Tuliokula ada za shule sababu ya Lowassa tukutane hapa

Tuliokula ada za shule sababu ya Lowassa tukutane hapa

dah lubuva anavyozid kutoa matokeo ndo pumzi yangu inazd kukata kiukweli kama magufuli akishinda ntaenda kuishi zanzbar kama cuf wakishinda nao wakishindwa itabidi nifanye mpango wa kuomba hifadhi ya ukimbizi ujerumani

Ndugu yangu mm ntaomba hata Burundi tu
 
Kwi Kwi Kwi Kwi Kwi Kwi Kwi Kwi Kwi Kwi Kwi Kwi Kwi Kwi Kwi Kwi Kwi daah mbavu zangu jamani
 
CCM na viongozi wataendelea kutibiwa India mpaka tutakapoweka katiba yenye kuwatendea haki watanzania wote. Maji, elimu, umeme, ajira, miundombinu, kilimo, mitakataba, nk. vitaendelea kuitafuna nchi yetu kwa kuwa tunatanguliza ujinga mbele. Walitunyima katiba tukanyamaza kimywa.

Wapinzani wakapigana kufa na kupona bungeni hatukuona hilo sasa tuendelee kula mapapishi yetu hadi tutakapoona waliyoyafanya wenzetu waliotanguliza maslahi ya mataifa yao mbele na sio wachache wasio hata na uzalendo au aibu. Tunalipa garama kubwa kusomesha watoto nje. Kwa nini? Elimu yetu imekufa. Hatuna viwanda vya uhakika. Kwa nini? hatuna mahospitali na wataalamu wa kweli. Kwa nini? Kwa nini raisi atibiwe kwa Obama na siyo Mhimbili 2015? Mbona Obama haji hapa kutibiwa?

Umeme ni wa kugawana. Kwa nini wakati gasi ipo tena kwa wingi tu? Mnasema Magufuli. Je atafanya kazi peke yake? Kama ni barabara alizojenga. Tutazilinganisha na barabara zipi duniani? Nchi inategemea vichochoro vilivyojaa mashimo ambavyo vinauwa watu kila siku kwa ajali. Reli hakuna. Ni kwa ninni? Watanzania tuache ushabiki.

Deni la taifa halifai hata kuzungumzia. Hizo pesa zilifanya nini? Mnakaa mkishabikia wabunge kina Nyalandu, Nape, Nchemba. Kweli? Hatuendi popote pale mpaka tupate kwanza akili na tuache kushabikia wizi huu wa mchana kweupe. Na nyie mnaokuja kubwaja hapa mtandaoni komeni na ujinga huu.

Hii sio nchi ya vilaza kiasi hiki. Shabia kitu ambacho kina faida kwako na watoto wako. Sio unakufa kwa ushabiki huku ukiwaachia wanao na wajukuu madeni ya kulipia kwa ajili ya viongozi uchwara wa ccm na ujinga wao usio na mwisho.

Kuazia sasa mm sitokuwa miongoni mwa walalamikaji kabisa, tumepewa nafasi tumeichezea wenyewe. Inamaana tulizike na matatizo tuliyo nayo maana hawa watu tunawapenda na kuwaamini kwa ujinga wetu.

Tutaongozwa mpaka na vituku vyao.
 
Nimecheka balaa... Poleni waungwana kwa nini mnaamini maisha ya bure bure.

Halafu ada yenyewe umenywea Pombe...... Najiuliza siju Lowassa angetujengea Taifa la aina gani wananchi wanategemea kila kitu bure!
 
So sad. tujipe moyo, iko siku hii kansa itakuja toka.
 
Unajua kila nikikumbuka matusi yaliyokuwa yakiporomoshwa kwa yeyote aliyezungumza tofauti au kushauri nini kifanywe na mgombea ili kukonga nyoyo za wafuasi na mashabiki alionekana mwehu,juha,punguani,katumwa,ni gamba,CCM ni zimwi,shetwain mwenye jicho moja,kwa miaka hamsini haijafanya lolote lile,ukimwona huyo anayeongea hayo ana miaka 25 au chini ya 30,shule aliyosoma hadi kufikia hapo alipo imejengwa na hilo hilo zimwi.Tuwe wakweli yapo mambo mazuri na yapo mabaya ambayo hayatekelezwa kwa kiwango kikubwa,tusubiri mwisho wa kipyenga.

Asante kaka umesema ukweli mtupu,..
 
Mikesha hiyo ilifanyika sehemu nyingi mno na ilihusisha vijana kwenye vijiwe vyao.Walikuwa wakiandaliwa kisaikoljia tarehe hiyo 24 october ili wapige kura za hasira za kuinyima kura CCM.

Ulibandikwa jina la mkesha wa kuaga CCM ambako vijana walilewa au kuleweshwa na magodfather na magodmother wa CHADEMA au wenyewe kwa pesa zao.Wakalewa wakacheza miziki.Na nyimbo zilizokuwa zimetawala zaidi ni ule wa Sarafina wa FREEDOM IS COMING TOMMORROW na ULE WA LOWASSA WEWE

Vijana wengi walilewea hadi ada zao kwa matumaini hewa siku hiyo.Alichoandika mleta mada si kitu cha kubuni wala nini ni kitu real.Mikesha hiyo ilikuwepo.

Ukweli mtupu kaka,..Ubarikiwe!
 
Eti Yericko Nyerere katoka kwenye Instagram anasema anayo matokeo yote hivyo watu wa UKAWA wasiwe na wasi wasi atamaliza mchezo !
Yaani Lowassa anamtegemea Yericko amtangazie ushindi

Labda matokeo ya instagram na Facebook,..
 
Last edited by a moderator:
Hahaaaa pole siasa mchezo mchafu ww tafuta maisha
usimtafutie mtu
 
Ukasahau hili....! "Ndimi bwana Mungu wako, usiabudu miungu mingine". Nawe ukamtumainia Lowassa badala ya Mungu wako hadi ukala ada ya shule....!
 
Back
Top Bottom