Tukubali ukweli, Watanzania si watu wa kufanya maandamano. Tusitegemee miujiza

akilinene

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
514
433
Makamanda, tukubali ukweli kuwa pamoja na wito wa kuandamana kutolewa mara nyingi na viongozi wa CHADEMA, hakuna iliyofanikiwa. Tunajilisha upepo kufikiri kuwa tarehe 5 Agosti itakuwa tofauti.

Ni muhimu sasa tuwaambie viongozi wa CHADEMA waachane na mkakati huu ambao siku zote unashindwa. Kwanza viongozi wenywe hawaoneshi mfano.

Tumeanza kusikia Mwenyekiti wa BAVICHA akitangaza kuwa "Watakaoandamana watapigwa na IGP" ina maana yeye tayari ameshajitoa. Kwa mazingira haya tusitegemee kuona yeyote anaandamana. Hakuna miujiza.

Tuendelea kutumia key boards zetu.
 
Slaa alikiandamania chama cha Mbowe hadi akavunjwa mikono, Mbowe alifanya nini zaidi ya kumzunguka kwa vipande 30 vya fedha?

Siyo kwamba watanzania hawawezi kuandamana, lakini unaandamana kwa ajili ya nini? Mbowe? Mzee wa MIGA? Wanasiasa bana!
 
Ni muhimu sasa tuwaambie viongozi wa Chadema waachane na mkakati huu ambao siku zote unashindwa. Kwanza viongozi wenywe hawaoneshi mfano.
SIo Watu wa KUFANYA MAANDAMANO kwa Sababu Haki hiyo Wanaminywa na Watawala kinyume na SHERIA
 
Slaa alikiandamania chama cha Mbowe hadi akavunjwa mikono, Mbowe alifanya nini zaidi ya kumzunguka kwa vipande 30 vya fedha?

Siyo kwamba watanzania hawawezi kuandamana, lakini unaandamana kwa ajili ya nini? Mbowe? Mzee wa MIGA? Wanasiasa bana!
Well said
 
Na Slaa sasa hivi yuko wapi?

Amandla....
 
Kama sio watu wa kufanya maandamano kwa nini nguvu za ziada zinatumika kuhakikisha hawafanyi maandamano?

Amandla...
 
Makamanda, tukubali ukweli kuwa pamoja na wito wa kuandamana kutolewa mara nyingi na viongozi wa CHADEMA, hakuna iliyofanikiwa. Tunajilisha upepo kufikiri kuwa tarehe 5 Agosti itakuwa tofauti.

Ni muhimu sasa tuwaambie viongozi wa CHADEMA waachane na mkakati huu ambao siku zote unashindwa. Kwanza viongozi wenywe hawaoneshi mfano.

Tumeanza kusikia Mwenyekiti wa BAVICHA akitangaza kuwa "Watakaoandamana watapigwa na IGP" ina maana yeye tayari ameshajitoa. Kwa mazingira haya tusitegemee kuona yeyote anaandamana. Hakuna miujiza.

Tuendelea kutumia key boards zetu.

ID zile zile watu wale wale. Pori jipya nyani wale wale:

IMG_20210804_123444_062.jpg

Unaonaje kama hizi taarifa zako za kiintelijensia ungempelekea Sirro moja kwa moja akajielekeza zaidi kwenye kupambana na majambazi?
 
Hivi unajua ulichoandika kweli? Sidhani kama kichwani kuko sawa!
Kwani hujamwelewa? Yaani ni kwamba politics za chadema zimepwaya sana kiasi kwamba hamna mnachokisimamia na hamna watu wa kuwaandamania. Huku uraiani ukimwuliza mtu kwa nini upo chadema anakujibu katiba mpya. Seriously?
 
Back
Top Bottom