Tulianzisha kanisa feki pamoja, anafosi nimuoe, vinginevyo anamwaga mboga

Na sisi waumini tujifunze kumtafuta Mungu binafsi nikimaanisha kusoma neno na kufanya maombi wewe mwenyewe. Mungu hana upendeleo, ukimtafuta kwa bidii utamuona. Kwenye ibada twende lakini macho na masikio yetu yawe wazi kupima yale tunayosikia. Tumeruhusiwa kuzijaribu roho kama zimetoka kwa Mungu au la. Tusipende shortcut.
 
Shida ya kuanza kwa kupanda mbegu ya uongo... Alafu tunaexpect Holy fruit... Haiendi hivyo hata kidogo. Two options :muachie vyote your business partner and start a fresh with God... Or else marry your business partner na muuendeleze huo uongo na kula matunda ya uongo...

Pamoja na yote niliyoyaandika hapa... Hii story nahisi ni stoooooriiii....
 
Mkuu kuna laana kubwa zaidi ya hicho anachokifanya? Huyu mtu amekuwa akimkejeri MUNGU kwa kipindi chote hicho, amedanganya watu na yumkini kesha zini na washiriki wake wengi tu. Anyway MUNGU ni mwema kwa kila mtu, yeye anachopaswa kufanya ni kutubu na kuwa na mwanzo mpya. Tofauti na hapo, hakuna asubuhi kwake.

Very true
 
Umempa majibu mazuri!!!!!!!!!!!!!!
OFA MOJA KWA AJILI YAKO LEO PLEASE!!!!!!!!!!!!
kipi bora!! Noah au Viti maalumu au Viti MOto...................
JOKING<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<:violin::drum::bounce::focus:
noah....
 
Nilipotoka chuo 2008 nilipata kazi yenye mshahara mdogo usioweza kufika hata tarehe 15, nikaona nitafute shughuli jioni baada ya kazi kuongeza kipato.

Mtaani kulikua na msichana mmoja Mshikaji wangu sana alikua amemaliza ualim ttc na alikua amepangwa hapo hapo mkoani, tukaamua Ku team up na kuanzisha kanisa letu ili tupate kipato zaidi, tulianza kama kikundi tu cha kuabudu huku tukitembea huku na huko kuwabembeleza wengine kujiunga, hatukua na upako wowote isipokua tulikua na vipaji vya kuongea mbele za watu bila hofu, Hasa mm ambae chuoni nilishiriki serikali ya wanafunzi

Tulikua tunafanyia ibada zetu katika kiwanja cha jamaa mmoja ambae aliishi dar hakua amekijenga bado, tulinunua turubai la blue la UNCR kubwa na tukawa tunaabudu hapo, kwa kweli karibu mshahara wangu wote ulikua unaishia pale, kununua viti vya plastic na mengineyo .

Kanisa liliendelea kukua na watu wakiongezeka kila wiki, after 2 years bulimia na waumini 102 hivi, kazi ya kupata waumin ni ngumu mno, na hasa wale wenye kazi zinazoeleweka.

Tumeendelea hivyo kwa muda hadi mwaka 2012 tulipoweza kumlipa mwenye kiwanja 15 million na hivyo kutuachia kiwanja, na 2013 tulianza kujenga Jengo dogo Pembeni ya hema tunalotumia tunatumia sadaka kulijenga, tuna waumini 530 active kwa sasa, hawa ni wale waliosajiliwa rasmi kwenye vitabu vyetu, ila wapo wapita njia wanaokuja wakiwa na magonjwa na shida mbali mbali na baadee kuondoka kama hawakupona.

Kwa sasa tumeacha kazi sehemu zetu za Ajira tunategemea kanisa.

Tatizo lenyewe

Huyu msichana tangu tunaanzisha hili kanisa tumekua marafiki Wa kawaida na Mara kadhaa Huwa tunakutana kimwili just for fun, hatukuwahi kuongelea ndoa hats siku moja, ila sijawahi kumuona na mchumba wala mpenzi, kumbe kipindi chote hicho ananisubiri mimi.

Kwamba aje kuwa mama mchungaji, mimi kwa bahati mbaya sikulifahamu hilo, nilishaanzisha uhusiano na msichana mmoja tuliemwingiza kanisani na tunapendana, tumepanga kufunga ndoa muda si mrefu.

Sasa binti tulieanzisha nae kanisa amekua akiwaambia watu wa karibu kwamba sisi ni wachumba na baadhi ya waumini wetu kuamini hivyo, mwezi uliopiita imenilazimu kumuita na kuzungumza nae kuhusu suala hilo, nikamueleza ukweli, cha ajabu ameacha kuja kanisani wiki ya tatu sasa.

Kaongea na mwenzangu mmoja katishia kwamba atasema kila kitu kwa waumini kwamba kanisa ni feki na sisi ni matapeli labda nimuoe yeye, sasa najiuliza hivi mtu kutembea na wewe m mbili tatu ni lazima nikuoe hata kama tabia sio nzuri?

Watu wa mungu naomba nijue kuna uhalali wowote wa huyu binti kulazimisha ndoa wakati Mimi simpendi kimapenzi?

Tunaogopa kumtimua kanisani maana anaweza kuharibu kila kitu.

Nimehangaika sana na hili kanisa na walau sasa hivi ndo naanza kuona matunda sasa siwezi kubali kuona mtu analivuruga kanisa, nipo radhi kutumia njia yoyote kumzimisha (mwenzetu mmoja ameshauri elimination method).

Maana anaweza haribu kila kitu tukimwacha, hasa akiwaeleza wainjilisti tunaowategemea kuombea wagonjwa na wenye shida mbali mbali.

Msaada wenu Wa mawazo unahitajika sana, mungu awabariki.

Mungu mkubwa haya ndio makanisa ya kiroho niliyokuwa nayaongelea kwenye post yangu ya leo asubuhi sijui imepelekwa wapi
 
siku Yesu akiwaambia tokeni hapa nyumba ya baba yangu siyo pango la wanyang'anyi ndo utajua
 
Eeeh! we unapoteza kondoo wa mwenyewe! sasa subiri arudi utakiona cha moto.
 
Bongo yangu inashindwa kuchakata hii data ya "ufeki"ivi hamkua na wito kumbe mlipojivika vazi la utumishi asee haikaii bongoni mwangu yaani mmejenga safina alafu hamuingii ndani yake "Kamesi"wakubwa nyie tubuni mkabatizwe nanyi mtapokea kipawa cha roho!
 
Back
Top Bottom