Kama umewahi kupigwa "changa" na matangazo ya ajira, tukutane hapa

Mohamedmteleke

Senior Member
Mar 21, 2019
137
171
Mwaka mmoja baada ya kuimaliza kidato cha sita, nilirudi nyumbani kuona hali inaendaje. Ups and downs zilipita za kutosha, hatimaye Mwananchi Communication Limited wakatangaza kuwa kampuni ya ATY kutoka Mafinga ina ajira. Maelezo kiasi na malipo ni mazuri, niende na chakula tu na chakula changu, wao watanipa chumba.

Basi, nikanunua godoro dogo la mwanafunzi, blanketi, na kubeba maskani. Nikaenda na pokey money kama 30,000 hivi. Nkakutana na mchizi wangu wa utotoni tukajaa Mafinga na tukafika headquarters kinyanambo, jirani na kituo cha mafuta cha CF. Bwana picha likaanzia pale, niliona wanawake wengi wakichonga vijiti kutoka kwenye miti ya mianzi.

Tukasajiriwa pale, lakini nilianza kushtuka baada ya kuona watu kutoka sehemu mbali mbali kama Dar es Salaam na Morogoro wakisajiliwa. Kama saa mbili usiku hivi tukakwea kwenye gari moja lenye moshi, tulipoipata, tukaacha Mafinga na kuanza kutafuta Wamimbarwe. Ni mbali kidogo ila usafiri uliichosha safari. Hadi hapo sijui naenda kufanya kazi gani.

Basi ikapiga mvua, mimi na wenzangu tulifunika vitanda vyetu, ikakata na tukakauka. Mishale kama ya saa 7 usiku tukaingia Wamimbarwe ambapo mbele kidogo kulikuwa na hilo camp lenyewe. Saa saba na nusu hivi tukaingia camp.

Ebwana sio poa, kwa mara ya kwanza niliona nyumba kubwa na majengo mengi kuliko shule, lakini yote ni made by mabanzi. Tukapewa vyumba na wanangu tisa, huo ni utaratibu wa kuangalia vitanda. Ooh, kucheck hivyo wanafunzi wana wenzangu na wengine hata shuka hawana! Imagine baridi ya Mafinga na ilikuwa inakaribia saa tano hapo.

Tukakutana na kitanda futi nane kwa nane kwa makadirio, dabo deka, daah mabanzi upande wa mgongo ndio yapo juu, na ndio unalalia hiyo. Sijui niite kichanja au niite kitanda.

Sikupata usingizi aisee, kama mida ya saa kumi na moja niliamka. Hapo bado sijui ni kazi gani na kila mtu hajui kudadek. Nkaamka na masela kadhaa ambao tuliripoti wote siku hiyo. Tukajaa nje, tukaona Mafinga kama mia hivi, yote kwa pamoja yakiwa yamewaka na kumetengwa vitu, japo asilimia kubwa Mafinga yalitengwa maharage. Tukaanza kuona vizuri mazingira ya pale, lilikuwa na mabweni sita na nyumba moja ya kisasa, bafu na vyoo vya kisasa, zizi lenye ng'ombe mmoja, duka na banda moja la chipsi, sehemu ya kuangalia TV na Samsung TV ya kama nchi Zaidi ya 57 hivi, vyote hivyo vilikuwa ndani ya fence ya mabanzi na ukubwa wa eneo zima ni kama mita 100 kwa 200 hivi. Nje ya fence kulikuwa na uwanja wa mpira na gari moja, na mapipa kama mia moja hivi yote yakiwa yameganda vitu kama lami hivi.

Ilipofika saa moja tukakabidhiwa kwa team leader na hapo ndipo akaanza kutuelekeza kazi ya kufanya huko. Tulitoka camp kuelekea msituni, misitu ilikuwa ya mipaina na imepangiliwa vema kwa mfumo wa grid reference, yaani kulikuwa na c1 hadi c12 na kila c ilikuwa na plot kadhaa. Tukatembea kama dakika 70 hivi hadi c10. Tulipewa visu flani vina teknolojia ya kipekee sana na ni vikali kupindukia.

Kumbe mchongo sio mchongo, bali mchongoma. Kazi ni kugema utomvu wa miti hiyo, utomvu huo ni mafuta ambayo hutumika kutengeneza rangi, vanish, na bidhaa nyingine zinazofanana. Kampuni ipo chini ya Wachina flani. Nkahisi kazi ni ngumu na maskan nimeacha mchongo simpoo wa kupata kipato sawa kabisa. Kwa mwezi ukikomaa pale unapata zaidi ya 250,000.

Ilibidi nisaze tu kwanza nikirudi nitaonekana mlaini. Basi mimi na mshkaj wangu tukapewa plot yenye miti 2000 na baadaye pekeeangu nikaongeza miti 1000. Sasa kazi ikaanza, kama mnavyojua kugema, kila siku lazima uchubue miti ili utomvu utoke na uingie kwenye kifuko tunaita PVC. Daah ilikuwa hatar, hadi kufika saa saba tukamaliza plot. Aisee msitu ni mkubwa kinyama yan. Aisee Saung Hill ni bonge la msitu. Nkawacheki wenzangu kwenye plot zao tukageuka.

Mbaya zaidi kila siku watu wanazidi kuja camp nao wanadanganywa kama mimi. Wengine wanamind na kusepa, wengine wanakomaa, wengine ni degree holders wengine lasaba. Kulikuwa na wasanii, mabaamed na wamasai pale, warembo pia walidanga pale. Yaani hakuna kitu utakachokosa. Kulikuwa na uwanja wa mpira japo hakukuwa flat ila tulipiga mpira kila jioni. Nlianaza kuridhika.

Siku moja nikiwa pale, kuna mwamba akatuletea mayai kutoka Silver Land Kampuni kwa sababu dada yake alikuwa anafanya kazi huko. Mayai yalikuwa adimu hivi pale, ilikuwa Ijumaa, lakini ilinipata allergy. Ngozi ikavimba na macho yakamezwa na ngozi ya uso. Huduma hakuna. Nkapewa salimia na mtu wa huduma ya kwanza, nikapoa. Usiku nikazidiwa. Asubuhi nikapata nafuu na nikatulia. Sikwenda msituni siku ile.

Jumamosi jioni nikazidiwa. Kuna jamaa akaninywesha na kunipaka mtishamba unaitwa Lwenye nikapoa. Saa mbili usiku nikazidiwa. Bahati nzuri, posho ikatoka siku ile, nikaandikiwa 60,000. Hii ilitokana na kazi niliokuwa nimefanya. Ilikuwa inaleta tumaini. Usiku nikazidiwa na ikabidi nisepe kuja mjini.

Bahati mbaya kulikuwa na gari moja tu, Noah, inayotoka kijijini Hadi Mafinga. Nauli ni shilingi 3,000. Gari iliondoka saa 11 alfajiri. Kwa hiyo, nililazimika kuenda kulala porini kutoka camp hadi porini. Nauli ya boda boda ni 15,000 kutoka camp. Ila kulikuwa na shortcut ya kuvuka mto, na mtoni maji yalijaa, lakini niliongea na watu wakanivusha. Baba alinipigia na kunituma 40,000.

Kufika camp nikala chakula cha buku na wakanipeleka kwa anayetoa huduma ya usafiri. Hapo ni saa nne unusu hivi. Jamaa alikuwa na chumba kimoja hakina chochote kile, hata bulb hakukuwepo. Nkachukua nguo kadhaa nzito nzito nikazimwaga chini, nikachukua blanketi nikatandika kisha nikajifunika.

Nikalala hadi asubuhi. Usingizi ule ulikuwa bora kuliko wa camp. Basi saa kumi na moja Noah ikaacha kijijini kuitafuta Mafinga. Niliposhuka tu garini nikaingia duka la dawa kujielezea kinagaubaga. Baada ya maelezo, nikaambiwa nitoa jero ili nipewe dawa.

Daah, hamuwezi amini, nilipona kwa tembe moja ya dawa. Allergy ilipata kisogo, dawa zikaanza kazi na ngozi ikajirudi kama mwanzo. Baba akanizuia kurudi kazini na mimi sikuwa na haja. Siku hiyo hiyo jioni nikatua uwanjani kitaa. Niliokuwa big nikarudi kimbau mbau af napiga mpira balaa kwa sababu bush nilikuwa napiga mechi kila siku.

Kwa hiyo, usipende kufanya kazi sehemu kabla hawajakuthibitishia usalama wako. Pia, serikali iangalie watu wanadanganywa na watu kuhusu ajira, kumbe sio. Pia, pale kazini hakukuwa na huduma wala usalama wa kazi. Misituni kulikuwa na chatu, ngiri, digidigi, na fisi kiasi. Pia, camp kulikuwa chafu na vuruboto sana. Kama kuna mtu anafanya kazi OSHA, aende kuwabana hawa Wachina, wananyanyasa sana raia huko porini na viwanda vya singboard.

Nimejifunza pia umuhimu wa kutambua kuwa unapotoka kutafuta fursa nje ya nyumbani, kuna watu kutoka maeneo mengine wanaokuja kufanya kazi katika eneo lako. Niliporudi kutoka likizo, nilikuta watu wengine walikuwa wameshachukua nafasi yangu na sikuijipatia tena. Picha iliyowekwa chini haikuwa na uhusiano na mkasa huu.

Malipo katika kazi hii yalitegemea uzalishaji wa pipa la gundi/utomvu. Mti mmoja ulihitaji kujazwa na lita moja ya utomvu, ambayo ilichukua kati ya wiki mbili hadi nne kujaza. Plot moja ilikuwa na miti elfu moja, na inaweza kutoa pipa nne. Kwa kufanya kazi kwa bidii, mtu angeweza kupata zaidi ya laki mbili kwa mwezi. Hata hivyo, wengi walikuwa wanapata tu shilingi 120,000 kwa mwezi, na posho zilikatwa mwishoni baada ya kuvuna gundi kwenye plot yako. Mtu aliyefanikiwa sana alikuwa amepata laki 680,000. Mimi binafsi sikuchukua malipo kwa sababu niliugua katika wiki mbili za mwanzo na sikutaka kurudi tena kwa sababu niliona kuwa si sahihi.

20220501_014949.jpg
 
Malipo ilikuwa ni kwa pipa la gundi/ utomvu...mti mmoja unakifuko Cha Lita moja,kinachukua wiki mbili had nne kujaza, plot moja Ina miti elfu moja, plot moja hutoa pipa nne ko ukipiga kazi inaweza pata laki mbili au Zaid , ila wengi walikuwa wakipata 120000 tu kwa mwezi , posho unakatwa mwishoni baada ya kuvuna gundi kwenye plot lako,...pia mtu aliefanikiwa saana alipiga laki 680000, Mimi sikuchukua malipo Kwan niliumwa katika wiki mbili za mwanzo na skutaka kurud Tena Kwan Ni uwaki niliona,
Mkuu MBNA haujasema malipo Yako?
 
Wewe hukupigwa changa ila ulishindwa kuendana na mazingira. Kuna watu wamepigwa pesa kwenye michakato ya ajira na vibarua, wengine wamepoteza nauli na muda na wanakuta empty
 
Malipo ilikuwa ni kwa pipa la gundi/ utomvu...mti mmoja unakifuko Cha Lita moja,kinachukua wiki mbili had nne kujaza, plot moja Ina miti elfu moja, plot moja hutoa pipa nne ko ukipiga kazi inaweza pata laki mbili au Zaid , ila wengi walikuwa wakipata 120000 tu kwa mwezi , posho unakatwa mwishoni baada ya kuvuna gundi kwenye plot lako,...pia mtu aliefanikiwa saana alipiga laki 680000, Mimi sikuchukua malipo Kwan niliumwa katika wiki mbili za mwanzo na skutaka kurud Tena Kwan Ni uwaki niliona,
Hilo tangazo analiloshika jamaa ni utapeli. Siku hizi yako mengi sana na watu wanalizwa kila siku. Ona umri wa waombaji ulivyoandikwa kijanja: miaka 18-70. Hii inawafanya wawe na pool/uwigo mkubwa ya watu wa kutapeli. Halafu hawaweki elimu wala ujuzi ili kila mtu anajione ana-qualify. Na malipo wanaweka kwa ujanja sh 10,000 kwa siku ili watu waone kama kuna ukweli kwani zamani walikuwa wanaweka figure kubwa mpaka watu wakawa wanajiuliza. Na mwisho sehemu wanasema tu ''Mbezi mwisho'' bila kutoa taarifa za kina. Ukiingia mkenge ukiwapigia simu wanakupa process na unajikuta unalipishwa ''malipo'' kidogo kama ada ya kitu fulani ili maombi yako yapitishwe.
 
Fala Sana Hawa watu....

Nawamind Sana sema watajaa kwenye ring tu
Hilo tangazo analiloshika jamaa ni utapeli. Siku hizi yako mengi sana na watu wanalizwa kila siku. Ona umri wa waombaji ulivyoandikwa kijanja: miaka 18-70. Hii inawafanya wawe na pool/uwigo mkubwa ya watu wa kutapeli. Halafu hawaweki elimu wala ujuzi ili kila mtu anajione ana-qualify. Na malipo wanaweka kwa ujanja sh 10,000 kwa siku ili watu waone kama kuna ukweli kwani zamani walikuwa wanaweka figure kubwa mpaka watu wakawa wanajiuliza. Na mwisho sehemu wanasema tu ''Mbezi mwisho'' bila kutoa taarifa za kina. Ukiingia mkenge ukiwapigia simu wanakupa process na unajikuta unalipishwa ''malipo'' kidogo kama ada ya kitu fulani ili maombi yako yapitishwe.
 
Back
Top Bottom