Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Ila jamani wanaume wanaroho ngumu!!!!!! Nilimwambia tulock tu milango tujifungie tusubiri hatma yetu kama watakuja kuvunja vioo watukute ndani. Alinijibu kwa ukali "Sifi kiboya" yaani hizo discussion fupi zilifanyika kama tunaugomvi maana mi nilishapaniki... acheni jamani uwii
HUYo jamaa yako kama sio jambazi, basi alishatekwa mara kibao, kwa hio anajua
 
Mimi kwangu ilikuwa tofauti kidogo kibao kilinigeukia, ilikuwa mwezi wa 12 wiki moja kabla shule hazijafunguliwa hivo inabidi nijiandae kununua vifaa vya shule, asubuhi mzee akaniachia hela nikanunue vitu kariakoo..
Nilitegea mida ya saa 8 hivi nikatupia T-shirt na kipensi kifupi wenyewe wanaviita vinjunga chini na sendo nahisi hii ndo iliniletea madhara. Nikafika kkoo nikakusanya kinachonihusu na begi langu mgongoni nikagombania daladala nikafanikiwa kupata siti mwisho kule,
Kutulia navuta pumzi akaibuka jamaa ana asili ya uarabu akadai ameibiwa simu mimi sina wasiwasi najua litapita then tutasepa,
Konda akasema aliyechukua simu arudishe tuendelee na safari kila mtu kimya jamaa akasema alichukua namjua direct akaja kwangu nilishtuka aiseee ukizingatia sina hizo mishe kila mtu analalamika mrudishie simu yake bana tuondoke,
Nikapigwa kibao kizito na mzee mmoja hivi jirani yangu nikaambiwa toa simu walivyoona nawaletea kiwingu wakazama mifukoni kunisachi mwengie akachukua begi akamwaga vitu vyote chini ..wakanivua adi shati ikaonekana sina jamaa aliyeibiwa akashuka chini akasema atakachonifanya sitokaa nisahau nikasema Mungu ndo anaejua kama nimeiba au sijaiba,
Dereva akaondoa gari..gari imetoka pale kumbe simu ilianguka pale mlangoni kwa konda kwa chini ndani kidogo ya uvungu wa gari kipindi tunagombania ..wamama wakaanza jamani sio vizuri mmedharirisha mtoto wa watu..dah niliumia sana omba hii kitu isikukute
Uyo mzee aliyekupa kibao si ndo ungeanza nae Sasa na wewe.
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums

Aroo hii balaa sana
 
Maaame huyo mzee alie kupaa banzi c ungezaa nae aisee
 
Hahahaha asee nimecheka Sana🤣
 
Hakuna kitu kinaitwa mkanda wa Shaolin dunia hii, sanasana Kuna kitu kinaitwa Martial arts ambalo humo Kuna Goju Ryu, Shotokan, Aikido, Karate , Kungfu, Jujitsu, Aikido, Hapkido, Capoeira, Krav Maga etc.

Mkuu nimeshafanya yale mawasiliano
 
Umesahau kuwa kungfu ina variants zake

Naomba nikumbushe kungfu ambazo zinafundisha na jinsi ya kutumia daggers na majambia

Hakuna kitu kinaitwa mkanda wa Shaolin dunia hii, sanasana Kuna kitu kinaitwa Martial arts ambalo humo Kuna Goju Ryu, Shotokan, Aikido, Karate , Kungfu, Jujitsu, Aikido, Hapkido, Capoeira, Krav Maga etc.
 
Mkuu tusimulie matukio mengine ukiachana na lile la ufuta
Mkuu mimi nlikutana na visa kama 4,5 hivi
Ila moja ambayo naona ilikuwa kubwa kuliko
Ni ile miaka ya 2003 nilienda na jamaa nairobi
Tulipeleka mitkasi fulani kufanya biashara
Tukafika vizuri kesho yake tukaenda kuonana
Na boss kibiashara nakumbuka tulipeleka mawe aina ya rhodelite kweli biashara ikaenda poa tukachkua hela tukaondoka zetu,kurudi mahali tulipo fikia usiku tukashanga tunavamiwa na watu wnaojifanya maskari wakatupukutisha
Kila kitu wakatuacha bila hela,basi ikabidi tufanye mchakato wa kurudi kwa kuungaunga
Ila tulichokuja gundua ile ofisi ilikuwa siyo jamaa pale ndiyo style zao za kimafia

LAKINI SIKU ZOTE NASEMA MJINGA SIKU ZOTE NI WAKATI WA KWENDA ILA KURUDI
TAYARI ASHAKUWA MASTER

ova
 
Mimi niliwahi toka 2003 umoja sekondari nilitoka fanya interview yakuingia pale form two wakat wa kurud singida nikapanda mohamed trans ya bukoba nikaenda kukaa siti moja na bibi mmoja bhas zima wanaongea kihaya kabla ya kupanda sekenke pale bas zilikuwa zinasimama kwanza yule bibi kumbe anakunywa konyag zile za packt za kipindi kile tumerud tunapanda mlima kumbe bibi kashaanza kuongea mimi mwizi muda tu sema kwa kihaya sielewi kidogo akaanza piga kelele kwenye zile bhas kipindi kile kulikuwa na askar wawili wa escort akaja mmoja akanisach kabeg kangu na maswali mengi akanichukua nikakaa kwenye boneti mpk singda km mwizi iliniuma sanaa na sitasahau
 
Hahahahahahahha noma sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom