Tuliharibiwa: Madhara ya Ufisadi Yanaonekana katika Masalia ya Fikra Za Watu Wetu

Kwa maoni yako Ufisadi umeacha madhara makubwa kwa taifa hadi sasa?


  • Total voters
    58
  • Poll closed .

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,203
2,000
Na. M. M. Mwanakijiji

1543422226438.png


Tulizaliwa katika mfumo wa kifisadi; tulikua na kuishi katika mfumo huo, na tulikufa tukiujua mfumo huo peke yake. Ndani ya mfumo tulienda na tukawa; watoto wetu na wajukuu wakaukuta mfumo na kuamini ndio maisha pekee wanayoweza kuishi. Ili mtu afanikiwe alitakiwa awe fisadi mwezeshaji au fisadi mwezaji.
Tulitengeneza taifa la mafisadi wakongwe na mafisadi vijana; mafisadi waliopo na mafisadi watarajiwa.

Ndugu zangu, madhara ya maisha haya sasa yanaonekana. Lakini tuweze kuelewa madhara yake ni vizuri kujua kabisa kuwa mfumo huu wa maisha uliwafanya watu waishi, jamii iende, nchi ionekane inakwenda n ahata pale ambapo haikwenda tulifisadiana katika kusaidiana kuifanya ionekane inaenda.

Ufisadi ulikuwa ni sehemu kubwa ya maisha kiasi kwamba watu walipanga bajeti za maisha na maendeleo na ndani yake waliweka bajeti ya ufisadi kukamilisha ndoto zao. Ukitaka kupata kibali cha shilingi 10,000 lazima utenge angalau 50,000 za kulainisha mikono ya watu. Ukitaka kujenga nyumba yako yenye gharama ya milioni mia moja gharama yake halisi ilikuwa kama milioni mia na hamsini – hamsini za kufanikisha mambo yako mbalimbali na yafanikiwe.

Hili lilikuwa kweli katika elimu, maji, afya, huduma mbalimbali na katika ngazi mbalimbali. Ufisadi ulikuwa ni sehemu ya maisha kuanzia kwenye kata vijiji hadi tarafa, wilaya hadi mikoa na tukaona ufisadi kutoka mikoa hadi taifa. Tukazoea kuishi kwenye maisha ya kashfa kubwa kubwa kama vile tunalazimishwa kuishi kwenye maji kama samaki; bila kashfa kubwa nchi ilikuwa haiendi. Kuanzia kashfa za kina Valambhia hadi kufika kina Rostam, kuanzia za kina Iddi Simba hadi Rugemalira Watanzania walizoea ufisadi na ufisadi uliwazoea Watanzania.

Tulicheka na kuchekeana katika ufisadi, tulizoea na kuzoeana , kubembeleza na kubembelezana huku tukisha na kushikana huku tukikodoleana na kutishana! Ufisadi ulikuwa kama dini iliyotuuunganisha, tukipiga magoti na kutoa dhabihu zetu za kushukuru mbele ya mafisadi katika madhabahu yao. Ukitaka kufanikiwa lazima umjue au umjue anayemjua anayejulikana. Ufisadi tungeweza kuuimbia nchi “ooh ufisadi wajenga nchi!” Na tuliamini ufisadi kweli kabisa unajenga nchi. Hata kama tuliulaani hadharani na kuwabeza mafisadi.

Uchaguzi wa 2015 ulikuwa ni ni uchaguzi wa ama kuendelea na maisha yale au kubadilisha mwelekeo. Ulikuwa ni uchaguzi wa kati ya kutamalaki kwa ufisadi au kuvunjwa vunjwa kwa madhabahu ya dini hiyo yenye watu wenye dini zote! Imani ya dini hiyo ni tumbo na kitabu chake kimeandikwa kwa maandishi ya tamaa. Uchaguzi ule ulikuwa ni wa ama kuendelea na tulivyokuwa tukiishi huku tunafurahi katika ufisadi wetu; hakuna maamivu ya moja kwa moja kila mtu akiishi kwa kujifurahisha mwenyewe na familia yake.

Ulikuwa ni uchaguzi wa kuamua kama tunataka kuuvunja mfumo huo haramau au kuulea kidogo kwa sababu tumeuzoea.

Tuliokuwa tumedeka kwenye mfumo huo hatukuweza kufikiria namna nyingine yoyote ya kuishi. Ni kama mtoto anayetoka kwenye familia iliyomdekeza na siku moja anaambiwa hakuna vya bure tena shika jembe ukalime. Mtoto yule anapolima kidogo tu mikono yote inamuuma na kuanza kuchubuka huku ikitokea malengelenge! Machozi yatamlenga na kujiuliza kumbe “kilimo ni kigumu hivyo”.

Hili linanikumbusha nilipoenda kuanza shule ya Sekondari miaka mingi nyuma kwenye shule ya Wazazi ya Boza, Pangani Tanga. Nakumbuka mtoto mmoja binti wa familia ya kitajiri aliyeletwa bweni kuanza maisha na kupaona mahali penyewe palivyo (wakati ule). Binti yule aliangusha kilio gari la wazazi wale lilipoondoka kumuacha na kwa karibu wiki nzima alikuwa hana raha mtoto wa watu, akigoma kula na tunashukuru Mungu hakukuwa na Facebook wala Whatsapp enzi hizo, wala Instagram! Kilichomsaidia binti yule (msema kweli Mpenzi wa Mungu) – ni kuwa alijaliwa “Neema za Allah” na vijana wengi (mimi si mmoja wapo) walijitolea kumsaidia kwa kazi zake mbalimbali – hasa ilipofika zamu ya kwenda kubeba kuni!

Baada ya muda alizoea, akazoea maisha ya kule kwani asingeweza kuwapa vijana wote vile walivyohitaji bila ya kujichafua jina lake. Miaka minne baadaye alipohitimu binti yule alikuwa ni “mama” akiwasaidia mabinti wengine walioifika pale na baadaye akaja kuolewa na mlalahoi mmoja. Aliingia shule akiwa hajui jinsi ya kushika kijiko, alihitimu akijua kushika mwiko; aliingia akiwa na madaha, alitoka akiwa na staha.
Ndugu zangu, ufisadi ulikuwa ni kama dawa ya kulevya; taratibu taratiu watu wakauzoea na mwisho wa siku wakata arosto.

Uchumi wetu na maisha yetu kama taifa na kama mtu mmoja mmoja yalihitaji dozi ya dawa hii ya ufisadi ili mambo yaende. Alichofanya Magufuli na ambacho anaendelea kufanya (japo naona kama mwendo umepungua kidogo) ni kuwakatisha watu kupata dawa hii haramu. Matokeo yake watu sasa wako katika hali ya kuonesha withdrawal symptoms. Yaani, watu sasa wanagundua kuwa hawawezi kuishi bila kupata kitu kidogo kwenye damu zao. Kuna wengine ambao wanaona labda asingefanya kwa ukali hivi kwani wakati mwingine mtu anapokatishwa kutumia madawa kwa ghafla anaweza kuishia kuumwa sana na hata kufa! Je, Magufuli angefanya taratibu, abembeleze, asiguse sana uchumi na aachie achie kidogo ili watu wasiumie?

Ndugu zangu, leo hii wapo watu wanapata shida. Kuanza kumomonyolewa na kubanduliwa kwa mfumo wa utawala wa kifisadi kunawafanya watu wakose pa kushikilia. Wenye kulia wanalia, wenye kuumia wanaumia lakini nawaambia kwa uthabiti kabisa wa moyo kuwa hakuna wakati muhimu sana kwa historia ya Taifa letu kama wakati huu. Miaka hii mitatu ya mwanzo ya Rais Magufuli inanithibitishia kabisa kuwa tulichelewa sana na sasa maumivu tunayoyaona ni maumivu ya mtu aliyechelewa kupata tiba na sasa analazimika kufanyiwa upasuaji mkubwa; si mchezo, si lele mama.

Miaka hii mitatu ya kujaribu kuvunja ufisadi, kujenga taifa la watu wanaojiamini na kujitegemea kifikra si jambo rahisi. Makosa yatafanyika, matatizo mengine yataibuliwa, vingine vitaharibiwa lakini kiujumla wake maisha yataenda tu ndugu zangu. Hata wagonjwa wanapofanyiwa upasuaji si wote wanapona na wakati mwingine kunatoke “complications” lakini nia na uthubutu wa madaktari hauwezi kupuuzwa au kubezwa.

Miaka mitatu baadaye ninapoangalia taifa letu linapokwenda sina sababu yoyote ya kujuta kukata marudio na mwendelezo wa mfumo wa utawala wa kifisadi. Sina majuto ya kuunyoshea kidole na kuukataa hata kama ungerudishwa kwa kisingizio cha “mabadiliko” ya kuzungusha mikono. Mambo yote leo yanafanyika nilivyotarajia? La hasha! Kuna vitu ambavyo ningependa vifanyike na havifanyiki au visifanyike na vinafanyika? Si kidogo! Lakini, kutengeneza nidhamu mpya, njia mpya na mwelekeo bora wa kitaifa linafanyika? Bila ya shaka!

Miaka miwili ijayo, itatupa mwanga zaidi; tutaona zaidi mafanikio ya utawala huu na nina uhakika Watanzania wengi zaidi – pamoja na maumivu na usumbufu wa sasa – watasimama na kusema tunahitaji miaka mingine mitano. Gharama ya kujenga mfumo wa maendeleo ni kubwa sana na tumeanza kuilipa. Nina uhakika yatafanyika masahihisho ya maeneo yanayosumbua sasa hivi. Tusije kuthubutu kuangalia nyuma na kutamani kule tulikotoka. Tukatae kabisa kuambiwa ati wakati wa Kikwete na Mkapa ulikuwa ni mzuri sana kwa sababu tulikula “nyama, matikiti maji na vitunguu saumu”.

Kwamba, kwa vile tuliishi katika Misri ya Ufisadi basi ilikuwa nzuri kwa sababu tulikuwa salama na wenye Amani. Tuwakatae na kuwapinga wanaotaka tukumbuke Misri ile ati tu kwa vile huku kwenye nchi ya ahadi kumbe tunatakiwa kufanya kazi, kuhenyeka na kufanya kazi kama uhai wetu unategemea.

Tusonge mbele kwa jitihada, ufanisi, na uwajibikaji. Tukifanya tunachopaswa kufanya basi kile tunachokifanya tutaona kweli kinatupasa!

Niandikie: klhnews@gmail.com
 

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
15,605
2,000
Naona umepigiwa simu kuja kutuliza hali ya hewa,lakini kumbuka it's too late,ndio umechelewa sana watu wengi sasa hivi wanaugulia maumivu ya hali ngumu,ajira,mafao ya kustaafu,kutokujua kesho yao na kikubwa zaidi kukosekana uhuru wa kukosoa yale mabaya yanayofanywa kwa kichaka cha Uzalendo na kujenga Nchi bila kusahau ukosefu wa Usalama na vitisho vya Dola.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,203
2,000
Naona umepigiwa simu kuja kutuliza hali ya hewa,lakini kumbuka it's too late,ndio umechelewa sana watu wengi sasa hivi wanaugulia maumivu ya hali ngumu,ajira,mafao ya kustaafu,kutokujua kesho yao na kikubwa zaidi kukosekana uhuru wa kukosoa yale mabaya yanayofanywa kwa kichaka cha Uzalendo na kujenga Nchi bila kusahau ukosefu wa Usalama na vitisho vya Dola.
Uchaguzi huwa una matokeo - elections have consequences; ukitaka sera tofauti kwenye nchi unahitaji kushinda uchaguzi... na ufanye yote unayoweza ili ushinde hata kama ni kwa hatua... (kwa mfano, kushinda serikali za mitaa, kushinda bunge, n.k). Usilalamikie tu sera za wastaafu usizozipenda... ungana na chama au unga mkono chama ambacho kina sera unazozipenda. Ndio maana ya demokrasia.
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
28,310
2,000
yani wewe jamaa akili na fikra zako hazina tofauti kabisa na pascal mayalla.mnahitaji msaada mkubwa kuliko nyie mnavyo jidhania kuwa mpo sawa
Watu wa ajabu, hawaongelei mauaji, cococ beach, haki za binadamu , azory gwanda, Ben , mawazo, and all evils done by this dictatorial regime, wanaona upuuzi mdogo mdogo kuwa una offset artrocities hizi! Ukabila kitu kibaya. Hawa wote ni wasukuma (ingawa jamaa siyo msukuma by blood, specifically paternal blood), kitambaa cheusi kimewafunika machoni
 

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,053
2,000
Watu wa ajabu, hawaongelei mauaji, cococ beach, haki za binadamu , azory gwanda, Ben , mawazo, and all evils done by this dictatorial regime, wanaona upuuzi mdogo mdogo kuwa una offset artrocities hizi! Ukabila kitu kibaya. Hawa wote ni wasukuma (ingawa jamaa siyo msukuma by blood, specifically paternal blood), kitambaa cheusi kimewafunika machoni
Kuna msemo mzuri wa wahenga usemao "Kill Without Mercy for The Sake Of Mercy"... Me say
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,203
2,000
Hii hoja ya watu wafanye kazi huwa inakera sana! Utadhani katika nchi hii huko awali watu walikuwa wanapewa ugali, ada, kodi na CCM kwenye milango yao!!

Usije kudhani "kufanya kazi" ina maana ya kujishughulisha; siyo kila anayejishughulisha anafanya kazi na siyo kila aliyekuwa anapata ugali, kulipa ada na kodi alikuwa anapata hela kutoka kwenye "kazi" yake. Unless unafikiria ufisadi ni ajira.
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,723
2,000
Tulicheka na kuchekeana katika ufisadi, tulizoea na kuzoeana , kubembeleza na kubembelezana huku tukisha na kushikana huku tukikodoleana na kutishana! Ufisadi ulikuwa kama dini iliyotuuunganisha, tukipiga magoti na kutoa dhabihu zetu za kushukuru mbele ya mafisadi katika madhabahu yao. Ukitaka kufanikiwa lazima umjue au umjue anayemjua anayejulikana. Ufisadi tungeweza kuuimbia nchi “ooh ufisadi wajenga nchi!” Na tuliamini ufisadi kweli kabisa unajenga nchi. Hata kama tuliulaani hadharani na kuwabeza mafisadi.
Tumeacha kuchekeana na mafisadi?!
RA.png

Mzee Mwanakijiji, you know better than this...

To every grand corruption, there will always be two sides of players; upande wa kwanza utahusisha, most likely business persons na upande wa pili utahusisha ama top government executives or high profile politician or both!

Tangu hizi drama za kupambana na ufisadi zianze, unakuta ni upande wa wafanya biashara tu ndio kwa mbaaaaaali unaguswa guswa wakati upande mwingine muhimu to keep corruption in equilibrium; hauguswi!

Mbaya zaidi, wale wanaoguswa wala hawawajibiki kwa Watanzania lakini wale wasioguswa, ndio tuliowapigia au kuwahi kuwapigia kura au ndio wanaoishio kwa kodi za wananchi!

Rugemalila kwa mfano, why should I be too concerned with Ruge mtu ambae hana wajibu wa kulinda maslahi yangu badala ya kuwa concerned na watu waliosababisha Ruge kuchota alizochota kwa sababu ni hawa watu ndio nina mkataba nao wa kuhakikisha wanalinda maslahi yangu na ya umma kwa ujumla!

Kwanini niwe concerned na yule mwenye madevu na kilemba wakati hata nikimwambia atamke jina langu kwa ufasaha huenda akashindwa lakini nijifanye kana kwamba huyo mwenye madevu alienda na vifaru pale BoT kiasi kwamba wale waliokuwa na wajibu wa kulinda maslahi yangu na ya taifa kwa ujumla; hawakuwa na jinsi zaidi ya kumwacha achote atakazo!

If am wrong, nitajie ONLY THREE high profile politicians and/or top government executives ambao wameguswa in the so called vita dhidi ya ufisadi! Kinyume chake, ningekushauri achana na hizo porojo kwa sababu bado mnacheka, kula, kunywa, kutembea na kupiga cheers na mafisadi na mengine yote ni porojo tu!

QN: Unadhani Said Lugumi alifanya ufisadi au alisingiziwa?
 

Denis denny

JF-Expert Member
Oct 7, 2012
5,787
2,000
Hata magufuli aliishi katika mfumo huo naye ni ngumu kujinasua sababu anatabaka lake tayari la kina makonda ambao ni master mind wa mission to be possible by any means..imefika mizizi komavu imeingia mizizi king'ang'anizi hakuna rangi tutaacha ona ..safari ndo kwanza imeanza
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,203
2,000
Watu wa ajabu, hawaongelei mauaji, cococ beach, haki za binadamu , azory gwanda, Ben , mawazo, and all evils done by this dictatorial regime, wanaona upuuzi mdogo mdogo kuwa una offset artrocities hizi! Ukabila kitu kibaya. Hawa wote ni wasukuma (ingawa jamaa siyo msukuma by blood, specifically paternal blood), kitambaa cheusi kimewafunika machoni

Mzee mwenzangu; hivi unafikiria hizi "atrocities" zimeanza leo? au zimeanza miaka hii mitatu ya JPM. Mbona tunaofuatilia siasa za nchi yetu hakuna lolote ambalo limetokea sasa ambalo halikutokea wakati wa Mkapa au Kikwete. It can even be argued (easily) kuwa sasa hivi yamepungua sana...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom