TUKUNE KICHWA,kiswahili ndio mdudu gani?

proton pump

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
5,357
6,896
Kila kunapokucha kiswahili kinasisitizwa sana kiwe lugha ya kufundishia kuanzia la kwanza hadi chuo kikuu,

Hiki kiswahili kitakupeleka wapi? Ili hali hata masomo ya art yameshapuuzwa? Wanafunzi wanasisitizwa kusoma sayansi la hasha hicho kiswahili wapi tena sasa.

Licha ya hivyo ni mtoto wa nan mwenye hela anasoma shule za kiswahili?

Tuna bidhaa gani tunazozalisha ili kutangaza kiswahili nchi za nje?

Bunge la afrika mashariki lenyewe lazima watu watoe sera kwa kiingereza

Ni masomo gani ya shule za sekondari yanatolewa kwa kiswahili isipokua kiswahili chenyewe?

Licha hivyo watafanya transilation lkn utakuta mtu kaandika labda chloroquine, sulfuric utabaidilishaje kwa kiswahili? Na hao unao waandaa watapata wapi soko?

Nchi nyingine wanakienzi kiingereza japokua kiingireza si njia kuu ya maendeleo

Tungekienzi mda huo tungekuta masomo yote yapo kwa kiswahili Lkn hadi sasa msingi kiswahili sekondari kiingereza.

Kiswahili kimeandaliwa ili maskini aendelee kuwa maskini kwa maana hapo ni fumbo,watoto wa matajiri wanasoma shule za kiingireza.
 
Duuuh huu mjadala hadi leo haujapata ufumbuzi mkuu...ila kuna nchi zilizoendelea kutokana na lugha yao mfano China, ujerumani, Japan n.k
 
Wao walianza mapema sisi hii elimu tumeandaliwa na waliotutawala hata hiki kiswahili wazungu ndio walio kiandika itabidi tuendane na matokeo sisi tukitaka kuvuruga zaidi tubaidishe mfumo.
 
Kiswahili kikiachwa kama kilivyo kwa asili yake basi ni tayari kipo kisayansi na kimataifa.

Tatizo nikiona pale inapoachwa asili na fasili ya Kiswahili huko kilikotokea na kuanza kukisanifu kwa kuweka maneno mapya ya tasnifa ambayo hayana mvuto wala raha kuyatamka.
 
Kiingereza kimesababisha kuwa na wasomi wenye idadi kubwa ya vyeti isiyo uiana na uelewa wa wao kwani hujifunza kwa kukariri. Mtu anapojifunza kwa lugha mama huelewa zaidi na inaongeza nafasi ya kuwa mahili katika jambo ajifunzalo. Kinacho hitajika ni uhiyari na maandalizi ya kutosha kufanya mabadiliko katika sekta ya elimu, na TATAKI wamethubutu

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
 
Hapo umenena makinikia
 
mi wananichosha hawa viongozi wetu...wanasema tukienzi kiswahili lkn watoto wao wote wanawapeleka English medium
 
Kila kunapokucha kiswahili kinasisitizwa sana kiwe lugha ya kufundishia kuanzia la kwanza hadi chuo kikuu,

Hiki kiswahili kitakupeleka wapi? Ili hali hata masomo ya art yameshapuuzwa? Wanafunzi wanasisitizwa kusoma sayansi la hasha hicho kiswahili wapi tena sasa.

Licha ya hivyo ni mtoto wa nan mwenye hela anasoma shule za kiswahili?

Tuna bidhaa gani tunazozalisha ili kutangaza kiswahili nchi za nje?

Bunge la afrika mashariki lenyewe lazima watu watoe sera kwa kiingereza

Ni masomo gani ya shule za sekondari yanatolewa kwa kiswahili isipokua kiswahili chenyewe?

Licha hivyo watafanya transilation lkn utakuta mtu kaandika labda chloroquine, sulfuric utabaidilishaje kwa kiswahili? Na hao unao waandaa watapata wapi soko?

Nchi nyingine wanakienzi kiingereza japokua kiingireza si njia kuu ya maendeleo

Tungekienzi mda huo tungekuta masomo yote yapo kwa kiswahili Lkn hadi sasa msingi kiswahili sekondari kiingereza.

Kiswahili kimeandaliwa ili maskini aendelee kuwa maskini kwa maana hapo ni fumbo,watoto wa matajiri wanasoma shule za kiingireza.
Hapo ndipo tulipo chezewa akili na baba wa taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiingereza kimesababisha kuwa na wasomi wenye idadi kubwa ya vyeti isiyo uiana na uelewa wa wao kwani hujifunza kwa kukariri. Mtu anapojifunza kwa lugha mama huelewa zaidi na inaongeza nafasi ya kuwa mahili katika jambo ajifunzalo. Kinacho hitajika ni uhiyari na maandalizi ya kutosha kufanya mabadiliko katika sekta ya elimu, na TATAKI wamethubutu

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
Hahahaha
 
Back
Top Bottom