Tulijadili hili ....

kiukweli kabisa nimekukaribisha wewe na wala si familia yako. Nyumba yangu kule mlimani inanitosha mimi na familia yangu (ambayo imeshatangulia) na mgeni mmoja tu.

Nakaa mbali na mlimani na familia yangu kwa zaidi ya miezi 11 kwa mwaka, kukaa nayo kwenye nyumba yangu mlimani kwa wiki mbili kwangu ni furaha isiyosemekana

tutajulishana vituo kwa pm! Thanx a lot my friend.
 
Siungi mkono wazo lako, wengine wetu tunaishi kama extended family, na wanafamilia wengi wapo ulipozaliwa so cyo mbaya once in a year ukaenda kuwaona maana ukitaka wao waje kukusalimia kwa jinsi walivyo wengi hata fastjet haitawatosha
 
yaani ktk kitu ambacho ningeweza kukibadili hiki ni namba moja. hivi Lisa unafikiri wanangu mm hawana hamu ya kumwona bibi ama babu yao hapa nyumbani kwao?? kwann walazimike tu kwenda kwao?? mm natamani siku itokee baba yangu aje alale hapa kwangu acheze na wajukuu nitoke job nimkute tupige story jamani mbona wanatunyanyasa sana na huuuu ukwe??

Hahaha..hakunaga aisee!!!! yani ndugu wa mumeo wakimkuta wanaruhusiwa kumpiga,lol!
 
Hujakatazwa kwenda home; swali langu ni je lazima iwe siku ya sikukuu????

Siku ya sikukuu hasa krismasi ndo mwisho wa mwaka mkuu na ofc nyingi za binafsi zinafungwa so inakuwa ni muda mzuri kuchoropoka kwenda kuwaona ndugu na jamaa kwa wingi wao
 
wee amu weeeee ngoja uolewe utaona.

binafsi huwa naamini katika kuwatembelea wazazi hasa msimu wa sikukuu ili wafurahi, muongee na ndugu zako kwa kina na kisha kuombeana. Ikumbukwe kwamba watoto ndio wanaopaswa kufwata wazazi na si wazazi wafwate watoto.

ni lazima kwangu x-mass na mwaka mpya nile ukweni kwangu ( hapa nnajiandaa tarehe 23 saa 11 alfajiri ngoma inanyuka iringaa)

ni lazima sikuu ya pasaka nile kwetu hivyo alhamis kuu ngoma hunyanyukaa kwetuuuuu nikiwa na kids na baba yao. hiyo ni lazima.

kuna miaka ambayo hupenda kuwaalika watu kwangu, nakumbuka kuna mwaka niliwaita wakwe zangu kula x-mass na new yr kwangu. na hapa niliita mawifi shem na baba na mama pamoja na wajukuu. duh ilikuwa bonge la raha ya ajabu manake utafikiri kuna sherehe lol! inapendeza sana kuona mtu anatoka kwake kuja kwako kukusalimia na familia yake mnakaa pamoja kwa wiki 2 hivi ni kula na kunywa tu. sitokaa nisahau. ilikuwa raha sana sana.

pia kuna pasaka niliwaalika baba na mama yangu kwangu but i was realy disappointed as wazazi wa kichaga huwa hawalali kwa mtoto wa kike hata ardhi ipasuke. sikupenda manake waliniambia tena kwa amri "SISI NI WAZAZI HATUTOKI KWETU KULA SIKUKUU KWA MTOTO BALI MTOTO NDO ATUFWATE SISI " ila nilipouliza kisa nn hasa manake mbona kwa kaka wanaendaga?? nikajibiwa yule ni mtoto wa kiume ila kwako wewe sio kwetu huko ni ukweni hatupaswi kupazoea. ..........arrrrgggggggggghhhhhhhhhh yaani nilimjibu tu hubby twende manake ishakuwa tabu.
sisi kwa kumaliza ubishi tumepangiana zamu.
mwaka huu wote tunaenda kwa wazazi (mama ndo kabaki), mwakani kwangu first born, mwaka unaofuata kwa mdogo wangu 2nd born, mwaka mwingine kila mtu kwake, kama mnaenda ukweni poa.
Ila mimi nina bahati wakwe zangu ni waislam, huwa tunaenda kwao sikukuu za Idd, kwa hiyo mwaka wa kukaa kwenu huwa tunatalii na watoto wetu.
 
Hata mseme nini/ kwetu tutakwenda tu, haiwezekani tukae mwaka mzima tusiende kusalimu wazazi na bibi zetu home, ndiyo matokeo yake watoto wanakuwa hawajui kwao kwa sababu ya kung'ng'ania mjini. HOME IS BEST>

TENA NGOJA NIKWAMBIE NI KWA NN SISI WA MOSHI TUNAPENDA KWENDA. Mf, unandugu yako anaishi mbeya, mwingine mwanza, mwingine sumbawanga na hamjaonana mwaka mzima basi pale ndipo pa kwenda kuonana na kuongelea mambo ya maendeleo, na kama umepata tatizo pale ndipo yanatatuliwa wewe pamoja na ndugu zako na wazazi.

wewe kaa huku mjini udhani wanaokwenda kwao ni wajinga!!!!
nadhani point ya jamaa umeiona tu sema unakomaa sababu ya ubishi haya nenda huko halafu urudi ukute umeibiwa kila kitu sijui utaomba au kusubiri mwisho wa mwaka uombe uchangiwe....hivyo ulivyo poteza...
 
nadhani point ya jamaa umeiona tu sema unakomaa sababu ya ubishi haya nenda huko halafu urudi ukute umeibiwa kila kitu sijui utaomba au kusubiri mwisho wa mwaka uombe uchangiwe....hivyo ulivyo poteza...

Hasara Roho , Vitu , Pesa ni makaratasi tutapata vingine, la muhimu ni roho na afya njema ndicho kitu cha muhimu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom