Tukio la kusikitisha Arusha leo

Tukio la kusikitisha Arusha leo

Sio kweli hospitali yenye vifaa vya kisasa na wataalam wenye viwango labda MOI ambayo nayo sio ya Serikali.

Nikiwa chuo Muhimbili mwaka 2007 mtoto wa kike wa miaka nane alikufa mbele ya lecturer mwenye PHD, madaktari na wanafunzi tukishuhudia kwa kukosa Oxygen, baadae mtungi uliletwa lakini ulikua wa kizamani ulikua unaitaji "spaner" ya kufungulia ili Oxygen itoke "spaner" haikuwepo mtungi haukufunguliwa na mtoto alifariki!

Sasa nafanya kazi wilayani sijawahi kuuona mtungi wa oxygen wala kusikia oxygen imeisha wanaenda kujaza!

Hii ndio TZ zaidi ya uijuavyo km unabisha pata ajali/ugua (emergency) halafu upelekwe hospitali ya serikali!
 
Kwani selian ni ya ccm..
Si wamejifanya hawataki hospitali yetu ya mount meru, baba lao arusha...sasa angalia wamempoteza mtanzania mwenzetu...na hapo hata udini utaibuka ...
Wewe sasa ndio unataka kuzua udini, tukio hilo ni uzembe tu uliokithiri kila mahali nchini kutokana na sera mbovu.
 
Jamani, kweli hili ni jambo la kusikitisha sana. Nawapa pole sana wafiwa. Hata hivyo naomba wa Tz wote tujiandae kwa mambo kama haya kwa sababu watu wengi wamepoteza uhai na wengine kupata ulemavu wa kudumu kwa sababu ya uzembe kama huu.


Lakini tatizo hili halianzii kwenye hospitali ama wahudumu wa afya. Linaanzia katika uzembe wa regulatory na supervisory systems za serikali. Kama vile serikali ilivyo na uzembe, katika idara zake zote, na hata haiwezi kusimamia wananchi na hivyo walaliswa sumu na kuathirika kwa namna nyingi tu.


Bila kuiondoa ccm madarakani, tutaendelea kuteketea ndugu zangu. Hakuna nchi iliyo na mfumo wa uongozi makini inayoweza kuruhusu wananchi wake wapate substandard na fatal services or products whether is from the Government or anybody.
Unachojaribu ni kulalama kwa propaganda dhidi ya CCM ambazo hazina hata mashiko.

Hivi unaijua supervisory na regulation iliyopo kati ya Selian hospital inayomilikiwa na KKKT na wajibu wa msingi wa Selian hospital ni upi.

Jenga hoja za maana kuliko kuanza kuficha uozo kwa manufaa yako au ya hospitali kisiasa.

We're talking someone died possibly, for negligence.

Kuna familia kwa sasa ina omboleza huku wewe ukilalama bila underlying support for argument.
 
Kwani selian ni ya ccm..
Si wamejifanya hawataki hospitali yetu ya mount meru, baba lao arusha...sasa angalia wamempoteza mtanzania mwenzetu...na hapo hata udini utaibuka ...

lazima uibuke we ujaona majina ya mgonjwa yalivyoandikwa.
 
Chagua CCM,
Chagua Matatizo!!

Weye ni hatari kama jina lako, CCM inahusikaje na hospital mali ya KKKT.

Mnaingiza mizaha hata kwenye serious issues. Gharama ya tiba waliyolipa hawa waathirika na huduma waliyopewa hailingani.

Uzembe kama huu kwa private hospital yenye huduma ghali kama hii haukubaliki.
 
Nesi aliyetoa tangazo la kwisha kwa oxygen ni mpumbavu! alitakiwa akae kimya mpaka wafike KCMC na daktari athibitishe kwamba mgonjwa alikuwa kafariki.
 
lazima uibuke we ujaona majina ya mgonjwa yalivyoandikwa.

Na haswaa ndiyo lengo la mleta thread hii si unaona na jina lake, anajaribu kutuonyesha kuwa mgonjwa alinyimwa hewa sababu ya dhehebu lake.

Ni lazima tumuonye. Waliompeleka mgonjwa kwenye hospitari hii walikuwa na imani na ubora wake. Hivyo tulaumu uzembe wa huduma na umakini ktk kazi. mtungi wa gesi una meter inayoonyesha ujazo kwanini hawakujua kuwa haitatosha?

Huu nu utapeli unaofanywana haspitali nyingi za binafsi, huduma ni za gharama lakini huduma mbovu.
 
Huduma za afya Tz ni mbovu, mbovu, mbovu hakuna mfano... Yaani zaidi ya 90% ya wagonjwa wanaofia hospitalini, ni kutokana na ubovu wa huduma!!!
 
Imekuwa hivo?? nilikuwa naiheshimu sana Seliani baada ya kumuokoa mwanangu kukatwa mguu, hoja iliyopendekwa na madaktari wa mount meru hospital,, itazamwe upya ni hospital nzuri sana!!
 
Ndugu wa marehemu ni kati ya kundi kubwa la wajinga wenye kuweka lawama mbele kuliko uhalisia...
Suala la oksijeni kupungua lipo nje ya uwezo wa hao wauguzi na hata dereva wa gari husika...
Swali la kwanza walitakiwa wajiulize, iweje hapo Arusha hakuna hospitali yenye hadhi kama KCMC maana ingalikuwepo hospitali ya hadhi hiyo basi huyo marehemu pengine angelikuwa hai...

Huwezi kumuita aliyefiwa mjinga!
Na walichikifanya maamuzi ambayo hufanywa kwa hasira za kuondokewa na mpendwa wao.
Na kusema suala la oxygen lkupungua liko nje ya muhudumu ! Ni point mbovu kabisa na muhudumu anhusika asilimia 100%.
Wewe kama muhudumu unapewa mgonjwa kupeleka masafa ya mbali. Ni wajibu wako kuhakikisha vifaa vyote ulipewa vitakufikisha huko uendako na kama huna oxygen ya kutosha wajibu wako ni kukataa kumchukua mgonjwa mpaka upewe kila kilicho muhimu.
Sasa kwa kuogopa kutia mchanga unga wake (kibarua) matokeo yake ameua!
Tena ana bahati yuko bongo ambako rushwa imetawala huyo nchi za haki zote au Europe hio ni manslaughter. Huyo nurse na boss wake na doctor aliye saini transfer wote ni kifungo cha miaka mingi mno.
Thamani ya binaadamu ni ndogo sana tz.
Wala msilete siasa kwenye hili janga.
 
Ndugu wa marehemu wanaweza kufungua case mahakamani na kuishitaki hospitali kwa kosa la professional negligence
 
Wanatia hasira sana hao wazembe kwani walikuwa hawajui kama O2 ilikuwa ndogo?
 
Utawala wa hospitali una mtu anayeshughulika na mitungi ya hewa ya oksijeni kwa nini safari ianze bila kuhakikisha kulikuwa na hewa ya kutosha kwenye mtungi? Je wenye mgonjwa ndio walilazimisha apelekwe KCMC? Tuweni makini tuwapo kazini.

Wafiwa poleni sana lakini kitendo mlichofanya sio kizuri!
 
Back
Top Bottom