Tukio linalotegemewa tega masikio sasa

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Baada ya ndugu Pinda kuingia madarakani ameamua kuwa na timu ya watu wake .Pinda na watu wake sasa yuko bize kupata majina ya wakuu wapya wa Mikoa na baadaye nadhani Wilaya. Habari ambazo nimeletewa muda huu na vilunyungu toka ndani ya ofisi ya waziri Mkuu ni kwamba Pinda kanuia kufanya kweli na anataka kwanza wakuu hao wapya. Baada ya siku chache majina yataenda mbele ya Mkuu wa kaya kwa baraka na kutangazwa. Huenda wakatoka hapa wana JF kwenda kusaidia kusafisha na si kuungana na Ufisadi .
Stay awake - JF inashika kasi.
 
Saharavoice

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,606
1,941
Haya Mkuu Lunyungu, Let's hope siyo nyepesi nyepesi. na hao wajao wawe waadilifu kuliko hawa waliopo.
 
Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
12,537
9,377
Lunyungu, Lunyungu
Ya kweli hayo??? ngoja nikaangalie ile suti yangu ya harusi labda panya wameionea aibu.

Ila nadhani endapo wengi walishiriki huko nyuma kuua yale mashirika ya umma na wapo ambao walishiriki kuiibia nchi halafu wakateuliwa kwa kuwa eti watabadilika, na kama endapo tutachanganywa nao hao hakika hakuna kazi itakayofanyika zaidi ya uwajibikaji wa pamoja.

Nashawishika kusema kuwa serikali itumie sana taarifa za Tume ya maadili ambapo naamini wana viapo vyao wale na watatoa taarifa sahihi za kila mteuliwa kuonesha rekodi yake na uchumi wake.

Nadhani sasa tuwageukie wakurugenzi na wakuu wa idara mbalimbali ambao wapo miaka nendarudi serikalini na wanafanya madudu ambayo yameigharimu serikali na taifa kwa jumla........ wasafishwe kwanza ndipo iundwe timu safi.
 
Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
613
14
Mkuu Lunyungu, tutatega masikio manake unajua kwa hapa nchini ukiangalia veyo kama wakuu wa mikoa na wilaya ni kwa ajili ya watu wa karibu na wazee.... So inawezekana isiwe watendaji kweli bali kurudisha takrima kwa wale waliwapigia debe wakati wakiw kwenye mihangaiko ya ubunge au marafiki.....

I don't want to speculate but hili swala la wakuu wa mikoa, wilaya na in some cases kwa kweli hao wateuliwa muda mwingi ukiangalia ufanisi wao inakufanya mtu mzima ukae chini na kujiuliza vigezo vya kuwateua na most of the times unakuta ka connection pale na wazee!!!

Haya twangojea mchele uwanjani!!
 
Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
613
14
Lunyungu, Lunyungu
Ya kweli hayo??? ngoja nikaangalie ile suti yangu ya harusi labda panya wameionea aibu.

Ila nadhani endapo wengi walishiriki huko nyuma kuua yale mashirika ya umma na wapo ambao walishiriki kuiibia nchi halafu wakateuliwa kwa kuwa eti watabadilika, na kama endapo tutachanganywa nao hao hakika hakuna kazi itakayofanyika zaidi ya uwajibikaji wa pamoja.

Nashawishika kusema kuwa serikali itumie sana taarifa za Tume ya maadili ambapo naamini wana viapo vyao wale na watatoa taarifa sahihi za kila mteuliwa kuonesha rekodi yake na uchumi wake.

Nadhani sasa tuwageukie wakurugenzi na wakuu wa idara mbalimbali ambao wapo miaka nendarudi serikalini na wanafanya madudu ambayo yameigharimu serikali na taifa kwa jumla........ wasafishwe kwanza ndipo iundwe timu safi.

Msanii, hapo mkuu umeongea maneno ambayo ndipo mzizi wa fitina ulipo wakurugenzi na wakuu wa idara..... yaani ukiangalia kuna mikurugenzi imekuwa kwenye mawizara huko miaka nenda rudi na kinachofanyika hakionekani... hujiulizi TCC, CRDB, TBL etc zimefanikiwa vipi na wale wakuu kule ni waTz kama mimi na wewe?!?! Kuna kitu kinaitwa REFORM ambacho tatizo ni kwamba serikali yetu tukufu haijajua kina maana gani.... Jamani reform sio kuweka new minister, total reform ni new PS, Directors and HODs ambao wao ndio wata drive the technical side ya wizara/idara zetu!!! Waziri apige gumzo siasani (duh si utani nadhani BAKITA hapo wamepata neno jipya) hawa nguvu na damu mupya wafanye majamboz!!!!!! Wakubwa mlione hili!!!
 
Semanao

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
208
15
Baada ya ndugu Pinda kuingia madarakani ameamua kuwa na timu ya watu wake .Pinda na watu wake sasa yuko bize kupata majina ya wakuu wapya wa Mikoa na baadaye nadhani Wilaya. Habari ambazo nimeletewa muda huu na vilunyungu toka ndani ya ofisi ya waziri Mkuu ni kwamba Pinda kanuia kufanya kweli na anataka kwanza wakuu hao wapya. Baada ya siku chache majina yataenda mbele ya Mkuu wa kaya kwa baraka na kutangazwa. Huenda wakatoka hapa wana JF kwenda kusaidia kusafisha na si kuungana na Ufisadi .
Stay awake - JF inashika kasi.

Kama kweli Pinda anataka kuonyesha uodari wake basi amshauri JK cheo cha Mkuu wa Mkoa kifutwe kwani hawana lolote la maan wanachokifanya. Kwanza vyeo vyote sijui mganga mkuu wa mkoa, PCCB mkoa, RSO, nk. vyote hamna kitu chochote wanafanya ni kula pesa ya walalahoi tu.
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Mimi habari hii imenifikia muda huu nami kwa kuwa comp yangu huzima saa nane usiku tu nikaona wacha nilete .Habari hizi zimetoka ndani kabisa watu wakiwa wana hahaha kutafuta connections.Nimeambiwa uteuzi wowote hawa angalii kigezo chochote bali ukipendwa unachukuliwa .Sasa zina ukweli kiasi gani ? Fungua macho na masikio nawe toka hapo ulipo ili sote tuanze kufuatilia hili .

Lakini nimesha penyeza zaidi vijana na by kesho ama kesho kutwa nitakupeni ukweli zaidi.Pamoja na haya naomba nyie mfanye kazi ya Ziada .

Ili uwapata watu wa maana na hasa walioko madarakani it is time now kuanza kujadili majina ya wakuu hawa.Kila mmoja na Mkoa wake ili kuona wamekuwa wakifanya nini tangia wamekuwa Wakuu na kama wana stahili kubakia .

Naanza nakuleta jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam .
Ndugu Abbas Kandoro.

In case of changes does he deserve to remain or he should go ?Mwenye data zake amwage na twenda Tanzania nzima tumsaidie PM Pinda kuwapindua .
 
Mkuu Lunyungu,
Nikisoma between the lines naona kama kuna kaharufu faulani kasikoeleweka ktk taarifa yako hii. Isije ikawa ndo serikali inakuja na mbinu nyingine ya kuwafahamu kirahisi wana JF ambao IP zao wamezihide. Nakusihi utuletee data kamili hapa kisha tuanze kujadili.

Haiwezekani mtu kuokotwa kokote kule kisha kupewa dhamana kubwa ktk serikali. Lazma kuna mkono fulani hapo. au ndo tuseme Pinda ameingia kazini rasmi?? Sintajitokeza hadharani. Najiunga na falsafa ya Mzee Mwanakijiji kuongea nyuma ya PAZiA.....
 
Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,324
37
Semanao mchango muhim sana...Hivi vyeo havina maana ni kupoteza pesa za Nchi..Raisi AFUTE wakuu wa mikoa.abakishe tu wakuu wa Wilaya..same na hao hizo Taasisi zingine...
Hawa wakuu wa Wilaya wawe wanaripoti straight.. ..Ukiangalia sana hata hawa Wakuu wa Wilaya nao hawana mpango...waache madiwani na wabunge wafanye kazi zao na Kurugenzi zingine.

Muundo wa Serikali yetu una utitiri wa Uongozi USIOKUWA na TIJA

Pia no need ya kujadili hayo Majina ya wakuu wa Mikoa...ni wastage wa Time kwani Kigezo kikuu ni Matashi ya JK,PM na waliokaribu...
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Mkuu Lunyungu,
Nikisoma between the lines naona kama kuna kaharufu faulani kasikoeleweka ktk taarifa yako hii. Isije ikawa ndo serikali inakuja na mbinu nyingine ya kuwafahamu kirahisi wana JF ambao IP zao wamezihide. Nakusihi utuletee data kamili hapa kisha tuanze kujadili.

Haiwezekani mtu kuokotwa kokote kule kisha kupewa dhamana kubwa ktk serikali. Lazma kuna mkono fulani hapo. au ndo tuseme Pinda ameingia kazini rasmi?? Sintajitokeza hadharani. Najiunga na falsafa ya Mzee Mwanakijiji kuongea nyuma ya PAZiA.....

Mkuu Msanii
Hii forum kuna watu wanajulikana nayo na mimi sijawahi na siwezi kuwa kibaraka wa mtu yeyote hapa ama nje .I am real .Habari za ofisin kwa Pinda zinasema hakuna vigezo maalumu so inategemea unajulikana kuanzia wapi .Ndiyo maana nikasema huenda Msanii unaweza kulamba dume .Hilo ndilo nimesikia na ninalisema lilivyo .Vigezo vya kuwa Mkuu wa Mkoa kwa Pinda sijalisikia .

Na data zaidi nazitafuta na nitazileta lakini yeyote mwenye nazo tafadhali aweke tu hapa ndiyo maana tunaitwa JF.
 
DAR si LAMU

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
2,929
532
Kama kweli Pinda anataka kuonyesha uodari wake basi amshauri JK cheo cha Mkuu wa Mkoa kifutwe kwani hawana lolote la maan wanachokifanya. Kwanza vyeo vyote sijui mganga mkuu wa mkoa, PCCB mkoa, RSO, nk. vyote hamna kitu chochote wanafanya ni kula pesa ya walalahoi tu.

..wakifutwa kazi zao nani afanye? kwa namna gani hawafanyi chochote?

..jenga hoja!
 
DAR si LAMU

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
2,929
532
Mkuu Msanii
Hii forum kuna watu wanajulikana nayo na mimi sijawahi na siwezi kuwa kibaraka wa mtu yeyote hapa ama nje .I am real .Habari za ofisin kwa Pinda zinasema hakuna vigezo maalumu so inategemea unajulikana kuanzia wapi .Ndiyo maana nikasema huenda Msanii unaweza kulamba dume .

..duh,hii kali!
Hilo ndilo nimesikia na ninalisema lilivyo .Vigezo vya kuwa Mkuu wa Mkoa kwa Pinda sijalisikia .

..sema hujasikia vigezo ni vipi. lazima kuwe na vigezo,hata chama cha wahuni kuna vigezo vya kuwa member!
 
Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
12,537
9,377
Msanii, hapo mkuu umeongea maneno ambayo ndipo mzizi wa fitina ulipo wakurugenzi na wakuu wa idara..... yaani ukiangalia kuna mikurugenzi imekuwa kwenye mawizara huko miaka nenda rudi na kinachofanyika hakionekani... hujiulizi TCC, CRDB, TBL etc zimefanikiwa vipi na wale wakuu kule ni waTz kama mimi na wewe?!?! Kuna kitu kinaitwa REFORM ambacho tatizo ni kwamba serikali yetu tukufu haijajua kina maana gani.... Jamani reform sio kuweka new minister, total reform ni new PS, Directors and HODs ambao wao ndio wata drive the technical side ya wizara/idara zetu!!! Waziri apige gumzo siasani (duh si utani nadhani BAKITA hapo wamepata neno jipya) hawa nguvu na damu mupya wafanye majamboz!!!!!! Wakubwa mlione hili!!!

Nakubaliana nawe kuwa siasa siyo msingi wa maendeleo yetu. Utendaji wa dhati unaozingatia maadili na miiko yenye wito.
Muungwana safisha nyumba yako maana bado inanuka.
 
Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,696
1,681
Haya Papa Mkulu Mkulu Lunyungu, tumekusikia. Na huenda Pinda kwa kuwa ni Shushushu wa muda mrefu, basi huenda atatuletea watu safi kwa kuwa inaweza kuwa rahisi kwake kujua nani msafi na anyyweza na nani mchafu
 
Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,812
630
Mkuu Lunyungu,

Mimi nimeshakata na tiketi, nataka mkoa ulio nyuma kuliko yote na baada ya mwaka kama hakuna jipya basi niwe fired tena kwa kusulubiwa kwi kwi kwi!!!!

Hao jamaa hawawezi kutoa kazi kwa watu ambao hawatawapigia magoti. Wanataka watu ambao watatekeleza yale wanayoambiwa na wakubwa zao. Watu huru kama wengi hapa JF, hata siku moja hawawezi kufikiriwa!
 
Nalijua hii Mzee Mtanzania lakini wao katika kuchagua wanasema hawajali nini wala nini .So kaa mkao wa Kula unaweza kulamba Dume ukapelekwa Mtwara .
 
Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,276
115
Nalijua hii Mzee Mtanzania lakini wao katika kuchagua wanasema hawajali nini wala nini .So kaa mkao wa Kula unaweza kulamba Dume ukapelekwa Mtwara .

Lunyungu,

Tumefahamiana kwa siku nyingi mkuu katika masuala ya maisha kama haya tuweke tofauti pembeni pls kama una access huko penyeza jina langu I would prefer U-RC lakini kwa kuanzia hata U-DC sio mbaya

Kindly do the needful nakuamini
 
Majita

JF-Expert Member
Jan 13, 2008
609
186
Mimi habari hii imenifikia muda huu nami kwa kuwa comp yangu huzima saa nane usiku tu nikaona wacha nilete .Habari hizi zimetoka ndani kabisa watu wakiwa wana hahaha kutafuta connections.Nimeambiwa uteuzi wowote hawa angalii kigezo chochote bali ukipendwa unachukuliwa .Sasa zina ukweli kiasi gani ? Fungua macho na masikio nawe toka hapo ulipo ili sote tuanze kufuatilia hili .

Lakini nimesha penyeza zaidi vijana na by kesho ama kesho kutwa nitakupeni ukweli zaidi.Pamoja na haya naomba nyie mfanye kazi ya Ziada .

Ili uwapata watu wa maana na hasa walioko madarakani it is time now kuanza kujadili majina ya wakuu hawa.Kila mmoja na Mkoa wake ili kuona wamekuwa wakifanya nini tangia wamekuwa Wakuu na kama wana stahili kubakia .

Naanza nakuleta jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam .
Ndugu Abbas Kandoro.

In case of changes does he deserve to remain or he should go ?Mwenye data zake amwage na twenda Tanzania nzima tumsaidie PM Pinda kuwapindua .

Ni mbabe sana,dharau,mtu wa visasi,hapendi kuwa chini ya mtu,fitina,wivu,mchonganishi na kibaya elimu yake ya masters degree haimsaidii.Sakata lake wakati akiwa DC Singida na aliyekuwa mkuu wa polisi RPC S.Dau linathibitisha hilo.Ikumbukwe kuwa baada ya Singida aliamishiwa Tabora kuwa RC na baada ya muda mfupi kamanda Dau nae akaamishiwa Tabora kama RPC so akamkuta kandoro akiwa ndo bosi wa Tabora.Ilimchukua Dau miezi michache tu kuhamishiwa Reli kama kamanda wa Reli baada ya Kandoro kumkataa Tabora kutokana na visa vyao vya Singida.Alimwandikia mahita kuwa hamtaki Dau kwenye mkoa wake.
 
Ogah

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
6,227
1,518
Lunyungu,

Tumefahamiana kwa siku nyingi mkuu katika masuala ya maisha kama haya tuweke tofauti pembeni pls kama una access huko penyeza jina langu I would prefer U-RC lakini kwa kuanzia hata U-DC sio mbaya

Kindly do the needful nakuamini

....utani mwingine bwana.............kwi kwi kwi kwi
 
Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,164
UDC au URC umekaa sana kisiasa kuliko kiutendaji, kama mtu unadhani unafaa kuwa kiongozi kwa ajili ya maendeleo basi nafasi ya mkurugenzi I mean wa wilaya, manispaa au jiji ndio haswaa yenye impact.

Kuna wakati serikali ilitangaza kwamba wakurugenzi watapatikana kwa intavyuu I am not sure kama hiyo iko in place tayari.

Anyway kwa kijana kuwania UDC au URC mimi nadhani ni kujipeleka kudumaza akili yako na kuishi kama bootlicker maana anytime unaweza kuwa fired bila hata kuelezwa sababu. I am sorry siko tayari kwa any of the two!!!!!!!!! Ni mawazo yangu nawakilisha...........
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom