Saudi Arabia wadhamini wakuu African Football League

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,663
4,875
Saudi Arabia imeingia kwenye ushirikiano wa kihistoria wa miaka mitano na soka la Afrika ukihusisha Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka la Saudi Arabia (SAFF).

Nukuu CAF | Mkataba uliosainiwa utazingatia mipango na maendeleo ya kiufundi na soka katika klabu na taifa, soka la wanawake, kusaka vipaji, mashindano, michezo ya kirafiki na fursa za kibiashara,”

Makubaliano mengine ya CAF ni juu ya kampeni ya Visit Saudi, mkataba unaosimamia kutangaza utalii nchini Saudi Arabia ambao ni wafadhili wakuu wa African Football League (AFL) itakayoanza Oktoba 20 hadi Novemba 11, 2023 ikihusisha vilabu nane bora barani Afrika.
 
Hakuna vipaji wala nn ...waarabu wanataka kutrend kupitia mpira by hook and crooks
Kweli na wamefanikiwa kikubwa baada ya kuambiwa mafuta yataisha siku moja
Ila kila kitu wamepeleka huko
Na wana ushindani SA na UAE na Qatar
Kila mmoja anataka aonekane yuko juu
Grand prix pia na mengine mengi
 
Back
Top Bottom