Tuliokula ada za shule sababu ya Lowassa tukutane hapa

Tuliokula ada za shule sababu ya Lowassa tukutane hapa

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2015
Posts
1,533
Reaction score
3,838
Wadau,

Mimi na mdogo wangu tulikula ada siku ya tarehe 24 kwenye mkesha wa kuiaga CCM. Mimi ni mwanafunzi nasoma masters na mdogo wangu anaingia mwaka wa pili undergraduate.

Tulikula ada kwa kuamini kuwa Lowassa atashinda lakini upepo ni mbaya mno, unapuliza kwa kasi kubwa. Hapa mimi na mdogo wangu tumeishiwa nguvu, tangu jana mdogo hana nguvu za kula.

Kama kuna wengine walikula ada tukutane hapa kupeana faraja.
 
teh teh teh teh,poleni wadogo zangu hayo matumaini mliyokuwa mkipewa sawa na kufukuza upepo. Msiwe na wasiwasi magufuli atatoa mikopo haraka mtaendelea na masomo yenu.
 
dah lubuva anavyozid kutoa matokeo ndo pumzi yangu inazd kukata kiukweli kama magufuli akishinda ntaenda kuishi zanzbar kama cuf wakishinda nao wakishindwa itabidi nifanye mpango wa kuomba hifadhi ya ukimbizi ujerumani
 
MKesha wa kuiaga CCM ulifanyika wapi?

Mikesha hiyo ilifanyika sehemu nyingi mno na ilihusisha vijana kwenye vijiwe vyao.Walikuwa wakiandaliwa kisaikoljia tarehe hiyo 24 october ili wapige kura za hasira za kuinyima kura CCM.

Ulibandikwa jina la mkesha wa kuaga CCM ambako vijana walilewa au kuleweshwa na magodfather na magodmother wa CHADEMA au wenyewe kwa pesa zao.Wakalewa wakacheza miziki.Na nyimbo zilizokuwa zimetawala zaidi ni ule wa Sarafina wa FREEDOM IS COMING TOMMORROW na ULE WA LOWASSA WEWE

Vijana wengi walilewea hadi ada zao kwa matumaini hewa siku hiyo.Alichoandika mleta mada si kitu cha kubuni wala nini ni kitu real.Mikesha hiyo ilikuwepo.
 
Hahahahahaaaa jamani mbavu zangu mnanifurahisha sana.mgufuli 4 change
 
Unajua kila nikikumbuka matusi yaliyokuwa yakiporomoshwa kwa yeyote aliyezungumza tofauti au kushauri nini kifanywe na mgombea ili kukonga nyoyo za wafuasi na mashabiki alionekana mwehu,juha,punguani,katumwa,ni gamba,CCM ni zimwi,shetwain mwenye jicho moja,kwa miaka hamsini haijafanya lolote lile,ukimwona huyo anayeongea hayo ana miaka 25 au chini ya 30,shule aliyosoma hadi kufikia hapo alipo imejengwa na hilo hilo zimwi.Tuwe wakweli yapo mambo mazuri na yapo mabaya ambayo hayatekelezwa kwa kiwango kikubwa,tusubiri mwisho wa kipyenga.
 
dah lubuva anavyozid kutoa matokeo ndo pumzi yangu inazd kukata kiukweli kama magufuli akishinda ntaenda kuishi zanzbar kama cuf wakishinda nao wakishindwa itabidi nifanye mpango wa kuomba hifadhi ya ukimbizi ujerumani

Unawaza kama mimi walah
 
dah lubuva anavyozid kutoa matokeo ndo pumzi yangu inazd kukata kiukweli kama magufuli akishinda ntaenda kuishi zanzbar kama cuf wakishinda nao wakishindwa itabidi nifanye mpango wa kuomba hifadhi ya ukimbizi ujerumani

Zanzibar kule Maalim Seif kashaharibu hapati hata serikali ya umoja wa kitaifa !
 
Poleni sana,, nilikuwa sitaki kuamini lakini nimeamini kwa sababu jana kuna taasisi fulani ya elimu tunaidai kama ofisi, lakini nilichoambiwa na Bursal ni kwamba wanachuo bado hawajaanza kulipa ada wakati siyo kawaida yao, wanasubiri elimu bure ya EL
kwa mantiki hiyo sasa naamini kuwa huenda ni kweli mmekula ada
 
CCM na viongozi wataendelea kutibiwa India mpaka tutakapoweka katiba yenye kuwatendea haki watanzania wote. Maji, elimu, umeme, ajira, miundombinu, kilimo, mitakataba, nk. vitaendelea kuitafuna nchi yetu kwa kuwa tunatanguliza ujinga mbele. Walitunyima katiba tukanyamaza kimywa.

Wapinzani wakapigana kufa na kupona bungeni hatukuona hilo sasa tuendelee kula mapapishi yetu hadi tutakapoona waliyoyafanya wenzetu waliotanguliza maslahi ya mataifa yao mbele na sio wachache wasio hata na uzalendo au aibu. Tunalipa garama kubwa kusomesha watoto nje. Kwa nini? Elimu yetu imekufa. Hatuna viwanda vya uhakika. Kwa nini? hatuna mahospitali na wataalamu wa kweli. Kwa nini? Kwa nini raisi atibiwe kwa Obama na siyo Mhimbili 2015? Mbona Obama haji hapa kutibiwa?

Umeme ni wa kugawana. Kwa nini wakati gasi ipo tena kwa wingi tu? Mnasema Magufuli. Je atafanya kazi peke yake? Kama ni barabara alizojenga. Tutazilinganisha na barabara zipi duniani? Nchi inategemea vichochoro vilivyojaa mashimo ambavyo vinauwa watu kila siku kwa ajali. Reli hakuna. Ni kwa ninni? Watanzania tuache ushabiki.

Deni la taifa halifai hata kuzungumzia. Hizo pesa zilifanya nini? Mnakaa mkishabikia wabunge kina Nyalandu, Nape, Nchemba. Kweli? Hatuendi popote pale mpaka tupate kwanza akili na tuache kushabikia wizi huu wa mchana kweupe. Na nyie mnaokuja kubwaja hapa mtandaoni komeni na ujinga huu.

Hii sio nchi ya vilaza kiasi hiki. Shabia kitu ambacho kina faida kwako na watoto wako. Sio unakufa kwa ushabiki huku ukiwaachia wanao na wajukuu madeni ya kulipia kwa ajili ya viongozi uchwara wa ccm na ujinga wao usio na mwisho.
 
Back
Top Bottom