Tulijadili hili ....

wee amu weeeee ngoja uolewe utaona.

binafsi huwa naamini katika kuwatembelea wazazi hasa msimu wa sikukuu ili wafurahi, muongee na ndugu zako kwa kina na kisha kuombeana. Ikumbukwe kwamba watoto ndio wanaopaswa kufwata wazazi na si wazazi wafwate watoto.

ni lazima kwangu x-mass na mwaka mpya nile ukweni kwangu ( hapa nnajiandaa tarehe 23 saa 11 alfajiri ngoma inanyuka iringaa)

ni lazima sikuu ya pasaka nile kwetu hivyo alhamis kuu ngoma hunyanyukaa kwetuuuuu nikiwa na kids na baba yao. hiyo ni lazima.

kuna miaka ambayo hupenda kuwaalika watu kwangu, nakumbuka kuna mwaka niliwaita wakwe zangu kula x-mass na new yr kwangu. na hapa niliita mawifi shem na baba na mama pamoja na wajukuu. duh ilikuwa bonge la raha ya ajabu manake utafikiri kuna sherehe lol! inapendeza sana kuona mtu anatoka kwake kuja kwako kukusalimia na familia yake mnakaa pamoja kwa wiki 2 hivi ni kula na kunywa tu. sitokaa nisahau. ilikuwa raha sana sana.

pia kuna pasaka niliwaalika baba na mama yangu kwangu but i was realy disappointed as wazazi wa kichaga huwa hawalali kwa mtoto wa kike hata ardhi ipasuke. sikupenda manake waliniambia tena kwa amri "SISI NI WAZAZI HATUTOKI KWETU KULA SIKUKUU KWA MTOTO BALI MTOTO NDO ATUFWATE SISI " ila nilipouliza kisa nn hasa manake mbona kwa kaka wanaendaga?? nikajibiwa yule ni mtoto wa kiume ila kwako wewe sio kwetu huko ni ukweni hatupaswi kupazoea. ..........arrrrgggggggggghhhhhhhhhh yaani nilimjibu tu hubby twende manake ishakuwa tabu.

Exactly! HAIWEZEKANI BABA NA MAMA WA KICHAGA AKAJA KULA NA KULALA UKWENI, HATA SI HAO TU HATA WAKURYA MA WAKEREWE HAWALALI UKWENI.NI MARUFUKU .
 
siyo opposition side , la ila ninakwambia kitu ambacho ni kizuri ni kwenu bwana, na ni vizuri wakat wa sikukuu maana wengi wanakuwa likizo ndiyo maana wanapenda kwenda wakati huo.

Hayo yataisha muda si mwingi; kuna wengine ni wajasiliamali katika secta binafsi, siku za sikukuu ndo siku za kufanya kazi; kwa waajiliwa wa serikalini sawa naweza nikawakubalia lakini ..... sio sana!

Tunapenda maisha ya kukariri, hatutaki kubadilika, hatujiulizi ni kwa nini tunafanya mambo fulani ambayo yalifanyika miaka ya zamani hadi sasa yanaendelea.
 
Haujakatazwa kwenda kwa watu; tunaangalia umuhimu wa kwenda kwenu / kwa baba yako siku za sikukuu wakati na wewe una mji na watoto; na kibaya zaidi kubeba familia nzima eti "tunaenda kula sikukuu"

kwa desturi yetu msimu wa sikukuu ndio ambao wengi wetu huwa likizo na hivyo muda huu mara nyingi tunautumia kusalimia wazazi na ndugu wengine pia ndio muda ambao tunautumia kuhani misiba ambayo baada ya kuzika hujawa kurudi kutoa pole.

ni ngumu sana kuwaita ndugu zako wajomba aunts baba mama kuja kwako kwani mahali pa kuwaweka ni tabu ila unapokwenda kwenu ndio unapata muda wa kusalimia ndugu wote, aunts, uncle's, brodas, sistas etc. mbaya zaid watu hawa utaenda kuwasalimia nyumban kwao tu wala hutatakiwa kuwaleta waje walale kwako na mara nyingi huwa ni safari ya muda mdogo sana like kama mm naweza kusalimia kijiji kizima kwa siku moja tu.

istoshe unapokuwa kwenu kuna ndugu zako ambao watapenda kuja kukusalimia watakaposikia kwamba umeenda so kwako ni muda wa kuimarisha undugu na ushirikiano na wale wa karibu yako.

unaweza ukamwalika mtu kuja kwako but mara nyingi sana lazima iwe si muda wa sikukuu unless kuwe na event maalum like harus ama msiba.
 
Exactly! HAIWEZEKANI BABA NA MAMA WA KICHAGA AKAJA KULA NA KULALA UKWENI, HATA SI HAO TU HATA WAKURYA MA WAKEREWE HAWALALI UKWENI.NI MARUFUKU .

yaani ktk kitu ambacho ningeweza kukibadili hiki ni namba moja. hivi Lisa unafikiri wanangu mm hawana hamu ya kumwona bibi ama babu yao hapa nyumbani kwao?? kwann walazimike tu kwenda kwao?? mm natamani siku itokee baba yangu aje alale hapa kwangu acheze na wajukuu nitoke job nimkute tupige story jamani mbona wanatunyanyasa sana na huuuu ukwe??
 
Last edited by a moderator:
Hayatuhusu. Sasa umeandika kitu gani hapa?? Hizi mada zenye kiwango cha chini pelekeni sehemu nyingine, sio humu JF. Kama huna hoja ya msingi, tulia kimya. Soma michango ya wengine, sio lazima uandike kila kitu.

Semea nafsi yako kwamba hayakuhusu. Hayawahusu wewe na nani? Kama hayawahusu mbona mnachangia? Kidogo kwako ni kikubwa kwangu. Kama unaona una uelewa mkubwa sana zaidi ya wenzako; pita uende zako!
 
yaani ungejua jinsi ambavyo unaboa wengine ungejiheshimu. yaani wewe halafu unajiona mjanjaaaaaaaaa kweli kweli kama mjanja njoo na ID yako tuliyoizoea
 
yaani ktk kitu ambacho ningeweza kukibadili hiki ni namba moja. hivi Lisa unafikiri wanangu mm hawana hamu ya kumwona bibi ama babu yao hapa nyumbani kwao?? kwann walazimike tu kwenda kwao?? mm natamani siku itokee baba yangu aje alale hapa kwangu acheze na wajukuu nitoke job nimkute tupige story jamani mbona wanatunyanyasa sana na huuuu ukwe??
Una mtazamo mzuri sana! Mnanyanyasika kijinsia them mnadanganyika eti kuna usawa!
 
exactly! haiwezekani baba na mama wa kichaga akaja kula na kulala ukweni, hata si hao tu hata wakurya ma wakerewe hawalali ukweni.ni marufuku .

toa sababu za msingi - usiseme haiwezekani, akilala ukweni anachubuka ubavu???
 
Last edited by a moderator:
yaani ungejua jinsi ambavyo unaboa wengine ungejiheshimu. yaani wewe halafu unajiona mjanjaaaaaaaaa kweli kweli kama mjanja njoo na ID yako tuliyoizoea

Hachana naye huyu ana mtindio wa akili.
 
yaani ungejua jinsi ambavyo unaboa wengine ungejiheshimu. yaani wewe halafu unajiona mjanjaaaaaaaaa kweli kweli kama mjanja njoo na ID yako tuliyoizoea

Sasa wewe unaona hii mada inafaa kujadiliwa hapa JF kweli? embu soma mada za JF ya mwaka 2006 na 2007 uone!! Halafu linganisha na mada zinazoletwa hapa 2012!! Utanielewa vizuri.
 
Wewe badala ya kuwakaribisha waje kwako unaenda kuwapa shida huko uendako! Jiulize utawakaribisha lini?

unajuaje kama wanaenda kuwapa shida? sehemu zingine ni "mgeni njo mwenyeji apone"
 
Semea nafsi yako kwamba hayakuhusu. Hayawahusu wewe na nani? Kama hayawahusu mbona mnachangia? Kidogo kwako ni kikubwa kwangu. Kama unaona una uelewa mkubwa sana zaidi ya wenzako; pita uende zako!

Sasa wewe unaona kuna pointi yoyote katika hii mada? You dont have to be a rocket scientist to conclude that.
 
Una mtazamo mzuri sana! Mnanyanyasika kijinsia them mnadanganyika eti kuna usawa!

ila sasa best kuna hili jambo, hivi baba mkwe(mzaa mkeo) yupo ndani mwako unatoka brum na wife asbh anajua usiku mwanangu kakung'utwa mpera lol! sijui utaimamisha wapi uso.

yaani kitendo cha baba yako kujua ama kuhisi tu kwamba ulipelekewa mpera kinatosha kumwondolea konfo kabisaaa. sasa jambo la ajabu ni kwamba nikienda kwetu na mume wangu huwa tunalala as mr&mrs. na hapo natengewa chumba kabisaa kwa raha zetu............ mmmh! mm yani sijielewi nn ni nn.
 
Umeona eh? Mbege na kisusio kinahuu bana! Haya mabia na kitimoto samtaimz yanachosha.

Hakuna wa kunizuia. Wazazi wawepo wasiwepo kwenda mlimani ndio mpango mzima.

Haya Shime Preta, Kaizer, Kimey, Bigirita, Filipo, sweetlady, Lily Flower, Arushaone, @RR, Cantalisia, Rejao, Mkuu rombo et el..... Tukutane mlimani tarehe zinajongea.... Kuhesabiwa muhimu atiii.

We umekuja na hoja ambayo naweza kukubaliana nayo japo si kwa asilimia 100; kuhesabiwa!!!

Waisrael wanajuana idadi ulimwengu mzima lakini hawalazimishani kwenda kubanana nchini mwao Israel.
 
Inapendeza ni mzuri kurudi homie na watoto kwenda kujumuika na ndugu kula sikuu unawaonyesha na wanao mto ukitiyirika maji kuwa ukiwa mdogo unasoma ulikua unakuja kuoga hapo na mafrendie wa utoto maisha ni kupanga na kuchagua mwenye kwao aende akawashe kibatari nyama za pori inakua bomba mnaowaiga wazungu nyie kaukeni dar kimpango wenu na vurugu za mji huu heeeeeee.
 
ila sasa best kuna hili jambo, hivi baba mkwe(mzaa mkeo) yupo ndani mwako unatoka brum na wife asbh anajua usiku mwanangu kakung'utwa mpera lol! sijui utaimamisha wapi uso.

yaani kitendo cha baba yako kujua ama kuhisi tu kwamba ulipelekewa mpera kinatosha kumwondolea konfo kabisaaa. sasa jambo la ajabu ni kwamba nikienda kwetu na mume wangu huwa tunalala as mr&mrs. na hapo natengewa chumba kabisaa kwa raha zetu............ mmmh! mm yani sijielewi nn ni nn.

Kwani walikuruhusu uende kuishi na huyo mwanamume ili iweje? Mi mbona kwangu mama mkwe anakuja na sioni tatizo lolote!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom