Fohadi
JF-Expert Member
- Jul 24, 2020
- 770
- 2,406
Mwaka 2006 hadi 2011 ni kipindi ambacho kama familia hatukuwahi kuwa na furaha ya kudumu. Dada yetu ambae ndie first born wa familia alikuwa anaumwa ugonjwa ambao haukuwa wa kawaida. Familia ilijitahidi kumtafutia tiba, pesa nyingi zilitumika na pengine matatizo ya dada ndiyo yaliyofanya familia yetu ikawa nyuma kimaendeleo kwani gharama nyingi sana sana zilitumika.
Katika kuhangaika huku na huku, familia ilifanikiwa kukutana na 'mtaalamu' mmoja wa jadi. Na katika harakati zake za kimatibabu, ilibidi kwa kutumia ujuzi wake aweze kuwaita wachawi ili wapate kuzungumza na baadhi ya member wa familia ili kujua tatizo ni nini na kwanini wameiandama sana familia yetu. Siku ya siku ikafika, kikao kikapangwa kufanyika usiku eneo la nje kidogo na nyumbani.
Nakumbuka kipindi hicho mzee alikuwa amesafiri nje ya mkoa. Hivyo mimi nikiwa kama mtoto wa kwanza wa kiume katika familia pamoja na Mama ndio tuliotakiwa kushiriki kwenye hicho kikao. Sikuwa na hofu wala kidogo maana kwa miaka 4 tayari mauza uza ya nguvu za giza nilikuwa 'nimeyazoea'. Na kweli, usiku ulifika, nikiwa mimi, mama yangu, mtalaamu wa jadi na watu wengine wawili tulikuwa tayari kwa kikao kile dhidi ya wachawi wale ambao wangeingia mda wowote. Tulipakwa dawa fulani usoni na kusubiri kikao.
Mtaalamu alianza kufanya yake na kuanza kuwaita wale wachawi na mara ghafla tukiwa tumekaa ndani ya hiyo nyumba ambapo kikao kilipangwa kufanyikia, waliingia watu watatu wakiwa kama walivyozaliwa wakiwa wamejipaka dawa nyeupe usoni.
Nakumbuka alikuwa Mwanamme mmoja mzee mnene ambae ndie alikuwa kiongozi wao na wanawake wawili wenye umri wa kama miaka 40's. Wale jamaa walikuwa wakali sana kwanini wameitwa. Mama yangu alikuwa anatetemeka kupita kiasi. Mmoja kati ya wale watu tuliokuwa nao alikuwa analia na wale wachawi walimkanya anyamaze mara moja.
Hakika ulikuwa ni usiku wa kutisha sana, wachawi waliokuja walikuwa watatu na walidai kuwa mshirika mwenzao ambae ndie mtesi wa familia yetu alikuwepo pale nje amekuja ila hakutaka kuingia ndani. Kikao kilichukua kama dakika 20 hivi na wale jamaa wakaomba kuondoka, hawana muda wa kupoteza wanawahi kuendelea na ratiba zao zingine usiku ule.
Sitasahau usiku ule, dunia imejaa watu makatili sana. Hatuna budi kumshukuru Mungu kama familia zetu zina furaha na amani. Binafsi namshukuru sana Mungu kwani mambo mengi leo yamebaki historia.