Tukio la Bustani ya Edeni na uhalisia wa siasa

INRI

JF-Expert Member
Oct 5, 2017
1,326
2,294
Habarani wakuu!

Leo kipindi nimeamka asubuhi, nikawa natafakari juu ya yaliyotokea pale bustanini Eden na yanayotokea nchini katika uwanja wa siasa.

Kwanini nimehusihanisha matukio haya mawili kwa pamoja?

Kila mtu aliyesoma vizuri na kuelewa vitabu vya Bibilia na Quran, anaweza kuelewa nini namaanisha hapa.

Ipo hivi: Baada ya Hawa kutenda dhambi na baadae Adam, Mungu alipokuja kuwahoji walianza kumtupia kila mtu mpira kwa mwenzie. Adam akasema ni hawa, Eva kasema ni shetani, ilihali hawa wote wawili walitenda makosa kwa ihari yao na ufahamu.

Tukirudi kwenye ulimwengu wa siasa, kuna matukio mengi yametokea na tumeyaona nitataja baadhi ninayoyakumbuka.

1. Utekaji

Hapa watu baaadhi walitekwa na kuonekana, wengine hawakuonekana kabisa.

Walioonekana ni kina Roma mkatoliki, Mo dewji, Mdude chadema, Tito magoti, Masoud Kipanya et all.

Wasioonekana hadi leo Azory Gwanda, Ben Saanane na wengine siwafahamu.

2. Mashambulio kwa viongozi wa kisiasa
Hapa tuna Mh. Tundu Antipas Lissu, Mwiba mkuu wa serikali. Alipigwa Risasi mwilini 16, mchana wa saa saba bungeni akiwa anarudi nyumbani, sehemu yenye ulinzi 24/7 na kuna CCTV- cameras. Zilitolewa baada ya tukio.

Tuna madiwani na hadi leo tumesikia kuna viongozi wameshambuliwa vibaya huko mtwara, Ruangwa, Viongozi wa upinzani.

3. Mashambulio na Uharibifu wa mali na majengo
Hapa nakumbuka kuna shambulio la ofisi za uwakili za Shangazi Wakili msomi, Fatma Karume, Upanga, Dar es salaam. Zilipigwa BOMU.

Tuna Tukio la kuharibiwa ofisi za uwakili za wakili aliyekua anamuwakilisha Yusuf Manji.

Tuna tukio leo la kuchomwa moto ofisi za CHADEMA, Arusha.

Hayo yote nimetoa kama mfano hai kwa baadhi ya matukio yaliyotokea nchini kwenye hii awamu. Ni matukio mabaya na ni UOVU machoni pa Mungu kwani kuna watu wamepoteza maisha, wamelemaa, wamemwaga damu zao kwenye hayo matukio.

Cha ajabu
Kama ilivyo desturi ya mtenda dhambi kumsingizia shetani ilihali yeye kafanya yaani adam na hawa.

Huku kwetu wanasema ni upinzani ndio wanaratibu wenyewe kupata kitu wanakiita KICK. Ilihali inafahamika ni wao wamefanya kutokana na Jeshi la polisi kutobainj nani alihusika katika Matukio yote hayo niliyotaja.

Kingine ni kauli zinazotolewa na viongozi wa chama tawala, zinadhihirisha yanayotokea "MNAJUA DAWA YA MTU MSALITI JESHINI".

"MKISHINDWA KUDEAL NAO BUNGENI, TUTADEAL NAO MTAANI"

"ZITTO NI MSALITI ANAPASWA KUULIWA" UVCCM- CHAIRMAN, IRINGA.

MUSIBA ET ALL.

Lengo langu ilikuwa ni kuweka uhusiano juu ya watenda mabaya wanapojaribu kujitetea kwa kusingizia fulani ili kujisafisha.

Hatima ya wazazi wetu adam na hawa, walifukuzwa bustanini.

Hatima ya haya matukio ni jambo la muda lakini yataondoshwa waliyofanya haya kwa njia Mungu anayoona inafaa.

Muwe na siku njema.
 
Back
Top Bottom