Tulijadili hili ....

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,025
6,555
Unamkuta Baba na Mama wanabebana na watoto kutoka nyumbani kwao wanasafiri eti wanaeda nyumbani walikozaliwa kula sikukuu. Binafsi siliungi mkono hata kidogo. Mtu ukishakuwa na familia - basi inakubidi usherehekee sikukuu na familia yako na ikibidi nawe ukawaalike ndugu zako (wapwa na wajomba).
Wanaopaswa kusafiri kwenda majumbani kwa wazazi wao kula sikukuu ni wale ambao hawajawa na familia na zaidi watoto wa shule.
Sasa we baba / mama unaacha mji wako na kusafiri umbali mkubwa; ukikuta hapo kwako kumeharibiwa na vibaka kwa kushirikiana na watu ulowaacha hapo kwako eti wakulindie nyumba / mji wako mtamlaumu nani?
 
Umeona eee?
Bora wangewasafirisha madogo peke yao kwenda kwa bib&babu kula sikukuku lakini mke na mume wenye mi.vuzi
big NO.
 
mazoea yana tabu.

eti mkuu fikiria kama babu yako yupo; wewe ukifunga safari kwenda kwa baba yako hautamkuta kwa kuwa naye atakuwa ameenda kwa baba yake ambaye ni babu yako. Mlolongo huu ukifuatiliwa hauna maana yoyote. Ni kuwafaidisha watu wenye vyombo vya usafiri pasipo sababu yoyote.
 
Wewe badala ya kuwakaribisha waje kwako unaenda kuwapa shida huko uendako! Jiulize utawakaribisha lini?
 
Wewe badala ya kuwakaribisha waje kwako unaenda kuwapa shida huko uendako! Jiulize utawakaribisha lini?

Inategemea. Nauli unayo? Unakokwenda kuna sehemu ya kulala? Nyie ndo mnakaa na watoto hata hawawajui ndugu zao wala asili yao. Alafu pia yafurahisha. It's like wazungu wanakuja kutalii Africa wewe utasema wanapoteza hela. It's an adventure. Utakaa mahali pamoja na beach za Dar tu? Be adventurous!
 
Hao utakaowaalika,kwanini waje?Kama wewe unaona si vyema kwenda kwa watu nao hawatakiwi waje kwako!
 
eti mkuu fikiria kama babu yako yupo; wewe ukifunga safari kwenda kwa baba yako hautamkuta kwa kuwa naye atakuwa ameenda kwa baba yake ambaye ni babu yako. Mlolongo huu ukifuatiliwa hauna maana yoyote. Ni kuwafaidisha watu wenye vyombo vya usafiri pasipo sababu yoyote.

Hata mseme nini/ kwetu tutakwenda tu, haiwezekani tukae mwaka mzima tusiende kusalimu wazazi na bibi zetu home, ndiyo matokeo yake watoto wanakuwa hawajui kwao kwa sababu ya kung'ng'ania mjini. HOME IS BEST>

TENA NGOJA NIKWAMBIE NI KWA NN SISI WA MOSHI TUNAPENDA KWENDA. Mf, unandugu yako anaishi mbeya, mwingine mwanza, mwingine sumbawanga na hamjaonana mwaka mzima basi pale ndipo pa kwenda kuonana na kuongelea mambo ya maendeleo, na kama umepata tatizo pale ndipo yanatatuliwa wewe pamoja na ndugu zako na wazazi.

wewe kaa huku mjini udhani wanaokwenda kwao ni wajinga!!!!
 
Haa!!!!! lazima niende kwetu 24th Dec. narudi 30th Dec

watoto mnaruhusiwa kwenda kwa baba zenu kula sikukuu. mimi baba kubebana na mke wangu na wanangu eti naenda kwa baba kula sikukuu si ata watoto wangu wananishangaa. utaratibu wangu ni kwamba watoto wakifunga shule wanaenda kusalimia kwa babu / ujombani n.k; sikukuu zikikaribia wote lazima warudi.
 
hata mseme nini/ kwetu tutakwenda tu, haiwezekani tukae mwaka mzima tusiende kusalimu wazazi na bibi zetu home, ndiyo matokeo yake watoto wanakuwa hawajui kwao kwa sababu ya kung'ng'ania mjini. Home is best>

tena ngoja nikwambie ni kwa nn sisi wa moshi tunapenda kwenda. Mf, unandugu yako anaishi mbeya, mwingine mwanza, mwingine sumbawanga na hamjaonana mwaka mzima basi pale ndipo pa kwenda kuonana na kuongelea mambo ya maendeleo, na kama umepata tatizo pale ndipo yanatatuliwa wewe pamoja na ndugu zako na wazazi.

Wewe kaa huku mjini udhani wanaokwenda kwao ni wajinga!!!!

kawaida mjadala wowote usipokuwa na opposition side hauendi vyema! Nimekusoma
 
Hao utakaowaalika,kwanini waje?Kama wewe unaona si vyema kwenda kwa watu nao hawatakiwi waje kwako!

Haujakatazwa kwenda kwa watu; tunaangalia umuhimu wa kwenda kwenu / kwa baba yako siku za sikukuu wakati na wewe una mji na watoto; na kibaya zaidi kubeba familia nzima eti "tunaenda kula sikukuu"
 
wee amu weeeee ngoja uolewe utaona.

binafsi huwa naamini katika kuwatembelea wazazi hasa msimu wa sikukuu ili wafurahi, muongee na ndugu zako kwa kina na kisha kuombeana. Ikumbukwe kwamba watoto ndio wanaopaswa kufwata wazazi na si wazazi wafwate watoto.

ni lazima kwangu x-mass na mwaka mpya nile ukweni kwangu ( hapa nnajiandaa tarehe 23 saa 11 alfajiri ngoma inanyuka iringaa)

ni lazima sikuu ya pasaka nile kwetu hivyo alhamis kuu ngoma hunyanyukaa kwetuuuuu nikiwa na kids na baba yao. hiyo ni lazima.

kuna miaka ambayo hupenda kuwaalika watu kwangu, nakumbuka kuna mwaka niliwaita wakwe zangu kula x-mass na new yr kwangu. na hapa niliita mawifi shem na baba na mama pamoja na wajukuu. duh ilikuwa bonge la raha ya ajabu manake utafikiri kuna sherehe lol! inapendeza sana kuona mtu anatoka kwake kuja kwako kukusalimia na familia yake mnakaa pamoja kwa wiki 2 hivi ni kula na kunywa tu. sitokaa nisahau. ilikuwa raha sana sana.

pia kuna pasaka niliwaalika baba na mama yangu kwangu but i was realy disappointed as wazazi wa kichaga huwa hawalali kwa mtoto wa kike hata ardhi ipasuke. sikupenda manake waliniambia tena kwa amri "SISI NI WAZAZI HATUTOKI KWETU KULA SIKUKUU KWA MTOTO BALI MTOTO NDO ATUFWATE SISI " ila nilipouliza kisa nn hasa manake mbona kwa kaka wanaendaga?? nikajibiwa yule ni mtoto wa kiume ila kwako wewe sio kwetu huko ni ukweni hatupaswi kupazoea. ..........arrrrgggggggggghhhhhhhhhh yaani nilimjibu tu hubby twende manake ishakuwa tabu.
 
Last edited by a moderator:
Haujakatazwa kwenda kwa watu; tunaangalia umuhimu wa kwenda kwenu / kwa baba yako siku za sikukuu wakati na wewe una mji na watoto; na kibaya zaidi kubeba familia nzima eti "tunaenda kula sikukuu"

siyo opposition side , la ila ninakwambia kitu ambacho ni kizuri ni kwenu bwana, na ni vizuri wakat wa sikukuu maana wengi wanakuwa likizo ndiyo maana wanapenda kwenda wakati huo.
 
Inategemea. Nauli unayo? Unakokwenda kuna sehemu ya kulala? Nyie ndo mnakaa na watoto hata hawawajui ndugu zao wala asili yao. Alafu pia yafurahisha. It's like wazungu wanakuja kutalii Africa wewe utasema wanapoteza hela. It's an adventure. Utakaa mahali pamoja na beach za Dar tu? Be adventurous!

Naona hujanielewa! kwani kama wewe ni mzaliwa wa Bukoba; ukiamua kutembea Arusha au Dar nani anakukataza! Issue ni kubebana msimu wa sikukuu kwenda huko Kiziba / Buyango eti kula sikukuu. Ina maana siku zingine huwa unazuiliwa na nani kupeleka watoto wakapaone kwao.
 
Unamkuta Baba na Mama wanabebana na watoto kutoka nyumbani kwao wanasafiri eti wanaeda nyumbani walikozaliwa kula sikukuu. Binafsi siliungi mkono hata kidogo. Mtu ukishakuwa na familia - basi inakubidi usherehekee sikukuu na familia yako na ikibidi nawe ukawaalike ndugu zako (wapwa na wajomba).
Wanaopaswa kusafiri kwenda majumbani kwa wazazi wao kula sikukuu ni wale ambao hawajawa na familia na zaidi watoto wa shule.
Sasa we baba / mama unaacha mji wako na kusafiri umbali mkubwa; ukikuta hapo kwako kumeharibiwa na vibaka kwa kushirikiana na watu ulowaacha hapo kwako eti wakulindie nyumba / mji wako mtamlaumu nani?

Hayatuhusu. Sasa umeandika kitu gani hapa?? Hizi mada zenye kiwango cha chini pelekeni sehemu nyingine, sio humu JF. Kama huna hoja ya msingi, tulia kimya. Soma michango ya wengine, sio lazima uandike kila kitu.

Similar Discussions

Back
Top Bottom