Tukumbushane ujinga tuloufanya pindi tukiwa watoto

Tukumbushane ujinga tuloufanya pindi tukiwa watoto

du mi nilikuwa kikojozi balaaaa, mara mbili usiku mmjo!
 
kombolera nilipenda sana., hasa ule wakati wa mimi na Mama watoto tuko chumbani heheh hatari kweli.
 
Mm nilikuwa nachimbia hela chini kwenye udongo ndo ilikuwa kama saving yangu haah

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hakuna ujinga niliopitia sema tumepitia michezo mbali mbali kama kupinga mputo, cha mkononi, Bing'oa ,cha kuku, kula mbakishie baba pamoja na michezo mingine ya kuchangamsha kama vile ukuti,Kioo,msusi etc.
Michezo hii haipo tena kwa hiki kizazi cha dot.com Krapka Davinoooooooo!!!!!!
 
nilikuwa nikioga tayari mara watt wenzangu wataleta mpira ili 2cheze ss miguu ikichafuka ili nisigombezwe nilikuwa nanawa miguu kwa kutumia mate
 
Kuwachungulia mtoni mabinti wakioga
Kukunja mgumu kwenye paja na kutengeneza umbo la K
Kuwawekea mabinti kioo chini ili kuwachungulia
Kupiga chabo
Kupiganisha kuku
Kununulia vitumbua sadaka
 
nikiiba 50 ya kununulia kachori shuleni naificha kwenye soks
 
Duh
Kweli nyi mmepita makuzi mbali mbali na michezo mbali mbali ya utotoni. Mwanangu ye sasa hivi utoto wake anachezea Blackberry, anachat JF, gemu zake zote ni PS3 hata kombolela halijui. Daaaaah.
Hili ni tatizo au ndo mda umeenda na teknohama imechukua nafasi yake?
 
Back
Top Bottom