Tuliharibiwa: Madhara ya Ufisadi Yanaonekana katika Masalia ya Fikra Za Watu Wetu

Kwa maoni yako Ufisadi umeacha madhara makubwa kwa taifa hadi sasa?


  • Total voters
    58
  • Poll closed .
mmmh.. lazima usome picha usione tu JPM anakuchekea itakula kwako... hoja muona Rostam anaimba mwenyewe "kidumu chama cha mapinduzi"... yuko kwenye hali mbaya sana jamaa.. na siku akitiwa pingu msije kushangaa "mbona alikunywa naye chai"...
Umeambiwa mtajie Wanasiasa watatu Top ambao walikuwa/wapo Serikalini walioshiriki ufisadi na wamefunguliwa mashtaka kwenye Vita zidi ya ufisadi.
 
Umeambiwa mtajie Wanasiasa watatu Top ambao walikuwa/wapo Serikalini walioshiriki ufisadi na wamefunguliwa mashtaka kwenye Vita zidi ya ufisadi.

Ni kwamba mwenzetu hata habari za nchi yetu hufuatilii au huamini unachosoma? Really.. unataka kunitafutie watu watatu tu.. mbona wako zaidi ya watatu.. google it..
 
mmmh.. lazima usome picha usione tu JPM anakuchekea itakula kwako... hoja muona Rostam anaimba mwenyewe "kidumu chama cha mapinduzi"... yuko kwenye hali mbaya sana jamaa.. na siku akitiwa pingu msije kushangaa "mbona alikunywa naye chai"...
Uliwahi tu ku-quoete post yangu kabla ya kujazia nyama vinginevyo labda ungekuwa na mengi ya ku-argue!!

But let's be honest here... man, we're talking of Ikulu hapa! Lau kama hiyo picha ingekuwa wamekutana somewhere else, hata kama wangekuwa wamekumbatiana na kupigana mabusu motomoto; wala nisingesema niliyosema na hapo hapo ningekubaliana na wewe kwa 101%! Kinyume chake, jamaa kafanya appointment, ikawa approved, akatimba hadi State House, wakanywa chai, wakatoka nje kupunga mikono ya kirafiki!

In some ways but less than 25% naweza kukubaliana na wewe kwamba, kwa Magu alivyo, anaweza kumkaribisha mtu Ikulu ili siku ya siku watu waseme "...yaani hata wale aliokuwa anacheka nao!" Lakini hiyo 75%, wala haielekei!
 
  1. Unaandika haya wakati Trilion 1.5 haijulikani zilipo
  2. Unaandika haya wakati waliosaini mikataba mibovu wapo wanapeta hakuna cha kufikishwa kwenye mahakama ya mafisadi wala cha nini
  3. unaandika haya wakati DC aliyekamatwa na rushwa kwenye Camera kapandishwa Cheo
  4. Unazungumza haya wakati watu wananunuliwa kuunga mkono juhudi
  5. Unazungumza haya wakati aliyeuza nyumba za serikali kakalia kigoda cha enzi
  6. Unazungumza haya wakati RC aliyeleta makontena na akataka kukwepa kodi bado yuko ofisini
  7. Unaongea haya wakati tunaambiwa Lugumu mambo yake swafi
Wewe Mzee unaota, Ufisadi gani unaouzungumzia?
Au umesahau maana ya ufisadi ni nini?
 
Kitu cha 1.5 trillion hakuna maelezo, alafu ati leo hakuna pesa za kulipa wastaafu. Nasema AJABU AJABU.

Wanadai pesa zimepelekewa kwenye miradi ILIHALI miradi yote imekopewa pesa zake? Jamani nauliza pesa ziko wapi?

Hiyo trilioni 1.5 sio kidogo atii ni mingi mno.
 
Na. M. M. Mwanakijiji
View attachment 949427

Tulizaliwa katika mfumo wa kifisadi; tulikua na kuishi katika mfumo huo, na tulikufa tukiujua mfumo huo peke yake. Ndani ya mfumo tulienda na tukawa; watoto wetu na wajukuu wakaukuta mfumo na kuamini ndio maisha pekee wanayoweza kuishi. Ili mtu afanikiwe alitakiwa awe fisadi mwezeshaji au fisadi mwezaji.
Tulitengeneza taifa la mafisadi wakongwe na mafisadi vijana; mafisadi waliopo na mafisadi watarajiwa. Ndugu zangu, madhara ya maisha haya sasa yanaonekana. Lakini tuweze kuelewa madhara yake ni vizuri kujua kabisa kuwa mfumo huu wa maisha uliwafanya watu waishi, jamii iende, nchi ionekane inakwenda n ahata pale ambapo haikwenda tulifisadiana katika kusaidiana kuifanya ionekane inaenda.
Ufisadi ulikuwa ni sehemu kubwa ya maisha kiasi kwamba watu walipanga bajeti za maisha na maendeleo na ndani yake waliweka bajeti ya ufisadi kukamilisha ndoto zao. Ukitaka kupata kibali cha shilingi 10,000 lazima utenge angalau 50,000 za kulainisha mikono ya watu. Ukitaka kujenga nyumba yako yenye gharama ya milioni mia moja gharama yake halisi ilikuwa kama milioni mia na hamsini – hamsini za kufanikisha mambo yako mbalimbali na yafanikiwe.

Hili lilikuwa kweli katika elimu, maji, afya, huduma mbalimbali na katika ngazi mbalimbali. Ufisadi ulikuwa ni sehemu ya maisha kuanzia kwenye kata vijiji hadi tarafa, wilaya hadi mikoa na tukaona ufisadi kutoka mikoa hadi taifa. Tukazoea kuishi kwenye maisha ya kashfa kubwa kubwa kama vile tunalazimishwa kuishi kwenye maji kama samaki; bila kashfa kubwa nchi ilikuwa haiendi. Kuanzia kashfa za kina Valambhia hadi kufika kina Rostam, kuanzia za kina Iddi Simba hadi Rugemalira Watanzania walizoea ufisadi na ufisadi uliwazoea Watanzania.

Tulicheka na kuchekeana katika ufisadi, tulizoea na kuzoeana , kubembeleza na kubembelezana huku tukisha na kushikana huku tukikodoleana na kutishana! Ufisadi ulikuwa kama dini iliyotuuunganisha, tukipiga magoti na kutoa dhabihu zetu za kushukuru mbele ya mafisadi katika madhabahu yao. Ukitaka kufanikiwa lazima umjue au umjue anayemjua anayejulikana. Ufisadi tungeweza kuuimbia nchi “ooh ufisadi wajenga nchi!” Na tuliamini ufisadi kweli kabisa unajenga nchi. Hata kama tuliulaani hadharani na kuwabeza mafisadi.

Uchaguzi wa 2015 ulikuwa ni ni uchaguzi wa ama kuendelea na maisha yale au kubadilisha mwelekeo. Ulikuwa ni uchaguzi wa kati ya kutamalaki kwa ufisadi au kuvunjwa vunjwa kwa madhabahu ya dini hiyo yenye watu wenye dini zote! Imani ya dini hiyo ni tumbo na kitabu chake kimeandikwa kwa maandishi ya tamaa. Uchaguzi ule ulikuwa ni wa ama kuendelea na tulivyokuwa tukiishi huku tunafurahi katika ufisadi wetu; hakuna maamivu ya moja kwa moja kila mtu akiishi kwa kujifurahisha mwenyewe na familia yake.
Ulikuwa ni uchaguzi wa kuamua kama tunataka kuuvunja mfumo huo haramau au kuulea kidogo kwa sababu tumeuzoea.

Tuliokuwa tumedeka kwenye mfumo huo hatukuweza kufikiria namna nyingine yoyote ya kuishi. Ni kama mtoto anayetoka kwenye familia iliyomdekeza na siku moja anaambiwa hakuna vya bure tena shika jembe ukalime. Mtoto yule anapolima kidogo tu mikono yote inamuuma na kuanza kuchubuka huku ikitokea malengelenge! Machozi yatamlenga na kujiuliza kumbe “kilimo ni kigumu hivyo”.
Hili linanikumbusha nilipoenda kuanza shule ya Sekondari miaka mingi nyuma kwenye shule ya Wazazi ya Boza, Pangani Tanga. Nakumbuka mtoto mmoja binti wa familia ya kitajiri aliyeletwa bweni kuanza maisha na kupaona mahali penyewe palivyo (wakati ule). Binti yule aliangusha kilio gari la wazazi wale lilipoondoka kumuacha na kwa karibu wiki nzima alikuwa hana raha mtoto wa watu, akigoma kula na tunashukuru Mungu hakukuwa na Facebook wala Whatsapp enzi hizo, wala Instagram! Kilichomsaidia binti yule (msema kweli Mpenzi wa Mungu) – ni kuwa alijaliwa “Neema za Allah” na vijana wengi (mimi si mmoja wapo) walijitolea kumsaidia kwa kazi zake mbalimbali – hasa ilipofika zamu ya kwenda kubeba kuni!

Baada ya muda alizoea, akazoea maisha ya kule kwani asingeweza kuwapa vijana wote vile walivyohitaji bila ya kujichafua jina lake. Miaka minne baadaye alipohitimu binti yule alikuwa ni “mama” akiwasaidia mabinti wengine walioifika pale na baadaye akaja kuolewa na mlalahoi mmoja. Aliingia shule akiwa hajui jinsi ya kushika kijiko, alihitimu akijua kushika mwiko; aliingia akiwa na madaha, alitoka akiwa na staha.
Ndugu zangu, ufisadi ulikuwa ni kama dawa ya kulevya; taratibu taratiu watu wakauzoea na mwisho wa siku wakata arosto. Uchumi wetu na maisha yetu kama taifa na kama mtu mmoja mmoja yalihitaji dozi ya dawa hii ya ufisadi ili mambo yaende. Alichofanya Magufuli na ambacho anaendelea kufanya (japo naona kama mwendo umepungua kidogo) ni kuwakatisha watu kupata dawa hii haramu. Matokeo yake watu sasa wako katika hali ya kuonesha withdrawal symptoms. Yaani, watu sasa wanagundua kuwa hawawezi kuishi bila kupata kitu kidogo kwenye damu zao. Kuna wengine ambao wanaona labda asingefanya kwa ukali hivi kwani wakati mwingine mtu anapokatishwa kutumia madawa kwa ghafla anaweza kuishia kuumwa sana na hata kufa! Je, Magufuli angefanya taratibu, abembeleze, asiguse sana uchumi na aachie achie kidogo ili watu wasiumie?

Ndugu zangu, leo hii wapo watu wanapata shida. Kuanza kumomonyolewa na kubanduliwa kwa mfumo wa utawala wa kifisadi kunawafanya watu wakose pa kushikilia. Wenye kulia wanalia, wenye kuumia wanaumia lakini nawaambia kwa uthabiti kabisa wa moyo kuwa hakuna wakati muhimu sana kwa historia ya Taifa letu kama wakati huu. Miaka hii mitatu ya mwanzo ya Rais Magufuli inanithibitishia kabisa kuwa tulichelewa sana na sasa maumivu tunayoyaona ni maumivu ya mtu aliyechelewa kupata tiba na sasa analazimika kufanyiwa upasuaji mkubwa; si mchezo, si lele mama.

Miaka hii mitatu ya kujaribu kuvunja ufisadi, kujenga taifa la watu wanaojiamini na kujitegemea kifikra si jambo rahisi. Makosa yatafanyika, matatizo mengine yataibuliwa, vingine vitaharibiwa lakini kiujumla wake maisha yataenda tu ndugu zangu. Hata wagonjwa wanapofanyiwa upasuaji si wote wanapona na wakati mwingine kunatoke “complications” lakini nia na uthubutu wa madaktari hauwezi kupuuzwa au kubezwa.

Miaka mitatu baadaye ninapoangalia taifa letu linapokwenda sina sababu yoyote ya kujuta kukata marudio na mwendelezo wa mfumo wa utawala wa kifisadi. Sina majuto ya kuunyoshea kidole na kuukataa hata kama ungerudishwa kwa kisingizio cha “mabadiliko” ya kuzungusha mikono. Mambo yote leo yanafanyika nilivyotarajia? La hasha! Kuna vitu ambavyo ningependa vifanyike na havifanyiki au visifanyike na vinafanyika? Si kidogo! Lakini, kutengeneza nidhamu mpya, njia mpya na mwelekeo bora wa kitaifa linafanyika? Bila ya shaka!

Miaka miwili ijayo, itatupa mwanga zaidi; tutaona zaidi mafanikio ya utawala huu na nina uhakika Watanzania wengi zaidi – pamoja na maumivu na usumbufu wa sasa – watasimama na kusema tunahitaji miaka mingine mitano. Gharama ya kujenga mfumo wa maendeleo ni kubwa sana na tumeanza kuilipa. Nina uhakika yatafanyika masahihisho ya maeneo yanayosumbua sasa hivi. Tusije kuthubutu kuangalia nyuma na kutamani kule tulikotoka. Tukatae kabisa kuambiwa ati wakati wa Kikwete na Mkapa ulikuwa ni mzuri sana kwa sababu tulikula “nyama, matikiti maji na vitunguu saumu”. Kwamba, kwa vile tuliishi katika Misri ya Ufisadi basi ilikuwa nzuri kwa sababu tulikuwa salama na wenye Amani. Tuwakatae na kuwapinga wanaotaka tukumbuke Misri ile ati tu kwa vile huku kwenye nchi ya ahadi kumbe tunatakiwa kufanya kazi, kuhenyeka na kufanya kazi kama uhai wetu unategemea.

Tusonge mbele kwa jitihada, ufanisi, na uwajibikaji. Tukifanya tunachopaswa kufanya basi kile tunachokifanya tutaona kweli kinatupasa!

Niandikie: klhnews@gmail.com
Big up mwanakijiji umeenda kwa ukweli kabisa, asiye na akili atamwaga matusi yote. Lakini ukweli ndo huo full stop.
 
uwe unafanya utafiti japo kidogo kabla hujasema. kuna wakurugenzi wangapi kwa mfano wenye kufuja na kuendlea na huo ufisadi? msafara wake una magari mangovyapi ya shiling ngapi? hovyo hovyo
 
Watu wa ajabu, hawaongelei mauaji, cococ beach, haki za binadamu , azory gwanda, Ben , mawazo, and all evils done by this dictatorial regime, wanaona upuuzi mdogo mdogo kuwa una offset artrocities hizi! Ukabila kitu kibaya. Hawa wote ni wasukuma (ingawa jamaa siyo msukuma by blood, specifically paternal blood), kitambaa cheusi kimewafunika machoni
Kumbe Mzee Mwanakijiji ni msukuma eeh? Ukabila kitu kibaya kupita maelezo. Ukabila huwa unakuwaga na kama “blanketi” flani hivi la ujinga. Hata mtu awe amesoma na exposure, hilo blanketi ni noma mbaya kabisa!😀 linafunikia mbalii! Unashangaa mtu anakuwa hola kabisa kichekesho na “unbelievable”
 
  1. Unaandika haya wakati Trilion 1.5 haijulikani zilipo
  2. Unaandika haya wakati waliosaini mikataba mibovu wapo wanapeta hakuna cha kufikishwa kwenye mahakama ya mafisadi wala nini
  3. unaandika haya wakati DC aliyekamatwa na rushwa kwenye Camera kapandishwa Cheo
  4. Unazungumza haya wakati watu wananunuliwa kuunga mkono juhudi
  5. Unazungumza haya wakati aliyeuza nyumba za serikali kakalia kigoda cha enzi
  6. Unazungumza haya wakati RC aliyeleta makontena na akataka kukwepa kodi bado yuko ofisini
  7. Unaongea haya wakati tunaambiwa Lugumu mambo yake swafi
  8. unaongea haya wakati Mzee wa Vijisenti ni mwenyekiti wa chombo nyeti na mikataba almost yote kaidraft yeye!
Wewe Mzee unaota?, Ufisadi gani unaouzungumzia kuwa tunapambana nao?
Au umesahau maana ya ufisadi ni nini?
 
Mwanakijiji bure kabisa. Kwa mfano Magufuli akifa leo ni transformation gani endelevu atakuwa ameiacha katika nchi hii ya kumkumbuka? Kunyimwa nyonfeza za mishahara? Kuzuia uhuru wa mawazo? Yeye binafs akifanta yfisadi nani atamsema? Kuamini kwamba yeye ndiye mzalendo pekee katika nchi? Huyu ambaye yeye mwenyewe kajifanya ni kila kitu? Huyu aliyeua mfumo wa kutaasisi katika nchi? Huyu ambaye ameivuruga kabisa duplomasia ya kimataifa kwa sababu za kipuuzi-uzalendo uchwara?

Huyu anayeamini yeye tu ndiye anajua kipi kinawafaa watanzania. Huyu anayedai hakuahidi katiba mpya? Yaani hajui maana ya katiba nzuri kwa nchi?

Kujenga nchi ni zaidi ya kupambana na ufisadi. As a leader you' ve got to be balanced.

By the way, huyu unayesema anapambana na ufisadi naye alikuwa sehemu ya ufisadi. Ni zao za mfumo wa kifisadi. Ndiyo maana anachofanya ni kujaribu kuonekana kama anapambanana ufisadi wakati in actual fact hafanyi hivyo. Kama kweli anapambana na ufisadi mbona hatuoni waliohusika kutengeneza huo ufisadi wakiwajibishwa? Nina maanisha viongozu na watawala waliopita mbona hawaonekani mahakamani, kinyumbe chake ni wale wadogowadogo?
Tuache kudanganyana. By the way, uelewa wako wa concept ya ufisadini narrow sana. Aidha kwa bahati mbaya au kwa kukussudia. Ufisadi ni zaidi ya wizi wa pesa za umma.

Kuua uhuru wa taasisi za checks na balances nao ni ufisadi. Hii ni kwa sababu rais na watu wake wachache sasa ndio wamejipa uhuru wa kufanya ufusadi bila kuulizwa na mtu yeyote. Sasa hivi ufisadi umekuwa centralized.
Ndio maana unaona rais anaweza kuamua kununua madege kwa cash money bila hata bunge kuhusishwa. Kujenga miundo mbinu mikubwa km viwanja vya ndege, maofsi na majengo ya taasisi kubwa kijijuni kwake bila kuhojiwa na yeyote. Kuruhusu baadhi ya wateule wake kufanya lolote bila kuhojiwa ( ref Makonda).
Ndugu yangu MM huu wote ni ufisadi na ni mbaya kuliko unaouzungumzia.
 
Ni kwamba mwenzetu hata habari za nchi yetu hufuatilii au huamini unachosoma? Really.. unataka kunitafutie watu watatu tu.. mbona wako zaidi ya watatu.. google it..
Kwanini ni-Google... nitajie! Please, not any politician kama akina Faraja Maranda ambao hata JK aliwatupa jela... nitajie high profile politicians wenye tuhuma za grand corruption ambao wamefunguliwa jalada!

Tena si afadhali hata JK's corrupt administration iliwatoa kafara akina Daniel Yona... name me 3 please!
 
uwe unafanya utafiti japo kidogo kabla hujasema. kuna wakurugenzi wangapi kwa mfano wenye kufuja na kuendlea na huo ufisadi? msafara wake una magari mangovyapi ya shiling ngapi? hovyo hovyo

kwani msafara wake anajipangia yeye mwenyewe... au ulinzi wake unaongozwa na mawazo yake.. jifunze kidogo haya mambo. Kwani msafara wa Kikwete na wa Mkapa ulikuwa na watu wangapi ili ulinganishe?
 
Kwanini ni-Google... nitajie! Please, not any politician kama akina Faraja Maranda ambao hata JK aliwatupa jela... nitajie high profile politicians wenye tuhuma za grand corruption ambao wamefunguliwa jalada!

Tena si afadhali hata JK's corrupt administration iliwatoa kafara akina Daniel Yona... name me 3 please!

Kwa kweli sikusaidii kwenye hili... mbona ni mwaka wa tatu tu; swali kama hili kwanza linahitaji JPM awe amemaliza muda wake na kusema "katika utawala wake hajafanya hili au lile". Sipendi kuweka magoli. Ila atakapotoka madarakani kuna watu watakuwa "wamelimia meno"...
 
Kumbe Mzee Mwanakijiji ni msukuma eeh? Ukabila kitu kibaya kupita maelezo. Ukabila huwa unakuwaga na kama “blanketi” flani hivi la ujinga. Hata mtu awe amesoma na exposure, hilo blanketi ni noma mbaya kabisa!😀 linafunikia mbalii! Unashangaa mtu anakuwa hola kabisa kichekesho na “unbelievable”

Mushi.. you should know better bwana; yaani kwa vile mtu kasema mimi ni "Msukuma" na wewe umekubali tu kuwa mimi ni Msukuma? Sina damu ya Kisukuma upande wowote wa wazazi wangu.
 
Mzee mwenzangu; hivi unafikiria hizi "atrocities" zimeanza leo? au zimeanza miaka hii mitatu ya JPM. Mbona tunaofuatilia siasa za nchi yetu hakuna lolote ambalo limetokea sasa ambalo halikutokea wakati wa Mkapa au Kikwete. It can even be argued (easily) kuwa sasa hivi yamepungua sana...
Hhahaa! This's new Mwanakijiji... lazima siku uwe una-justify udhalimu unaofanyika na ule uliowahi kufanyika! Utasikia "hii si mara ya kwanza kutokea... hata enzi za deshi na deshi iliwahi kutokea!" Come on man, stop this!!

Btw, hao wengine tayari tunawajua hawakuwa ma-"superman" like Magufuli! So, haina maana yoyote unapojaribu kuhalalisha udhalimu unaofanyika ndani ya "superman" administration kwa sababu udhalimu kama huo uliwahi kutokea kwa watawala ambao hawakuwa "superman"!
 
Mzee Mwanakijiji , hapo uliposema “tusubiri miaka miwili ijayo”, inaonyesha bado uko kwenye ile kitu inaitwa denial.

Ngoja tu niseme Labda utakuwa umeangukia kwenye kundi la wale “laggards”

Kuna watu ambao huwa inachukuwa muda mrefu zaidi kuelewa na kuona jambo flani. Sababu za kuchelewa huko zinaweza kuwa za aina mbali mbali.

Mimi ni mpaka nitakapoona juhudi sahihi kuhusiana na sera ya Tanzania ya viwanda, ndipo nitasema kuna matumaini, siyo hizi vurugu mechi.

Pia kama nia ni kumaliza ufisadi, kumiminya uhuru wa habari ni kuhakikisha hayo yanafunikwa. Kwahiyo ufisadi una kuwepo lakini kwa siri.

Kuna mtu alichukia ufisadi kama mwalimu Nyerere? Lakini walijipanga na wakaendelea kutafuna nchi pamoja na ukali wote wa mwalimu. Yani inakuwa siri kubwa tu lakini tatizo lina kuwa pale pale. Ni vyema sana kusikiliza mawazo mbadala hata kama hutayatumia, utaweza kupata mwangaza flani na kuona mambo in different dimensions
 
Back
Top Bottom