Tukumbushane ya Pugu Sekondari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukumbushane ya Pugu Sekondari

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by KAUMZA, Oct 30, 2011.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Si vibaya mtu ukikumbuka ulipotoka.

  Nakumbuka siku ya kwanza kukanyaga Pugu ilikuwa tarehe 5 mwezi februari. ilikuwa ni siku ya mapumziko (public holiday), siku ya kuzaliwa CCM(Kwa miaka hiyo tarehe ya kuzaliwa CCM ilikuwa inaadhimishwa kitaifa na inakuwa ni mapumziko).

  Nilipangiwa bweni la Maendeleo 2 na baada ya muda nilichaguliwa kuwa dom monitor. Kipindi kile pale Pugu mbele kidogo ya jiko kulikuwa na mradi wa nguruwe ambapo wanafunzi walikuwa wanawahudumia bila kujali wewe ni wa dini gani, mimi na wenzangu tulisimama kidete kupinga mradi ule hadi ukafutwa.

  Nakumbuka shida ya maji ya kunywa pale shuleni na ilikuwa inatupasa twende pondi ya mzee wa shamba kuchota maji na kuja kuyafungia katika makabati yetu maarufu kama lockers.

  Maisha ya bweni yalikuwa ni mazuri sana, ratiba ya chakula ilikuwa ni kama ifuatavyo: Tulikuwa tunakunywa uji saa 4, saa nane ugali maharage na usiku pia isipokuwa siku ya jumatano usiku ilikuwa ni siku ya wali maharage na alhamisi mchana tunapewa matunda(ndizi) na usiku wa alhamisi ni ugali kwa nyama(kipindi kile nyama tulikuwa tunaita kishoka).

  Vyoo vya Pugu maarufu kwa jina la bettle vilikuwa vina harufu kali sana na ilikuwa inatupasa tuvue mashati kabla ya kuingia vinginevyo utanuka mpaka bwenini/darasani kwa harufu.

  Pugu!!!!!!! nakumbuka mengi, walimu wangu akina Cobra "hilo ni jina la utani, jina lake halisi silikumbuki", mwl Charwe(huyu aliwahi kuninyang'anya viatu vyangu vya ngozi nilivyokuwa nimepewa na mzee wangu ambaye alikuwa ni afisa wa jeshi), mwl Juma Wasiwasi, Mwl Maliki, Mwl Shangwe, Mwl mukuru, marehemu mwl Swai, mabagala(sijui yupo wapi siku hizi), Mwl Mamilo, huyu alinikamata na "feki" la Physics NECTA na hatimae nikafutiwa matokeo yangu ya NECTA. Nimekumbuka sana shule yangu, ambayo imesaidia kujenga historia yangu.

  WANA PUGU, MNAKUMBUKA NINI PUGU!!!! LET'S SHARE
   
 2. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2013
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,498
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Hivi haya maneno DOCEBIT VOS OMNIA yanamaanisha nini? Yameandikwa kwenye ule ukuta una-oface parade ground, halafu kwa juu yake kuna picha ya Njiwa/Hua
   
 3. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2013
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kobra jina lake aliitwa Wajimira,namkumbuka mukuru aliyekuwa akituchezesha kwata uwanja wa mpira ,nakumbuka disko la welcome na graduations ,ruvu girls walikuwepo siku hiyo. Mr malick alikuwa mwalimu wa history ,mabagala kemia ,je wakumbuka uji ulikuwa ukinywewa kweny Tg na maboza? Je wamkumbuka mzee wa shamba aliyekuwa akituuzia mihogo? Je wakumbuka mashamba ya mihogo na minazi na je vipi zamu ya kuchunga ng'ombe . Pugu boys wazee wa ku drop wakati mwingine na vidumu vya kutafuta maji ya kunywa pale gongo la mboto mashine. Credit ziwaendee marehemu Mtera my only headmaster f1 to 4
   
 4. crome20

  crome20 JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2013
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Nusura nihailishe mwaka baada ya kuugua tyford kali wiki kabla ya mtihani. Paper ya Math na Pysics practical nikuwa naharisha vibaya hata matokeo hayakuwa mazuri, nikapiga E Mbili na C moja, sikuweza kwenda chuo direct, nimefurukuta tu baada ya kuingia mtaani. Nakumbumbuka WAJIMIRA(Cobra) alitupa adhabu ya kung'oa visiki kule majohe sababu ya kuchelewa kurudi toka likizo, jamaa alikuwa katili sana sijui yuko wapi siku hizi. Nakumbuka patashika siku ya kishoka, jamani maisha yale du sina hamu, na kibaya zaidi tulikuwa tunachanganywa na watoto wa form one basi patashika tupu.
   
 5. hoffman

  hoffman Senior Member

  #5
  Dec 6, 2013
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 131
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Pugu si mchezo, nakumbuka mabagala asubuhi asubuhi kama hujaenda assemble full kukimbizana, namkumbuka mama P muuza wali, R. I P mama P alifanikisha vya kustosha mimi kuishi Pugu. nakumbuka J3 siku ya nyama watu mapema sana wapo DH, ilikuwa kiambulia mchuzi kitu cha kawaida sana... nakumbuka Pond, nakumbuka battle... nakumbuka ili full kudrop kila ijumaa ikifika... Pugu imesaidia sana kuwa hapo nilipo..
   
 6. amani91

  amani91 Member

  #6
  Dec 7, 2013
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pugu nakumbuka vifuatavyo

  • Kudrop-maana yake kuondoka shuleni kwenda nyumbani bila ruhusa hiki kipindi mpaka naondoka form 4 mwaka 2010 kilikuwa bado kipo sana na kurudi shuleni ni Jumapili jioni sana au JumatatU asubuhi  • Mwalimu Ogesa(makamu mkuu wa shule) - Wanafunzi walipenda kuiga sauti yake sana na walimpondea mkanda wake kwamba hakuweza kuubadili tangu tunaingia form one mpaka tunaondoka form four.


  • Jeshi la wokovu walikuwepo waalimu wafuatao

  • Mwero[mkuu]
  • Ogesa[msaidizi]
  • Nampanda
  • Angelo
  • Magari
  • Senga[ndo jina la utani tangu nafika form one mpaka naondoka ckujua jina lake kamili]
  Kazi ya hili kundi nikuhakikisha kila mtu anaingia darasani sababu utoro ulikuwa umezidi sana yani baada ya break tu watu hawarudi tena darasani wenginewalilala sababu wametoboa wengine uvivu wameshiba maandazi ya mama Mainda au sambusa na chapati za mama Bonge au maandazi ya mama Maqantity walienda Gongo la mboto ,Mwisho wa lami wengine walienda kwenye tarehe zao  • Mwalimu Magari ni mwalimu wa malezi alikuwa mahahrufu wa kukariri visogo vya watu yani mtu akimuona anakimbia huku akiwa ameficha kichogo badala ya uso sababu alikuwa akiona kichogo bhasi tena ashakujua alikuwa mwalimu wa kipekee sana lakini kabla sijaondoka pale Pugu alienda kuwa mkuu wa shule ya O level ya jirani na Pugu
  • Vurugu za machungwa hapa siku kama sijakosea ilikuwa siku za ugali pia Vurugu za mikate iliyokuwa wanagawa siku za ugali pia ila saa nne ndo walikuwa wagawana mikate midogo super Loaf 5 kwa 25 boys hapa kama hauko chap unaambulia patupu nilikuwa mmoja wao walio ongoza kwa kukosa mikate  • Kuzamia madish ya watu au Table leader anapochukua dish nakuelekea sehemu ambayo watu hawaijui kisha watu wanamis na kwenda kuzamia kwa madish ya watu wengine sanasana siku za wali na nyama watu walitumia majina kupewa msosi na table leader sababu siku ya J3,J5,Jmoc ni wali Ijumaa ni nyama zilikuwa zinazua hadi ngumi beef nzito matusi ya nguoni na hadi kufichuliana siri coz ya hasira ya kumisishwa msosi.


  • Docebit vos Omnia -- Nilimuuliza head master Mr.Mwero akanijibu ni UJIO WA KRISTO YULE NJIWA NDO KRISTO NDO MAANA ANAKUWA ANAPAA KUELEKEA CHINI TOKEA JUU.
  :peace::love::love::love:
   
 7. Quicklime

  Quicklime Senior Member

  #7
  Jun 15, 2015
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Jamani wakuu nataka kujua tarafa na kata inapopatika shule ya sekondary ya Pugu
   
 8. e

  ejogo JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2016
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35


  Docebit vos Omnia = He will teach you everything
   
 9. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2016
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Boza ,container ya plastic ilitumika kunywea uji,TG, ni kikombe na bakuli zilizotumika kulia chakula na kunywea uji, mzee wa shamba ni mzee aliyekuwa maarufu kuuza mihogo, kobra ni mwalimu maarufu aliyekuwa akifundisha physics na alikuwa mwalimu wa malezi
   
 10. Nassib Sanga

  Nassib Sanga Senior Member

  #10
  Feb 25, 2016
  Joined: Aug 11, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Nakumbuka siku ya kwanza nimeenda kureport form one Pugu baada ya kupatiwa bweni lilikuwa Umoja 2 ile kufika bwenini tu nikaenda chooni kulia. Nilimwaga sana machozi lakini nashukuru nikaja kuzoea shule.. Mwenyeji hadi wa pondi
   
 11. Nassib Sanga

  Nassib Sanga Senior Member

  #11
  Feb 25, 2016
  Joined: Aug 11, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Daaah umenikumbusha mbali sana kaka.
   
 12. k

  kabunda88 JF-Expert Member

  #12
  Feb 25, 2016
  Joined: Nov 8, 2015
  Messages: 2,303
  Likes Received: 1,439
  Trophy Points: 280
  Nawakumbuka sana teachers wa chemistry Shrondinga jina lake kimili nimelisahau alikuwa mzur sana kwenye organic chemistry
  Kiberit..huyu alikuwa mzee daaa kwa practical za chemistry alikuwa njema sana na tulielewana sana maswali ya chemistry nilikuwa nayo niliyasolve yote kwa msaada wake kwahyo students ilikuwa lazma anione akitaka solution za practical aliwaelekeza waje kwangu
  Anjelo..mtaalam wa physical chemistry nilifanya mitihan ming kwake
   
 13. k

  kabunda88 JF-Expert Member

  #13
  Feb 25, 2016
  Joined: Nov 8, 2015
  Messages: 2,303
  Likes Received: 1,439
  Trophy Points: 280
  Nilikaa bweni la Maendeleo1 na walemavu kulikuwa na chumba cha stafu pale niliwazoea sana wakina KAPETO,,,Edo boy
  Bwen la walemavu weng walikuwa wanalitenga flan hv na kuwaogopa
   
 14. U

  Umuhirindahu JF-Expert Member

  #14
  Feb 25, 2016
  Joined: Feb 2, 2014
  Messages: 344
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  bad news,head master wetu mwlm Mtera kumbe ni marehemu? alifariki mwaka gani? Mungu amlaze mahali pema peponi.
   
 15. U

  Umuhirindahu JF-Expert Member

  #15
  Feb 25, 2016
  Joined: Feb 2, 2014
  Messages: 344
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Mwlm Mkandawile aka "madam" mwalimu wa chemistry enzi zenu hakuwepo?
   
 16. U

  Umuhirindahu JF-Expert Member

  #16
  Feb 25, 2016
  Joined: Feb 2, 2014
  Messages: 344
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Mimi nakumbuka sana "battle" nilikuwa naishi "Mapinduzi ",,,nakumbuka pia maisha ya pond,,maisha ya kubeba maji ya kunywa kwenye kidum cha lita tano....zaidi ya yote naikumbuka sana shule yangu Pugu high school ilinilea vizuri sana...wako wapi mkali wa hesabu mwlm Aradai,mkali wa physics mwlm Sarawati?
   
 17. k

  kabunda88 JF-Expert Member

  #17
  Feb 25, 2016
  Joined: Nov 8, 2015
  Messages: 2,303
  Likes Received: 1,439
  Trophy Points: 280
  Nilimsikia tu hakutufundsha sis
   
 18. k

  kabunda88 JF-Expert Member

  #18
  Feb 25, 2016
  Joined: Nov 8, 2015
  Messages: 2,303
  Likes Received: 1,439
  Trophy Points: 280
  Nimeimc Jid,,hahahahahaha harakat nyng tulfanya pale
   
 19. R

  Rollin riy Member

  #19
  Feb 25, 2016
  Joined: Aug 14, 2015
  Messages: 21
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 5
  nimeimis pugu mm kipindi niko pale nilifanikiwa kulala mabweni yote..
   
 20. Newfame

  Newfame JF-Expert Member

  #20
  Feb 25, 2016
  Joined: Feb 27, 2015
  Messages: 377
  Likes Received: 879
  Trophy Points: 180
  Mwl Sarawati mkali wa physics alihamishiwa Ifunda Tech
   
Loading...