Lunyungu, Lunyungu
Ya kweli hayo??? ngoja nikaangalie ile suti yangu ya harusi labda panya wameionea aibu.
Ila nadhani endapo wengi walishiriki huko nyuma kuua yale mashirika ya umma na wapo ambao walishiriki kuiibia nchi halafu wakateuliwa kwa kuwa eti watabadilika, na kama endapo tutachanganywa nao hao hakika hakuna kazi itakayofanyika zaidi ya uwajibikaji wa pamoja.
Nashawishika kusema kuwa serikali itumie sana taarifa za Tume ya maadili ambapo naamini wana viapo vyao wale na watatoa taarifa sahihi za kila mteuliwa kuonesha rekodi yake na uchumi wake.
Nadhani sasa tuwageukie wakurugenzi na wakuu wa idara mbalimbali ambao wapo miaka nendarudi serikalini na wanafanya madudu ambayo yameigharimu serikali na taifa kwa jumla........ wasafishwe kwanza ndipo iundwe timu safi.
Baada ya ndugu Pinda kuingia madarakani ameamua kuwa na timu ya watu wake .Pinda na watu wake sasa yuko bize kupata majina ya wakuu wapya wa Mikoa na baadaye nadhani Wilaya. Habari ambazo nimeletewa muda huu na vilunyungu toka ndani ya ofisi ya waziri Mkuu ni kwamba Pinda kanuia kufanya kweli na anataka kwanza wakuu hao wapya. Baada ya siku chache majina yataenda mbele ya Mkuu wa kaya kwa baraka na kutangazwa. Huenda wakatoka hapa wana JF kwenda kusaidia kusafisha na si kuungana na Ufisadi .
Stay awake - JF inashika kasi.
Mimi habari hii imenifikia muda huu nami kwa kuwa comp yangu huzima saa nane usiku tu nikaona wacha nilete .Habari hizi zimetoka ndani kabisa watu wakiwa wana hahaha kutafuta connections.Nimeambiwa uteuzi wowote hawa angalii kigezo chochote bali ukipendwa unachukuliwa .Sasa zina ukweli kiasi gani ? Fungua macho na masikio nawe toka hapo ulipo ili sote tuanze kufuatilia hili .
Lakini nimesha penyeza zaidi vijana na by kesho ama kesho kutwa nitakupeni ukweli zaidi.Pamoja na haya naomba nyie mfanye kazi ya Ziada .
Ili uwapata watu wa maana na hasa walioko madarakani it is time now kuanza kujadili majina ya wakuu hawa.Kila mmoja na Mkoa wake ili kuona wamekuwa wakifanya nini tangia wamekuwa Wakuu na kama wana stahili kubakia .
Naanza nakuleta jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam .
Ndugu Abbas Kandoro.
In case of changes does he deserve to remain or he should go ?Mwenye data zake amwage na twenda Tanzania nzima tumsaidie PM Pinda kuwapindua .
Mkuu Lunyungu,
Nikisoma between the lines naona kama kuna kaharufu faulani kasikoeleweka ktk taarifa yako hii. Isije ikawa ndo serikali inakuja na mbinu nyingine ya kuwafahamu kirahisi wana JF ambao IP zao wamezihide. Nakusihi utuletee data kamili hapa kisha tuanze kujadili.
Haiwezekani mtu kuokotwa kokote kule kisha kupewa dhamana kubwa ktk serikali. Lazma kuna mkono fulani hapo. au ndo tuseme Pinda ameingia kazini rasmi?? Sintajitokeza hadharani. Najiunga na falsafa ya Mzee Mwanakijiji kuongea nyuma ya PAZiA.....
Kama kweli Pinda anataka kuonyesha uodari wake basi amshauri JK cheo cha Mkuu wa Mkoa kifutwe kwani hawana lolote la maan wanachokifanya. Kwanza vyeo vyote sijui mganga mkuu wa mkoa, PCCB mkoa, RSO, nk. vyote hamna kitu chochote wanafanya ni kula pesa ya walalahoi tu.
Mkuu Msanii
Hii forum kuna watu wanajulikana nayo na mimi sijawahi na siwezi kuwa kibaraka wa mtu yeyote hapa ama nje .I am real .Habari za ofisin kwa Pinda zinasema hakuna vigezo maalumu so inategemea unajulikana kuanzia wapi .Ndiyo maana nikasema huenda Msanii unaweza kulamba dume .
Hilo ndilo nimesikia na ninalisema lilivyo .Vigezo vya kuwa Mkuu wa Mkoa kwa Pinda sijalisikia .
Msanii, hapo mkuu umeongea maneno ambayo ndipo mzizi wa fitina ulipo wakurugenzi na wakuu wa idara..... yaani ukiangalia kuna mikurugenzi imekuwa kwenye mawizara huko miaka nenda rudi na kinachofanyika hakionekani... hujiulizi TCC, CRDB, TBL etc zimefanikiwa vipi na wale wakuu kule ni waTz kama mimi na wewe?!?! Kuna kitu kinaitwa REFORM ambacho tatizo ni kwamba serikali yetu tukufu haijajua kina maana gani.... Jamani reform sio kuweka new minister, total reform ni new PS, Directors and HODs ambao wao ndio wata drive the technical side ya wizara/idara zetu!!! Waziri apige gumzo siasani (duh si utani nadhani BAKITA hapo wamepata neno jipya) hawa nguvu na damu mupya wafanye majamboz!!!!!! Wakubwa mlione hili!!!
Mkuu Lunyungu,
Mimi nimeshakata na tiketi, nataka mkoa ulio nyuma kuliko yote na baada ya mwaka kama hakuna jipya basi niwe fired tena kwa kusulubiwa kwi kwi kwi!!!!
Hao jamaa hawawezi kutoa kazi kwa watu ambao hawatawapigia magoti. Wanataka watu ambao watatekeleza yale wanayoambiwa na wakubwa zao. Watu huru kama wengi hapa JF, hata siku moja hawawezi kufikiriwa!
Nalijua hii Mzee Mtanzania lakini wao katika kuchagua wanasema hawajali nini wala nini .So kaa mkao wa Kula unaweza kulamba Dume ukapelekwa Mtwara .
Mimi habari hii imenifikia muda huu nami kwa kuwa comp yangu huzima saa nane usiku tu nikaona wacha nilete .Habari hizi zimetoka ndani kabisa watu wakiwa wana hahaha kutafuta connections.Nimeambiwa uteuzi wowote hawa angalii kigezo chochote bali ukipendwa unachukuliwa .Sasa zina ukweli kiasi gani ? Fungua macho na masikio nawe toka hapo ulipo ili sote tuanze kufuatilia hili .
Lakini nimesha penyeza zaidi vijana na by kesho ama kesho kutwa nitakupeni ukweli zaidi.Pamoja na haya naomba nyie mfanye kazi ya Ziada .
Ili uwapata watu wa maana na hasa walioko madarakani it is time now kuanza kujadili majina ya wakuu hawa.Kila mmoja na Mkoa wake ili kuona wamekuwa wakifanya nini tangia wamekuwa Wakuu na kama wana stahili kubakia .
Naanza nakuleta jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam .
Ndugu Abbas Kandoro.
In case of changes does he deserve to remain or he should go ?Mwenye data zake amwage na twenda Tanzania nzima tumsaidie PM Pinda kuwapindua .
Lunyungu,
Tumefahamiana kwa siku nyingi mkuu katika masuala ya maisha kama haya tuweke tofauti pembeni pls kama una access huko penyeza jina langu I would prefer U-RC lakini kwa kuanzia hata U-DC sio mbaya
Kindly do the needful nakuamini