SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,130
- 7,899
Haya mashindano aina ya African Football League ni rahisi kuona kwa nini huwa yanakwama sehemu nyingine na uwezekano wa kukwama hapa Africa tayari unaonekana.
Kutokana na mzozo wa kisiasa unaoendelea huko Mashariki ya Kati, mechi ya ufunguzi iligubikwa na viashiria vya kusapoti Palestina, kuanzia mabango yaliyoshikwa na mashabiki hadi ushangiliaji wa magoli wa wachezaji wa Al Ahly.
Tukumbuke mmoja wa wadhamini wakubwa wa AFL ni Saudi Arabia. Nimesoma mahali Israel wamewaambia raia wake waondoke Misri. Unadhani nini kinaenda kutokea katika mechi za Al Ahly pale Misri? Saudi Arabia wameamua kumwaga mapesa mengi katika soka duniani kote na hili linaleta mtafaruku huko Ulaya maana inaonyesha nyuma ya pazia kuna nia isiyo njema. Ni wiki iliyopita tu timu ya taifa ya Tanzania ilikwenda Saudi Arabia katikati ya ratiba ngumu za ligi na mashindano ya kimataifa, halafu eti tukacheza mechi ya kirafiki na Sudan. Safari ile ilikuwa na tija gani kwa timu? Mwisho wa siku wachezaji wanaonekana wameenda kwa shughuli za kiimani zaidi. Nitawaacha mconnect dots.
Moja ya maswali ya msingi ambayo Motsepe ilitakiwa kuulizwa ni utofauti utakaokuwepo kati ya mashindano haya mapya na mengine ya CAF hasa linapokuja suala la tabia mbovu ya nchi za Kaskazini katika mashindano ya CAF kuanzia uamuzi wa marefa, tabia za wachezaji uwanjani na mashabiki wao.
Kama mambo ni yale yale na kilichobadilika ni maslahi kuongezwa, linakuja swali, kwa nini hayo maslahi hayakupelekwa katika mashindano yaliyokuwepo na kuboresha tu taratibu? Ukiongeza timu zikawa 24, ina tofauti gani na group stage ya mashindano ya champions league? Kama bado tutaendelea kushuhudia mashabiki wanarusha mabomu ya moshi viwanjani pale timu zao zinapozidiwa, utofauti na hadhi iliyotegemewa ya mashindano haya haitakuwepo.
Haya mashindano yakionekana yameanzishwa yakiwa na agenda za siri nje ya mpira hayatafika mbali. Usishangae hata haya ya msimu huu wa kwanza yasifike mwisho.