu. Naamini angekuwa baba mzuri kwangu, ila alifariki nikiwa hata sijitambui.

Nawaonea wivu.
 
Back
Top Bottom