Tukutane hapa tuliopata ubaba kabla ya ndoa, ilikuwaje, ulichukua maaamuzi gani, ndie uliemuoa?

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Nakumbuka jioni ya siku kama ya leo kuelekea weekend nilimuita aje tuspend kwangu.

Mida kama hii nashangaa msosi naoukuta mezani sio kawaida yake kuniandalia akija, aliandaa juice nzito, pilau la nazi na njegere.

nimemaliza kula namsifu kwa mapishi yake ajiandae nae nimle, ndio akanifungukia "babe nikwambie kitu" nikamjibu awe huru, akaniambia "ila usichukie" mi nikajua ni hela na nilijua chakula kaandaa ili anilainishe kutoa pesa, nikamjibu tu awe huru "Sizioni siku zangu babe i think utakuwa daddy" tumbo ni kama lilizunguka kwa speed ya ajabu sana, mdomo upo wazi huku kichwani nikijiuliza maswali mengi sana kwa mpigo

hio siku sikuongea sana nilikuwa na mawazo, next day nilimpa laki 3 aende kuchomoa mimba, Why ? honestly nilipanga nijipigie tu na kusepa zangu, mimba haikuwa kwenye mipango wala kulea nae watoto, pia nilipata wasiwasi mtoto huenda nimebambikiziwa huyo kamkimbia.

Nilimbembeleza sana lakini aliikataa, akaj kujifungua na rasmi nikawa baba, kidogo angalau nilipoona mtoto ni copy yangu nikapunguza presha.

Ilibidi nimuoe awe wife na mama wa watoto wangu, kwa sasa tumeachana kuna kipindi upepo wa pesa ulinipitia zikamzuzua sana akajazwa upepo tuachane ili apate kitonga.
 
Mida kama hii nashangaa msosi naoukuta mezani sio kawaida yake kuniandalia akija, aliandaa juice nzito, pilau la nazi na njegere...
Kutoa mimba ni jambo baya sana, vipi ulienae sasa anampenda mwanao wa kwanza kwa huyo xwife? Au ndo anamuoneshea chuki wazi wazi?
 
Aiseé npo hapa single father niliyempata kijana wangu nikiwa na miaka 23 ,now ana miaka yake 8 alafu fresh tu na mama yake hata hatujuagi yupo nchi gan

Aiseé kulea damu Yako Raha sana ,wanaumee wenzangu msitelekeze watoto wenu au kumwachia mwanamke mtt wako .kuitwa dingi Ina Raha yake aiseee
 
Nakumbuka jioni ya siku kama ya leo kuelekea weekend nilimuita aje tuspend kwangu.

Mida kama hii nashangaa msosi naoukuta mezani sio kawaida yake kuniandalia akija, aliandaa juice nzito, pilau la nazi na njegere.

nimemaliza kula namsifu kwa mapishi yake ajiandae nae nimle, ndio akanifungukia "babe nikwambie kitu" nikamjibu awe huru, akaniambia "ila usichukie" mi nikajua ni hela na nilijua chakula kaandaa ili anilainishe kutoa pesa, nikamjibu tu awe huru "Sizioni siku zangu babe i think utakuwa daddy" tumbo ni kama lilizunguka kwa speed ya ajabu sana, mdomo upo wazi huku kichwani nikijiuliza maswali mengi sana kwa mpigo

hio siku sikuongea sana nilikuwa na mawazo, next day nilimpa laki 3 aende kuchomoa mimba, Why ? honestly nilipanga nijipigie tu na kusepa zangu, mimba haikuwa kwenye mipango wala kulea nae watoto, pia nilipata wasiwasi mtoto huenda nimebambikiziwa huyo kamkimbia.

Nilimbembeleza sana lakini aliikataa, akaj kujifungua na rasmi nikawa baba, kidogo angalau nilipoona mtoto ni copy yangu nikapunguza presha.

Ilibidi nimuoe awe wife na mama wa watoto wangu, kwa sasa tumeachana kuna kipindi upepo wa pesa ulinipitia zikamzuzua sana akajazwa upepo tuachane ili apate kitonga.
Laki tatu kutoa mimba?

Kuna mademu wakikujua watakuwa wanakwambia wana mimba zako kila mwezi!
 
Back
Top Bottom