Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Mimi nililima hekari 40 za mpunga Ifakara (signal). Nilitumia milioni kumi lakini nilikuja kuvuna gunia 14 tu. Na hizo gunia 14 ndiyo pesa ya vibarua; mfano kukata, kukusanya, kupiga kupepeta, kununua viroba. Kwa ufupi ziliishia humo tu. Niliambulia kupata gunia moja la mpunga nikakoboa nikapata mchele kilo 70. Kesho yake nikapanda basi kurudi Dar Nikawaletea chakula tu kilichopatikana. Nipo Ilala nawaza bora ningefungua duka la spea, ILA YA MUNGU MENGI.
ZINGINALI wenyewe wanapaita.
 
Mimi nililima mpunga heka kumi ukakubali kweli kweli shamba lilikua langu bwana bwana kukaa hivi napigiwa simu wasukuma wameingiza ng'ombe usiku wamekula shamba lote aisee nilidata. Alafu washenzi wale wamehonga polisi ukienda kushtaki unapigwa danadana tu nilitamani nikapige risasi ng'ombe wote. Morogoro iyo
 
Duh aisee pole sana hayo maumivu yake kama nayaona vile.
 
Kuongea ni rahis sana ingia field uone utamu wake. Unakodi eneo unaweka matikit then unakod gari unaanza kusambaza una mzigo fuso limejaa ukifika kwa wanunuzi mtaani anakwambia nachukua matikit 15, anaenda kwa mwingine anachukua 6, mwingine anataka mkopo. Kadri siku zinavyoenda yapoteza ubora wakati huko na we gharama zinazidi za kukaa Dodoma pamoja na za kusambaza mzigo
Faida yote itaishia kulipa hilo Fuso, maana utakua unazunguka nalo kutwa.
 
Usilime kwa ushawishi fanya research ya soko kwanza. Kuna dada ninamfahamu wateja wake ni foreigners. Analima carrots, cabbage, hoho, nyanya vitunguu. Kila siku anapeleka mzigo kwa nyumbani kwa wateja. Ana list yao kabisa akifunga jumu shillings 10,000. Hakosi 200,000-250,000 kwa siku.
Hiki ndo kilimo cha online, kinashawishi kinoma.
 
Mi niliingia ktk kilimo kwa partnership na ndugu zng wa huko bush ili km ikibuma basi maumivu yawe ½!

Msimu wa kwanza tulilima cabbage kwa kumwagilia! Niliwatumia ndugu zangu wa huko shamba kama nguvu kazi! Mimi nikatoa fund kwa ajili ya pembejeo!Cabbage ikatupiga hatari! Ilipigwa na ugonjwa, ikazaa chini ya Makadirio! Kidogo iliyopatikana tuliuza pale pale Kijijini!

Changamoto!
1. Mtu tuliemuamini km mtaalamu wa cabbage hakua na utaalamu husika na hivo alitupeleka chaka ktk maeneo km mbolea na sumu za wadudu waharibifu!

2. Tulilima kwa kutumia maji ya mto, kutokana na wingi wa wakulima, maji haya yalikuwa na zamu lini na lini wamwagilie akina nani. Ilifika wakati ikifika zamu yk let's say Juma5, mto hauna Maji!

Suluhisho!
Tumechimba kisima shambani. Pump tunayo!

Msimu huu tumelima MAHINDI Gobo gobo! Kila kitu kimeenda sawa! Yamezaa vizuri sana!

Hofu:
Tuna hofu na bei ya sokoni ya MAHINDI ya kuchoma!

Plan B:
Km MAHINDI ya Gobo gobo hayatakuwa na bei nzuri, tutayaacha yakauke ili tuvune MAHINDI ya Ugali! Kwa sasa sokoni bei ya ipo vizuri. Kijijini kwa sasa debe ni 20k!
 
Safi mkuu hapo ujipange namna ya kuhifadhi gobo isishambuliwe na wadudu au kuoza shambani ktk kipindi cha mvua unaposubiri ikauke
 
Kunaitwa NDUNGU mkuu unaingilia hapa mombo nimefika kote kule hadi gonja ila nimeuliza nimeambiwa ule mchele sio mtam kama wa kyela na ifakara ni mbegu za Kijapan.
We lima uza mbona watu wanatoboa tu huko Same.
 
Naanza kwa kutoa experience yangu.

Niliingia kwenye kilimo baada ya kushawishika na vipindi vya Clouds Media kuhusiana na fursa. Presenters walishawishi sana kuwa vijana hatujitumi na hatutumii brain zetu vizuri.

Nikajitosa kwenye kilimo cha tikiti Migoli Iringa na milioni zangu 2. Nikaingia front mwenyewe sikutaka kilimo cha simu. Nilikutana na changamoto katika kulima nikapambana nazo nilikuwa nalala shamba kwenye vibanda vya nyasi, vibarua wanazingua balaa na changamoto ya madawa. Baadae nikafanikiwa kuvuna na yalikubali sana.

Mziki ukaja kwenye soko sasa. Unatoka mjini na mfanyabiashara kuja shamba kununua mzigo, mjini umeacha bei ya tikiti 1 ni elfu 4. Mfanyabiashara shamba anataka kununua tikiti 1 sh 500, nikaamua kwenda nayo mwenyewe sokoni Dodoma. Kufika pale, dah! washaambizana wafanyabiashara wao hawanunui direct kutoka kwa mkulima; wananunua kupitia madalali, ikanibidi niwakabidhi madalali mzigo. Hapo nilichoka nilirudi nyumbani na laki 4.

Nikaingia kwenye kilimo cha vitunguu Ruaha Mbuyuni. Nikapambana nacho; jani lilikubali balaa kila siku nikawa napiga picha narusha social media. Wakati wa kuvuna kuja kuchimba chini chenga tu nikaishia kuuza reja reja nikatoka na laki 7.

Nikaja kulima mahindi ya kuchoma maarufu kama Gobo. Nilipambana nayo mpaka mwisho kwenye soko tena changamoto. Mfanyabiashara anakuja kuchagua mahindi shamba anataka kununua muhindi mmoja kwa sh 120 ilihali mjini muhindi mmoja sh 500, nikaghairi kuuza nikasubiri yakauke bahati nzuri bei ya mahindi nzuri.

My take: Katika kilimo madalali na wafanyabiashara ndiyo wanaonufaika sana kuliko wakulima.
Mimi nilishapigwa na kilimo kwasasa sina ham nacho kabisa,ninachokifanya nachukua mazao kwa mkulima then nayaweka store bei ikipanda nauza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom