Tuliaminishwa na Media kuwa Bakhresa anakwepa kodi kumbe upotoshaji baada ya kauli ya Rais

Sasa najiuliza hizo habari za ukwepaji wa kodi wa Said Bakheresa, waandishi wetu wa habari na baadhi ya members wenzetu humu JF walikuwa wanazipata wapi.
Wanamsingizia tu, Bakhresa ni mlipakodi mzuri tu:

By Erick Kabendera

The government's new measures to curb tax evasion have helped the Tanzania Revenue Authority collect over Tsh1.3 trillion in less than two months.

President John Magufuli has cracked the whip on TRA and Dar es Salaam port senior officials who were suspected of colluding with business people to import thousands of containers without paying taxes.

As a result of the crackdown, at least 20 officials accused of involvement in the illegal network have been sacked and most of them charged with abuse of office.

Officials of Azam Inland Container Depot (ICD), owned by prominent businessman Said Salim Bakhresa, were also charged alongside TRA officials for economic sabotage and causing loss of Tsh12.7 billion in unpaid taxes.


Na waongo wengine hawa hapa

Dr Mpango explained further that Said Salim Bakhresa and Company Limited was required to pay Sh12.6bn as owner of the ICD where all the 329 containers were kept.

He said in addition to Sh2.2bn the company had already paid, it was expected to pay Sh2bn more yesterday afternoon.

He elaborated that TRA expected to collect Sh12.6bn from Azam ICD, which is owned by Said Salim Bakhresa and Company Ltd.

The TRA chief said other companies whose clearance of their containers did not abide by the procedure would also be required to clear the payments within seven days as directed by President Magufuli.

Other companies on the list, with their number of containers in brackets, included Lotai Steel Tanzania Ltd (100); Tifo Global Mart (Tanzania) Company Limited (30); IPS Roofing Company Limited (20); Rushywheel Tyre Centre Co Ltd(12); Homing International Limited (9); Red East Building Materials Company Ltd (7), and Tybat Trading Co Limited (5).
 
Mkuu kwa faida ya JF unaweza kutufahamisha hayo madeni yake aliyolipa yalikuwa kiasi gani?

Na hayo madeni alikopa wapi mkuu?

Tunasubiri majibu.
Rais aliwatangazia wote waliokuwa wanadaiwa kodi walipe,tena aliwapa muda. sema tulijawa nas iasa za maji taka. Haya tunaamini amelipa ndio maana rais amefika pale kuahidi kuendelea kumpa sapoti. Tuache gubu mkuu,kama mambo yamekaa sawa ya nini kuendeleza figisu. Tujenge nchi ya viwanda.
 
images-137.jpeg
 
Wanaukumbi.

Kupitia humu JF tulikuwa tunasoma habari kutoka kwa members wenzetu na waandishi wa habari kuwa mfanyabiashara Said Bakhresa, ni mkwepa kodi mkubwa ambaye anaikosesha serikali mapato.

Lakini leo kinyume chake tumemsikia leo Rais Magufuli, akisema kuwa "hongera sana mzee wangu Bakhresa. Wewe ni mlipaji kodi mzuri, na mimi napenda walipa kodi."

Sasa najiuliza hizo habari za ukwepaji wa kodi wa Said Bakheresa, waandishi wetu wa habari na baadhi ya members wenzetu humu JF walikuwa wanazipata wapi.

Au ndiyo muendelezo wa chuki zisizo na msingi dhidi ya mzalendo mlipaji kodi mzuri Mzee Bakheresa.
View attachment 413553
Kwahiyo hata ile sukari yake iliyoshikiliwa na serikali, na rais akaamuru waziri aichalie, nayo iliaminishwa na waandishi wa habari na members wa JF?
 
Achana na wanasiasa... Kama mizigo ilipitishwa bandarini bila kulipiwa inavyostahili manaka alikwepa kodi!! Sema kunamda wanasiasa humpamba mtu for a reason, ofcause huwezi zindua kiwanda huku ukimponda mmiliki.
Mbona unachosha, unamaanisha Raisi wetu ni mnafiki na hasemi ukweli bali anampamba Bakhresa.

Tuache chuki na wivu, tulishaambiwa tunaongoza kwa wivu.

Bakhresa kaanzia mbali sana na ameonyesha uutu wake kwa mtu msafi, mwenye imani na anaipenda nchi yake. Ni mlipaji wa kodi vizuri sana. Wakwepa kodi wanajulikana tokea enzi za Mwalimu na hata katika awamu zilizopita.

Nadhani katika wafanyi biashara wote hapa nchini, Bakhresa ni number 1 kwa kutoa ajira directly na indirectly period.
 
Ndio waandishi wetu hao. Tatizo la waandishi wetu ni kutojua kutofautisha taaluma (academic) na ujuzi (profession). Waandishi wa wenzetu kwanza mtu anakuwa mtu anakuwa mwanamazingira halafu ndio anaenda kusomea fanibya habari ili awe mchambuzi katika masusla ya mazingira. Kwetu ni tofauti, kiasi waandike uzushi.
 
Wanaukumbi.

Kupitia humu JF tulikuwa tunasoma habari kutoka kwa members wenzetu na waandishi wa habari kuwa mfanyabiashara Said Bakhresa, ni mkwepa kodi mkubwa ambaye anaikosesha serikali mapato.

Lakini leo kinyume chake tumemsikia leo Rais Magufuli, akisema kuwa "hongera sana mzee wangu Bakhresa. Wewe ni mlipaji kodi mzuri, na mimi napenda walipa kodi."

Sasa najiuliza hizo habari za ukwepaji wa kodi wa Said Bakheresa, waandishi wetu wa habari na baadhi ya members wenzetu humu JF walikuwa wanazipata wapi.

Au ndiyo muendelezo wa chuki zisizo na msingi dhidi ya mzalendo mlipaji kodi mzuri Mzee Bakheresa.
View attachment 413553
Hivi rais ndiye asesa wa kodi?
 
Hakuna mkate mgumu mbele ya chai,hata kama anakwepa kodi mfanyabiashara ni yuko mbele kuliko serikali lazima waufyate tu hawa tycoons sio watu wa mchezo wanaweza kuzamisha jahazi lako within a second na usipate msaada toka huko tulikotoka wanapata heshima yao ila kidogo tuliteleza juzi hapa naona wakongwe wamemshtua kua nahodha usicheze na wafanyabiashara chombo kitashindwa kutia nanga bandari salama hapo ndio inabidi turudi tuwapambe kwa nyimbo na vigelegele na ndio maana tulisema hapa tutarudi kuwasafisha na tukubali tu sisi saizi yetu watumishi wa umma hawa hata makofi tutapiga hawana pa-kwenda ila wafanyabiashara ndio pumping machine ya damu kwa uchumi wetu.
kweli kabisa,mfanyabiashara yuko mbele ya serikali
 
Kwa Mwaka jana tu Viwanda vyake vya Soft drink kwa Mujibu wa risala aliyosomewa kwa Rais na Mtoto wa Bakhresa ni kuwa wamelipa kodi jumla ya Tsh. 50 Billion!
 
Watu wengi na viongozi wao huwa wanaongea kwa mihemuko Juu ya mambo wasiyoyajua wala kuyafanyia utafiti. Bhackresa na makampuni mengine mengi ya watanzania wazalendo waliitwa wakwepa kodi kipindi kile cha taharifa ya sakata la upotevu makontena bandarini. Mamlaka ya Bandari TPA walitaka kuwaangushia jumba BOVU makampuni ya uwakala wa forodha Kama njia ya Kujitetea kwao. Hapo ndipo majina mabaya ya kila Aina yalipotolewa. Watu wakiwa hawajui kinachoendelea wakadandia Tren lile na kushambulia kwa Maneno kila mdau WA Tasnia nzima ya uwakala wa Forodha. Sifa Mbaya zikavuma ndani na nje ya nchi watu tuliokuwa tunawahudumia wakapoteza imani nasi na pia wakapoteza imani na Bandari yetu matokeo yake woote tumeyaona. Sasa leo hii Waungwana walewale Hawaii kinyaa hata Kidogo wanayaramba matapishi yao. Hii Ndiyo Tanzania yetu nchi inayoongoza kwa ukurupukaji.
 
Back
Top Bottom