Tukumbushane! Mwongozo wa utoaji wa vibali vya ujenzi na usimamizi wa ujenzi wa majengo kwenye mamlaka za serikali za mitaa

Elisha Sarikiel

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
889
1,515
TAMKO LA WAZIRI WA NCHI NA KATIBU MKUU OFISI YA RAIS -TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

Walengwa wa Mwongozo huu ni Mamlaka za Serikali za Mitaa, Taasisi mbalimbali za Serikali zinazoshughulika na Ujenzi wa majengo, waendelezaji, wawekezaji wa ndani na nje pamoja, wananchi na wadau wengine katika sekta ya Ujenzi wa majengo.

Tamko la Mwongozo huu umezingatia kutoa maelekezo kuhusu utoaji wa Vibali vya Ujenzi wa majengo na usimamizi wa ukaguzi wa hatua zote za ujenzi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa. Taratibu hizo zimekuwa zikifanyika bila ya kuzingatia Mipango ya Jumla ya Uendelezaji (General Planning Schemes), Mipango ya Kina (Detailed Planning Schemes) na Mipango ya Matumizi ya Ardhi Vijijini. Hata hivyo, Miji na Vijiji vingi havina mipango ya matumizi ya ardhi ambapo husababisha Ujenzi wa majengo kufanyika bila ya kizingatia viwango na ubora unaokubalika ki-Sheria.


MUHIMU KUFUNGUA PDF NILIYOAMBATANISHA YENYE KURASA 50 KUSOMA YALIYOMO KAMA YAFUATAYO:

UTANGULIZI............................................................................................................................. 1

Lengo la Mwongozo.................................................................................................................... 1

Walengwa wa Mwongozo............................................................................................................ 2

Matokeo ya kuwepo kwa Mwongozo............................................................................................


Fursa Changamoto..................................................................................................................... 3

Utoaji wa Vibali vya Ujenzi............................................................................................. 3

Usimamizi na ukaguzi wa Ujenzi wa majengo................................................................. 5

3.0 SERA, SHERIA, KANUNI NA MIONGOZO.......................................................................... 6

3.2 SHERIA, KANUNI NA MIONGOZO...................................................................................... 8

Utaratibu wa kutoa Vibali vya Ujenzi....................................................................................... 12

Maelekezo ya kutekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa............................................ 12

1.2 Maombi ya Vibali vya Ujenzi.......................................................................................... 15

Ukaguzi wa awali wa michoro ya majengo.................................................................... 15

Malipo ya Ada za Ukaguzi wa Michoro, Ramani na Ada za Vibali vya Ujenzi.............. 17

Uandaaji wa Michoro ya Majengo................................................................................. 17

Wataalamu watakaochunguza/watakaokagua Michoro ya majengo na nyaraka........... 18

Utaratibu wa kuwataarifu waombaji wa Vibali vya Ujenzi........................................... 20

Vikao vya Timu ya kuidhinisha Vibali vya Ujenzi ambavyo vimekidhi vigezo................ 20

Utaratibu wa usimamizi wa ujenzi wa majengo.......................................................................... 21

Usimamizi wa Ujenzi wa Majengo ya Makazi ya kawaida............................................. 21

Usimamizi wa Ujenzi wa majengo ya ghorofa na majengo Makubwa........................... 21

Ukaguzi wa pamoja na Mikutano kwenye eneo la mradi /Ujenzi..................................... 22

Wahusika wa ukaguzi wa ujenzi wa majengo................................................................. 22

Masuala Muhimu ya kuzingatiwa kwenye usimamizi wa ujenzi wa majengo................. 23

Kutoa Cheti cha kutumia jengo (Certificate of Occupation)....................................................... 24

5.0 Mfumo wa Utawala wa utoaji wa Vibali Vya Ujenzi Mijini..................................................... 25

2 Kutoa Vibali vya Ujenzi kwa waombaji..................................................................................... 25

5.4 Muda wa kutoa Vibali vya Ujenzi.............................................................................................. 26

UDHIBITI NA URASIMISHAJI WA UJENZI HOLELA KWENYE VIJIJI NA MIJI MIDOGO INAYOCHIPUKIA ......... 27

Masharti ya utoaji Anwani za Makazi kwenye Vijiji na Miji Midogo Inayochipukia.................. 27

Urasimishaji na Uboreshaji wa Makazi holela.............................................................................. 28

Uandaaji wa Mipango ya kina ya Makazi Vijijini......................................................................... 29

Utawala wa Anwani za Makazi na Urasimishaji kwenye Miji Inayochipukia............................. 29

7.0 HITIMISHO............................................................................................................................... 31​

Kibali cha Ujenzi (Building Permit) ni nyaraka ya ki-Sheria inayotolewa na Mamlaka za Upangaji (Planning Authorities) ambazo ni Mamlaka za Serikali za Mitaa (The Local Government Authorities) ili kuruhusu Ujenzi mpya, kubomoa, kuondosha, kuongeza, au kufanya marekebisho makubwa. Kufanya hivyo kutasaidia kurekebisha kasoro zinazoweza kuathiri uimara wa jengo na mifumo mingine ya maji safi na taka, tahadhari za moto, umeme, usalama wa jamii na uharibifu au uchafuzi wa mazingira.

Mwongozo huu umezingatia kutoa maelekezo kuhusu utoaji wa Vibali vya Ujenzi wa majengo na usimamizi wa ukaguzi wa hatua zote za ujenzi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa. Taratibu hizo zimekuwa zikifanyika bila ya kuzingatia Mipango ya Jumla ya Uendelezaji (General Planning Schemes), Mipango ya Kina (Detailed Planning Schemes) na Mipango ya Matumizi ya Ardhi Vijijini. Hata hivyo, Miji na Vijiji vingi havina mipango ya matumizi ya ardhi ambapo husababisha Ujenzi wa majengo kufanyika bila ya kizingatia viwango na ubora unaokubalika ki-Sheria.

Mwongozo huu umeandaliwa ili kuondoa changamoto zilizopo kwenye utaratibu wa utoaji wa Vibali vya Ujenzi na usimamizi wa Ujenzi wa majengo.
Kwa mujibu wa Vifungu 124 na 125 vya Kanuni za Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) (Udhibiti Uendelezaji), Sura 288 (GN 242 ya mwaka 2008), Ujenzi wowote ndani ya Mamlaka za Upangaji ambazo ni Mamlaka za Miji Midogo, Halmashauri za Miji, Manispaa na Ma-jiji ni lazima upate kibali cha Ujenzi kutoka kwenye Mamlaka husika.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 35 (i) cha Sheria ya Mipangomiji Na. 8 ya mwaka 2007, Mamlaka ya Upangaji inatakiwa kutoa kibali cha Ujenzi katika kipindi kisichozidi siku 60 kuanzia tarehe mwombaji alipowasilisha maombi yake. Aidha, ndani ya muda huo mamlaka inatakiwa kumjulisha mwombaji kuwa amekubaliwa au amekataliwa ombi lake na kutaja sababu zilizopelekea ombi lake kukataliwa.

Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Kifungu 122(4) imezipa majukumu Mamlaka za Wilaya ya kutoa au kubadilisha majina, namba za barabara, mitaa na nyumba kama ilivyobainishwa kwenye Mwongozo wa Anwani za Makazi na Postikodi wa Agosti 2016. Kufanya hivyo, kutadhibiti uendelezaji holela wa Vijiji na Miji Midogo inayochipukia.

Mwongozo huu ukifuatwa kikamilifu, kwa kigezo cha kiashiria cha utoaji wa Vibali vya Ujenzi, utaboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa. Mamlaka hizo zinatakiwa kutoa Vibali vya Ujenzi ndani ya kipindi cha kati ya siku saba na mwezi mmoja. Pia, mwongozo utaboresha usimamizi wa ukaguzi wa Ujenzi wa majengo.

Jukumu la Ofisi ya Rais - TAMISEMI ni kusimamia utekelezaji wake kwa kushirikiana na Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa; Mwongozo huu usomwe kwenye vikao vya Baraza la Madiwani ili Waheshimiwa Madiwani wauelewe na kuusimamia kikamilifu kwenye maeneo yao; Mikoa iwasilishe taarifa za utekelezaji kila baada ya robo ya mwaka; na Mwongozo huu uanze kutumika rasmi kuanzia tarehe 01 Julai, 2018.

 

Attachments

  • Mwongozo wa Utoaji wa Vibali vya Ujenzi na Usimamizi wa Ujenzi wa Majengo kweny Mamlaka za Ser...pdf
    542.2 KB · Views: 143
Gharama za vibari vya ujenzi sh.ngapii
Gharama za kuomba kibali cha ujenzi inategemea Halmashauri husika unapoomba. Ni vema kuwasiliana nao !

Kila halmashauri imepanga gharama zake kulingana jengo unalotaka kujenga na pia kuna tofauti gharama kati ya jengo la makazi, Biashara na taasisi nk.
 
Vibali vya Ujenzi ni tabu mno kupata, Wakurugenzi na maafisa ardhi wanasumbua saana kupata vibali. Mie nimeomba kibali cha ujenzi tokea Mwaka jana mpk sasa hivi nazungushwa tu mpk nimekata tamaa.
 
Vibali vya Ujenzi ni tabu muno kupata Wakurugenzi na maafisa ardhi wanasumbua saana kupata vibali,mie nimeomba kibali cha ujenzi tokea Mwaka jana mpk sasa hivi nazungushwa tu mpk nimekata tamaa.

Si kweli, Labda enzi za JK ila kwasasa vibali vinatoka chap chap ni ufuatiliaji tu.
 
Vibali vya Ujenzi ni tabu muno kupata Wakurugenzi na maafisa ardhi wanasumbua saana kupata vibali,mie nimeomba kibali cha ujenzi tokea Mwaka jana mpk sasa hivi nazungushwa tu mpk nimekata tamaa.
Ni halmashauri ipi bado ina mchezo mchafu kwa sasa Tanzania ⁉️
 
Wanasumbua hata za mijini urasimu mtupu.

Ukienda unaambia afisa umpe shilingi 100,000 ya kuja kuona eneo, baada ya hapo hadithi na danadana Mpaka mwananchi unakata tama
 
Hebu naomba unipe procedures mkuu, kama unataka kujenga nyumba ya nakazia ya familia

Kiwanja hicho hapo, naanza na nini??

Thanks

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app

Simple tu, nazungumzia viwanja vilivyopimwa:-

1. Andaa michoro ya hiyo nyumba kama ya chini ni ramani moja ila kama ghorofa ni ramani mbili(icluding Structural), ramani (z)ipigwe mihuri.
2. Hakikisha haudawi kodi ya kiwanja.
3. Nenda Halmashauri husika, kajaze form ya kupata kibali cha ujenzi watakupa maelekezo, utaambatanisha hati ya kiwanja.
4. Utaenda kwa mtaalmu wa mipango miji atafanya calculation za kulipia,utaenda acountant watakupa control number utaenda kulipia Bank.
5. Ukishalipia utapewa mtu wa kwenda kuangalia site kama haina jengo lolote ,kama ulishajenga utapigwa fine ya 2% ,mtaalam atapeleka ripoti kwamba papo sawa.
6. Then unasubiri kibali tu baada ya process n0. 5, ni easy tu.

Estimation price ya kibarli ni around 200k - 250k kwa nyumba za kawaida na ghorofa around 500k - 1.2m nazungumzia za makazi maana bei inategemea na sqm za nyumba.
 
Mzee unasema ni easy tu sio Tanzania yote inategemea, Mie nilikua nataka kuwekeza nchini kwangu nimepeleka kila kitu mpk wameenda kukagua eneo lakini kibali sijapewa nazugushwa tu, nilikua nikaona wananichelewesha nikajenga store kubwa tu kwa ajili ya kuweka vifaa vyangu wakapiga X duu lakini nilichokuja kugudua ni baaada ya kujua kuwa naishi Europe sasa wanataka kupiga hela.wameona ramani ya campsite hatari sasa wanasumbua lkn nitajenga siku wao watakua hawana hivyo vyeo tena.
 
Haina u ishi, kuna halmashauri zinasumbua sana upatikanaji wa vibali vya ujenzi Kibaha mji mi moja wapo ...
 
nitajenga
Mzee unasema ni easy tu sio Tanzania yote inategemea ,Mie nilikua nataka kuwekeza nchini kwangu nimepeleka kila kitu mpk wameenda kukagua eneo lkn kibali sijapewe nazugushwa tu nilikua nikaona wananichelewesha nikajenga store kubwa tu kwa ajiri ya kuweka vifaa vyangu wakapiga X duu lkn nilichokuja kugudua ni baaada ya kujua kuwa naishi Europe sasa wanataka kupiga hela.wameona ramani ya campsite hatari sasa wanasumbua lkn nitajenga siku wao watakua hawana hivyo vyeo tena.
Mkuu vibali imekuwa ishu sana siku hizi. Nimepata tenda ya kumjengea client wangu nyumba ya floor moja Nipo nazunguka halmashauri ya Arusha karibu mwez sasa nimekamilisha kila kitu lakini wanagoma kutoa kibali boss kashaanza kukata tamaa na ujenzi kabisa. Kiukwel serekali yetu imekuwa sio rafiki kabisa katika hili. Walalahoi tunaotegemea tenda ndogondogo kama hizi ili maisha yaende tunakwamishwa Sana
 
Mkuu vibali imekuwa ishu sana siku hizi. Nimepata tenda ya kumjengea client wangu nyumba ya floor moja Nipo nazunguka halmashauri ya Arusha karibu mwez sasa nimekamilisha kila kitu lakini wanagoma kutoa kibali boss kashaanza kukata tamaa na ujenzi kabisa. Kiukwel serekali yetu imekuwa sio rafiki kabisa katika hili. Walalahoi tunaotegemea tenda ndogondogo kama hizi ili maisha yaende tunakwamishwa Sana
Ni kweli vibali imekuwa ishu...halmashauri ya jiji la mwanza naona wanaongoza kwa usumbufu,ukifika wanakuandalia mazingira ya rushwa,nimekata tamaa sasa nimeamua nitajenga bila kibali chochote.
 
Back
Top Bottom